Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Kuna usemi unasema 'Mwosha naye huoshwa!'.....Nina amini kabisa kuwa ipo siku CCM pia itafutwa na kufutika ghafla hivihivi, tena itakuwa ni zaidi ya ilivyofanya kwa vyama vya upinzani!
Haikatazwi, Ila si mwenendo na Sera za Chama cha watoto Chadema!
 
Kwanini mlishiriki uchaguzi wakati mnajua Tume ni ile ile ya Uchaguzi mlioisusia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa? Hamkujua kuwa mtaibiwa au kuonewa?
Bora wameshiriki na matatizo ya kikatiba yanayowakabili wapinzani yamebainika na kujlikana na ulimwengu wote! Tujiulize je wasingeshiriki uchaguzi ule wizi wa kura uliobainishwa ungejulikana vipi??
Zaidi ya yote unapokuja na hoja kama hiyo ni lazima ukumbuke kuwa Tanzania kuna vyama vya siasa vingine ni vibaraka wa chama tawala, na ubaya zaidi ni vingi kwa idadi , vipo zaidi ya 9!
Sasa ukisema CHADEMA, ACT wazalendo wasishiriki uchaguzi alafu hivyo vikashiri, itahesabika uchaguzi ulihusisha vyama vya upinzani, na riport zitatolewa na kusema ulikuwa huru na wa haki! Je faida ya kutoshiriki ni ipi? Je imekula kwa nani kama sio kwa waliosusa??
 
Jamaa hata mwezi haujaisha baada ya uchaguzi ameamua kuwakimbia makamanda ''maandazi''!
wakina Ponda na Bagonza kama viongozi wa dini wameshindwa kabisa kipewa maono na Mungu kujua nia mbaya ya Lissu kitumiwa na mabeberu.
 
Dr Slaa anabaki kukumbukwa kama kiongozi shujaa, imara na mzalendo aliyewahi kutokea chadema
Chadema iling'ra sana enzi zake kwa misingi imara aliyoiweka na kuisimamia
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu.

Matokeo yake amekuwa ni kati ya wanasiasa ambao wameididimiza CHADEMA kimaslahi huku yeye akiamua kwenda kupata ''income support'' nchi za watu.

Kelele za ''mtaalam wa sheria'' kwenye majukwaa zilikuwa ni nyingi huku akiwaaminisha anaenda Ikulu lakini ufanisi ni zero.

Tukumbuke kuwa, Mwaka 2005, ''Mzee wa anga'' aliikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 4 na baada ya Uchaguzi akaiacha ina wabunge 5.

Mwaka 2010, ''Baba Paroko'' akaikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 5 na baada ya uchaguzi aliiacha ina wabunge 48.

Mwaka 2015, ''Fisadi Papa'' akajitosa na kuikuta CHADEMA ina wabunge 48 na kuiacha ina wabunge 70.

Mwaka huu, ''Mtaalam wa sheria'' ameikuta CHADEMA ina wabunge zaidi ya 50 na ameiacha ina mbunge 1 ambaye kwa aibu hataki kumtambua!

Unaweza kusema lolote au kuchanganua na kuchambua lakini ukweli utabaki palepale kuwa amekuwa ni mmoja wa watu walioiporomosha CHADEMA kimapato na kuikimbia haraka sana!

''Fisadi Papa'' ilimchukua miaka 4 baada ya uchaguzi Mkuu kuikimbia CHADEMA, huyu ''Mtaalam wa sheria'' hata mwezi mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu haujaisha ameamua kuikimbia CHADEMA!

Wafuasi wake ''maandazi'' walituaminisha huyu ''mtaalam wa sheria'' sio kama ''Fisadi Papa'' kwa sababu ni jasiri na kwa maana hiyo ''chama cha kijani'' kisimpuuzwe!

Thread zilijazana hapa Jamiiforums za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' kwa ujasiri na nguvu za kisiasa alizonazo huku mgombea wa ''chama cha kijani'' akiambiwa ajiandae kukabidhi Ikulu kwa kupenda au kutopenda baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!

