Tundu Lissu akiwasili mahakamani kwa ulinzi mkali

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kutoka viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam tunakusogezea kuona jinsi msafara uliomleta Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu alivyoingia Mahakamani hapo mapema leo, Jumatano Septemba 10.2025

Lissu ambaye amefikishwa Mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Jeshi la Magereza, ameletwa kwa ajili ya mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili ambapo Mahakama chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Ndunguru kwa siku ya tatu mfululizo inaendelea kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwa na mshtakiwa.

Your browser is not able to display this video.
Chanzo: Jambo Tv
 
jamaa anakiona chamtema Kuni?
Ni mpango wa Mungu ili siku moja yatokee yaliyotokea Nepal

Huko Nepal, watawala walipofunga mitandao na kuminya haki za raia huku ufisadi ukishika kasi, hawakujui nini kitatokea.

Huko Nepal waziri kadakwa kabaki na kichupi huko wengine wakitoroko na helicopter.

Nepal raia waliitwa waoga, ila watu walipochoka, waoga hao waligeuka kuwa ni watu hatari na wakakomboa nchi yao.

Elewa tu ni lazima ukandamizaji , uonevu, wizi na rushwa vitangulie kabla ya raia kuingia mabarabarani.

CCM inapita mule mule ila watawala hawawezi kuelewa until it is too late.
 


Kuelewa what is cooking up, kutokana na ushenzi unaowanyia watu, inahitajika uwe na akili japo kidogo. Sasa hawa wa kwetu, wapo wenye hiyo akili?
 
Hilo basi la mahabusu au wenye kesi unaweza kukuta wamepanda wote Askari magereza
Nao kumbe wafungwa
 
Na Kisutu ingekuwa mchakamchaka kama hivi,hii mbungi ingeshaisha labda angekuwa ashakata na rufaa au angekuwa mtaani kitambo.
 
Waafrikia tuna shida sana. something is wrong somewhere. Mioyo yetu imejaa giza, midomo yetu imejaa uongo na akili zetu ziko polluted kama vile hazifanyi kazi vizuri. We can not achieve anaything kwa jinsi hii. Tunahitaji mageuzi ya akili na fikra jinsi ya kupambanua vitu ili tuwe na mazingara rafiki ya kuendeleza nchi zetu hizi zinzoitwa bara la giza. Kwa jinsi hii tutaendelea kungangania madaraka kwa ajili ya umaskini na kuua wengine bila sababu ili mimi na watoto wangu tuishi vizuri bila kujua kwamba yote hayo yatageuka siku moja maana huwezi kuwa tajiri among the poor people wakuache salama. Mwisho wa yote tujue kuna Mungu mbinguni anayeona yote unayonfanyia mwenzako au jirani yako yawe mema au mabaya. Tujifunze kutenda mema siku zote na wewe ambaye umeamua kutenda mabaya endelea tu maana there is a day that you will face the consequences of you wrong doings.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…