The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Kutoka viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam tunakusogezea kuona jinsi msafara uliomleta Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu alivyoingia Mahakamani hapo mapema leo, Jumatano Septemba 10.2025
Lissu ambaye amefikishwa Mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Jeshi la Magereza, ameletwa kwa ajili ya mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili ambapo Mahakama chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Ndunguru kwa siku ya tatu mfululizo inaendelea kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwa na mshtakiwa.
Chanzo: Jambo Tv