Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Chadema wamekiua chama wao wenyewe sasa ruzuku sijui itakuwa shs ngapi?
hawatapata hata sent mkuu, sisi wana CCM tumefurahi sana kwa kweli . maana walikuwa wanakwamisha sana MAENDELEO. Tuwaache wapinzani wajifie kwa NJAA sisi ni muda wetu sasa kuwaletea wananchi maendeleo. Tumechelewa sana miaka 50 ya Uhuru wapinzani wametukwamisha sana sasa hivi tungekuwa mbali sana kimaendeleo zaidi ya California
 
Sawa bhana asante kwa kupanua Hilo domo lako linalotoa harufu.

Mmewamliza wapinzani Sasa jengeni nchi maana wapinzani walichelewesha Sana maendeleo Sasa yanini maneno?
 
MsemajiUkweli naona Kama unawaongezea dozi ikiwa hata kupona bado
 
hivi we kwa akili yako unaona kabisa kina mbowe lema heche msigwa na wengineo walishindwa uchaguzi?
 
mkuu hebu tuwaache CHADEMA wajifie bwana. Sisi wanachi tuliwakataa kwenye BOX LA KURA. Wewe unataka lissu awarudishe bungeni yeye kama nani. Achana naye huyo BEBERU.
 
Mtu bora kisiasa ni yule yuko Ikulu!

Maandamano yanayofuata taratibu na sheria za nchi sio jinai! Kinyume cha hivyo ni jinai!
 
Jibu swali! Alisema atawaingiza watz barabarani na hatakubali? Mbona yeye ndiyo amekuwa wa kwanza kukimbia kwenda ubalozi wa Ujerumani na baadaye kwao Ubelgiji??

Kwa jinsi Policcm walivyojiandaa Kuua walitumia busara....Kupambana na viongozi walafi wa kiafrika inahitaji "TIMING".....Kupambana na MADIKTEKA ni lazima uwashirikishe "MABEBERU" aka WAHISANI ....Madikteka wakisagiwa kunguni na kuminywa MBUPU na MABEBERU huwa wanasalimu amri.
 
".... mwenyekiti (mbowe ) mwenyewe ana elimu ya magumashi"- Zitto

".....Anayeamini maneno ya Mwenyekiti Mbowe 100% inabidi apelekwe Mirembe"
Bora elimu ya magumashi yenye faida kuliko elimu yako ya first class ya kusujudu upuuzi wa lumumba na kulamba matter call ya "MEKO".
 
NI MPUMBAVU WA KIWANGO KILICHOTUKUKA ANAYEWEZA AMINI KUWA ANGUKO LA CHADEMA LIMESABABISHWA NA LISSU.

Kwa wenye upeo wa kutosha wanafahamu kuwa;

Sheria za uchaguzi ziliwekwa dakika za majeruhi kuwezesha wizi wa kura!

Uchaguzi ulihujumiwa hata kabla haujafanyika na matokeo kupangwa.

Kauli na matendo ya viongozi na wana ccm yanaonyesha nini kilitarajiwa(rejea kauli ya bashiru juu ya chama dola kushindwa uchaguzi ).
Kiapo cha "jiwe" kufuta upinzani kufikia 2020.

Madhila na maudhi dhidi ya viongozi wa CDM (Mbowe,Lema,Lissu,n.k)tangu magufuli aingie madarakani ni ishara tosha ya nia ovu.

HITIMISHO:
Yaliyojiri uchaguzi 2020 yanajulikana kwa wote.Hujuma na uhuni wote uliofanywa wajulikana kwa wote(wapinzani na wana ccm). Bali ni wakweli na wanyoofu tu ndiyo wanaweza kukiri wazi wazi.Na wanafiki na wasio na chembe ya ustaarabu tu ndiyo wanaweza kusifia na kupongeza.

Tusubiri muda ndiyo utasema nani yu sahihi na nani ni tapeli baada ya baradhuli kukamata hatamu.
 
Cha kustaajabisha hata udiwani karibu halmashauri zote mmechukua nyie hii ni remarkable!

Yani hata kwenye vitongoji huko wananchi hawakuangalia mtu mmoja mmoja!
 

Kwani CHADEMA wana mbunge? CHADEMA hawayatambui matokeo ya uchaguzi huo.

Mbona mnajishaua shaua hivyo?
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nini?
Point noted
 
Heshma ya pekee kwa aliyekuwa katibu mkuu wangu Dr Slaa👍👏
Yeye alikua mzalendo aliyealiyejua maana halisi ya demokrasia ya vyama vingi💥
 
Heshma ya pekee kwa aliyekuwa katibu mkuu wangu Dr Slaa👍👏
Yeye alikua mzalendo aliyealiyejua maana halisi ya demokrasia ya vyama vingi💥
Kwa utawala wa jpm hata yy angefeli tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…