Hizi ni baadhi ya thread za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' ambaye alikimbilia kwenye majengo ya balozi za Ulaya baada tu ya kumaliza kuitisha maandamano yasiyo na kikomo!

Kinachofurahisha zaidi, ameamua kukimbia bila kuwaeleza makamanda ''maandazi'' kama amesitisha maandamano au bado yapo palepale!

LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
Mmetumwa haondoki mtu..poleni sanaa
 
Bora wameshiriki na matatizo ya kikatiba yanayowakabili wapinzani yamebainika na kujlikana na ulimwengu wote! Tujiulize je wasingeshiriki uchaguzi ule wizi wa kura uliobainishwa ungejulikana vipi??
Zaidi ya yote unapokuja na hoja kama hiyo ni lazima ukumbuke kuwa Tanzania kuna vyama vya siasa vingine ni vibaraka wa chama tawala, na ubaya zaidi ni vingi kwa idadi , vipo zaidi ya 9!
Sasa ukisema CHADEMA, ACT wazalendo wasishiriki uchaguzi alafu hivyo vikashiri, itahesabika uchaguzi ulihusisha vyama vya upinzani, na riport zitatolewa na kusema ulikuwa huru na wa haki! Je faida ya kutoshiriki ni ipi? Je imekula kwa nani kama sio kwa waliosusa??
Kwani mliposusia Uchaguzi wa Serikali za mitaa mlipata faida ipi au hasara ipi? Kwani ACT NA CHADEMA mkisusia Uchaguzi ni lazima vyama vingine visusie? Kama vyama vyenu vinaona havitendewi haki kaeni pembeni
 
Aliingia madarakani nchi ikiwa na demokrasia ya kuridhisha, hivi sasa anapanga matokeo yawe vipi akiwa ikulu. Hakukuwa na wakimbizi wa kisiasa, ila sasa hivi wapo. Nchi aliikuta ikiwa na mijadala na midahalo, sasa hivi kawageuza wananchi makondoo wa kuhutubiwa na kushurutishwa kutawaliwa. Alikuta nchi ina deni la chini ya 40t kutokana na marais wote wanne, sasa ni zaidi ya 56t ndani ya miaka mitano! Yale makundi ya watu wasiojulikana yaliyokuwa tunayasikia huko Rwanda, sasa hivi ndio yanatamba hapa kwetu. Data nyingi huko nyuma zilikuwa ni za kweli kwa kiwango cha kuridhisha, ila sasa hivi upishi wa data ili kuhadaa wananchi ndio fashion. Samahani kama niko nje ya mada.
Mkuu hakuna namna yoyote ya kuhalalisha wenye fikira tegemezi kuwa wanastahili kuwa Asylum seekers!! Hao wanaona aibu na wanatafuta sababu za kuhalalisha unyonyaji wa kodi za wananchi wa nchi zinazo wahifadhi. Na hiyo wanafanya dhuluma na kupora haki ya wananchi wa nchi hizo kufaidi haki ya matumizi halala ya kodi zao. Lissu na wenzake waone aibu katika hili!!!

Ninyi si mnasema hakuna jambo la kuzuia raia zaidi ya milioni 40 kudai haki yao hata litumike jeshi la aina gani! Mimi pia nakubaliana na ninyi kwenye hilo. Sasa kama kweli ongozeko la deni la taifa kwa muda mfupi lingekuwa la kutilia mashaka na hakuna haki imetendeka....unadhani serikali ya awamu ya tano ya nchi yetu ingehimili nguvu ya umma ya watu milioni zaidi ya arobaini kupinga ongozeko hilo kama kunge kuwa na mangumashi? Ukweli watanzania wanaona ela zinaelekea wapi na matunda wanayaona! Na hiki ndicho kisa cha matokeo ya uchaguzi ya mwaka huu. Unata hivyo hivyo hutaki hivyo!

Mkuu, wewe ni mmoja ya wale ambao hawakuathiriwa sana na tabia za Antipasu za uongo . Mara kadhaa umeonyesha objectivity kwenye kutoa maoni. Sasa umekwama wapi kiasi cha kutotambua kabla haya niliyoeleza hapo juu!? Mkuu ebu weka mambo sawa usiniangushe.
 
