Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Hapa waswahili wanasema umegonga kunako...
 
Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!
Taarifa za awali zilisema ana tiketi ya ndege ya tarehe za mwezi Desemba, ghafla kapata ya mwezi November! Salary Slip anajuta kumfahamu Antipasu. Alivyomtosa ezi za MIGA na acacia somo hakulielewa...kwa sasa atakuwa amemuelewa Antipasu vinginevyo awe amekodi IQ yake kwa muda huu.
 
Kwa sababu ya uharibifu mkubwa ajabu wa uchaguzi uliofanywa na dola kwa niaba ya CCM!.

Uchaguzi uliopita ni Uhaini dhidi ya Jamhuri ya Muungano na Watu wake!
Mkuu Missile of the Nation, alichoandika Msemaji Kweli ni hitimisho la kile nilichokuwa naamini na kukisitiza humu JF kuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la upinzani Lissu amepigilia.

Mimi ni mpinzani wa demokrasia ya vyama vingi kwenye nchi maskini. Ni moja ya njia inayotumika na mataifa makubwa (mabeberu) kutawala nchi hizo kwa kuwagawa kimawazo, kifikra na kiutendaji - yaani "Divide and Rule”.

Toka kuanzishwa kwa vyama vingi 1992, kumekuwepo na msuguano ukikwamisha maendeleo. Viongozi wa upinzani wakitumika kukwamisha maendeleo. Wengi wao, bila kujitambua au kwa makusudi, waliamini kusifia mazuri yanayofanywa na Serikali ya Chama Tawala ni kukipa kiki ya kisiasa hivyo basi wamejikuta wakifanya kila hila kukwamisha maendeleo. Hili limekuwa bayana katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano iliyopiga marufuku siasa za majukwaani ili wananchi wachape kazi. Matokeo yake kila mtu ameona.

Sasa wafuasi wa upinzani, kama wewe Missile of the Nation na wenzio, mtaishia kujaza mitandao ya kijamii na lugha za kulaani, kuomba dua, na kila aina ya kufuru na kafara. Mnapaswa kutambua kuwa, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vyama vingi, Tanzania inakuwa salama na maendeleo yatakuwa kwa kasi. Nanyi vizabinazabina mtafaidi matunda yake.

Hatimaye wasaliti wamejitokomeza wenyewe kwa kujilipua kabisa na waliobaki wasamehewe tu makosa yao kwa kuwa wanaishi kwa fikira tegemezi.
 

Aliingia madarakani nchi ikiwa na demokrasia ya kuridhisha, hivi sasa anapanga matokeo yawe vipi akiwa ikulu. Hakukuwa na wakimbizi wa kisiasa, ila sasa hivi wapo. Nchi aliikuta ikiwa na mijadala na midahalo, sasa hivi kawageuza wananchi makondoo wa kuhutubiwa na kushurutishwa kutawaliwa. Alikuta nchi ina deni la chini ya 40t kutokana na marais wote wanne, sasa ni zaidi ya 56t ndani ya miaka mitano! Yale makundi ya watu wasiojulikana yaliyokuwa tunayasikia huko Rwanda, sasa hivi ndio yanatamba hapa kwetu. Data nyingi huko nyuma zilikuwa ni za kweli kwa kiwango cha kuridhisha, ila sasa hivi upishi wa data ili kuhadaa wananchi ndio fashion. Samahani kama niko nje ya mada.
 
Kwa ule umwagaji wa damu na kura kwenye mabeg, nikisikia neno aibu nacheka kwa nguvu.
Haya mambo kama yana ukweli yasiishie kwenye mitandao, mpaka sasa ni kupost Twitter na JF inatakiwa hatua stahiki zichukuliwe tuambiwe ilitokea nini hiyo tar 27/28 mpaka watu wakapigwa risasi.

Ipo tume ya haki za binadamu,mahakama zipo n.k
 
Yupi Bora?Je,ni aliyeahidi kuwaingiza wananchi barabarani ama anayetishia,kupiga ama kuua waandamanaji?Maandamano ni jinai kwa sheria za Tanzania? Je,kosa la kuandamana hukumu/adhabu yake ni kuuawa?
CCM imepata ilichokitaka,wabunge,madiwani na Rais,tuleteeni maisha bora/maendeleo kama Ulaya/Dubai,acheni choko choko dhidi ya wapinzani (CDM/ACT/CUF).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…