Tundu Lissu akirudi nchini itakuwa kama George Floyd, Tanzania itazizima

Tundu Lissu akirudi nchini itakuwa kama George Floyd, Tanzania itazizima

Kitendo cha Tundu Lissu kusema atakuja kugombea urais kimewavuruga sana CCM hasa jiwe, nina hakika akija tena kugombea urais itakuwa ni kama Lionel Messi kuingia uwanjani dakika 15 za mwisho, huku CCM ikiwa inaongoza bao moja kwa ulinzi wa vyombo vya dola na tume ya uchaguzi. Inabidi mtu mwingine awekwe kama backup iwapo Lissu atafungwa, maana hiyo ndio njia pekee ya jiwe iliyobakia. Nashauri Zitto Kabwe maana ana uwezo mzuri wa kujenga hoja, na zikaeleweka kwa wananchi.
Happy usitegemee wanasiasa tena. Kuna uwezekano tuka record risasi au bomu la Kwanza kupinga ukandamizaji
 
Natabiri Lisu akirudi atapokelewa na raia wachache kuliko walio ipokea ile Bombardier ya kwanza
 
Kila siku najisema wazi mimi ni MwanaCCM na sidanganyi lakini. Pia nakubali JPM anafanya vizuri ndiyoooooo (lakini ni kwenye jambo moja tu may be macro economics) lakini kuna mambo ameharibu sana (kuminya demokrasia, nepotism, rushwa kwa wapendwa wake imekithiri, wafanyakazi ndiyo nyang'anyng'a usiseme kabisa, kulinda uovu fulani, ubabe, kutozuia au hata kukemea tu mauaji yanayofanywa na wasiojulikana, kutotia neno TL alipopigwa risasi, kufunga gerezani wapinzani, kuharibu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, n.k). Kwa hakika ameharibu sana sana hapo.

Sasa jana Mnyika kanikosha, tena kanikosha sana. Iwapo Tundu Lisu atatia nia mara moja atabadilisha upepo wa kisiasa nchini ingawa najua fika atakapofika tu watamkamata. Wakimkamata hapo sasa ndiyo mzimu George Floyd utaanza Tanzania. Ni MCCM lkn sitaogopa kitu, nitaomba Mungu TL awe ndani mpaka siku ya kura. Tutampigia Kampeni akiwa ndani. Hatutaogopa Mapolisi - hatutaogopa virungu vyao na wala risasi zao.

Moja ya slogan ya Kampeni itakuwa ni kumwachia Rais wetu awe huru. Najua uongozi wa sasa hautakuwa tayari kumwachia Lisu kwa namana yeyote ile na hapo itakuwa ni kama Mungu katusikia maombi yetu kwa sababu hilo watakalofanya ndilo litakalowapotezea kura.

Serikali hii sio tu kuwa ni ya kibabe lakini pia haina hata upendo na watu wake kwa sababu sikio lao linataka nyimbo tamu tu na hawataki kukosolewa. Juzi nimeacha kubeaba kadi yangu ya CCM lkn sasa kama Tundu Lisu akija na akawekewa vikwazo ndipo nitaichoma kabisa kadi hiyo.

Agosti sio mbali - imebaki miezi miwili tu. CHADEMA nawaomba pls pls watia nia waruhusiwe wajiseme hadharani na mfuate utaratibu kama mlivyoweka. Jitahidi msitoe Mgombea nje ya Chama this time. Tunamtaka Tundu Lissu. Hata huku huku CCM baadhi tunanyanyasika. Tena tunanyanyasika sana. Tumewachoka hawa wagawana Tausi wa Ikulu.

Tunataka mabadiliko ili wananchi na wafanyakazi wa kawaida mafurahie uhuru wa nchi yao. Midege na mitreni ya mwendo kasi sio ugali. Mi fly ova ya Ubungo sio pembejeo za kilimo za Idukilo. Mivyeo inayotolewa kwa wanajeshi sio nyongeza ya mishahara kwa wafanyazi wengine.

Tunamtaka Tundu Lissu nchi hii ibadilike. Tumechoka kunyimwa hewa ya kukosa demokrasia. We can't breath!
Naona unatumia muda mwingi kurudia rudia kuwa wewe ni CCM???
unafikiri Ngombe hata akirudia mara Elfu kuwa yeye ni Simba atabadilika na kuwa Simba??? Bora ungestick kwenye hoja yako na sio kutumia muda mwingi kujibadilisha kitu ambacho hakikusaidii chochote....

Turudi kwenye hoja; wewe unaonekana msomi ila hutumii Elimu yako vizuri bali unatumia hisia kitu ambacho sio sawa; Acha wale ambao hawajabahatika kupata elimu wachambue hivyo ila kwa uchambuzi wako ndio mnafanya wasomi wa siku hizi wasipate sifa stahiki au kwa lugha nyingine wadharauliwe!!!
 
IMG_20200601_122407.jpeg
 
Kwa mwenye Akili timamu kabisa na zinazomtosha Kichwani akiyasoma haya Maelezo yako itakuwa ni ngumu Kuamini Wewe ni mwana CCM hasa.
 
Natabiri Lisu akirudi atapokelewa na raia wachache kuliko walio ipokea ile Bombardier ya kwanza
Wala hawatakiwi watu wengi kwenda kumpokea. Kinachotakiwa ni maneno yake ya kuondosha ukandamizaji wa demokrasia wakati wa Kampeni zake
 
Kwa mwenye Akili timamu kabisa na zinazomtosha Kichwani akiyasoma haya Maelezo yako itakuwa ni ngumu Kuamini Wewe ni mwana CCM hasa.
Naona unatumia muda mwingi kurudia rudia kuwa wewe ni CCM???
unafikiri Ngombe hata akirudia mara Elfu kuwa yeye ni Simba atabadilika na kuwa Simba??? Bora ungestick kwenye hoja yako na sio kutumia muda mwingi kujibadilisha kitu ambacho hakikusaidii chochote....

Turudi kwenye hoja; wewe unaonekana msomi ila hutumii Elimu yako vizuri bali unatumia hisia kitu ambacho sio sawa; Acha wale ambao hawajabahatika kupata elimu wachambue hivyo ila kwa uchambuzi wako ndio mnafanya wasomi wa siku hizi wasipate sifa stahiki au kwa lugha nyingine wadharauliwe!!!
Msomi wewe hapo!
 
Back
Top Bottom