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu.

Matokeo yake amekuwa ni kati ya wanasiasa ambao wameididimiza CHADEMA kimaslahi huku yeye akiamua kwenda kupata ''income support'' nchi za watu.

Kelele za ''mtaalam wa sheria'' kwenye majukwaa zilikuwa ni nyingi huku akiwaaminisha anaenda Ikulu lakini ufanisi ni zero.

Tukumbuke kuwa, Mwaka 2005, ''Mzee wa anga'' aliikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 4 na baada ya Uchaguzi akaiacha ina wabunge 5.

Mwaka 2010, ''Baba Paroko'' akaikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 5 na baada ya uchaguzi aliiacha ina wabunge 48.

Mwaka 2015, ''Fisadi Papa'' akajitosa na kuikuta CHADEMA ina wabunge 48 na kuiacha ina wabunge 70.

Mwaka huu, ''Mtaalam wa sheria'' ameikuta CHADEMA ina wabunge zaidi ya 50 na ameiacha ina mbunge 1 ambaye kwa aibu hataki kumtambua!

Unaweza kusema lolote au kuchanganua na kuchambua lakini ukweli utabaki palepale kuwa amekuwa ni mmoja wa watu walioiporomosha CHADEMA kimapato na kuikimbia haraka sana!

''Fisadi Papa'' ilimchukua miaka 4 baada ya uchaguzi Mkuu kuikimbia CHADEMA, huyu ''Mtaalam wa sheria'' hata mwezi mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu haujaisha ameamua kuikimbia CHADEMA!

Wafuasi wake ''maandazi'' walituaminisha huyu ''mtaalam wa sheria'' sio kama ''Fisadi Papa'' kwa sababu ni jasiri na kwa maana hiyo ''chama cha kijani'' kisimpuuzwe!

Thread zilijazana hapa Jamiiforums za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' kwa ujasiri na nguvu za kisiasa alizonazo huku mgombea wa ''chama cha kijani'' akiambiwa ajiandae kukabidhi Ikulu kwa kupenda au kutopenda baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!

Hizi ni baadhi ya thread za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' ambaye alikimbilia kwenye majengo ya balozi za Ulaya baada tu ya kumaliza kuitisha maandamano yasiyo na kikomo!

Kinachofurahisha zaidi, ameamua kukimbia bila kuwaeleza makamanda ''maandazi'' kama amesitisha maandamano au bado yapo palepale!

LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
walikuja na kamsemo kao eti "Ni yeye'
 
Ndio ukichokaririshwa kisha unakitumia kujenga hoja na wanaume?
😂 Kila utakapotaka kuwa na wazo la kutaka kuniandika Kwa maneno ya kunikejeli, hutaandika vizuri mkuu,Embu cheki ulichokiandika sasa!

Tysitukanane bhana!! Haifai mkuu!
Si vizuri kutafutiana ligi kiongozi
 
Mleta mada ungekuwa na akili timamu ningekushauri kitu. Ila elewa kuwa;
Uchaguzi ungekuwa huru kwa kuheshimu kura za wapiga kura CDM ingekuwa na wabunge zaidi ya 60.
Kura za Lissu 'zingepindua meza', amini maneno yangu.

Tundu Lisu aliwaahidi nini kuhusu huko mnakokuita ,,kuibiwa kura zake '' ?
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nn ?
Zile mbwembwe na kejeli walizokua wanatoa, unataka waachwe hivi hivi kwanni? Lazima waambiwe ukweli.
 
Mkuu hakuna namna yoyote ya kuhalalisha wenye fikira tegemezi kuwa wanastahili kuwa Asylum seekers!! Hao wanaona aibu na wanatafuta sababu za kuhalalisha unyonyaji wa kodi za wananchi wa nchi zinazo wahifadhi. Na hiyo wanafanya dhuluma na kupora haki ya wananchi wa nchi hizo kufaidi haki ya matumizi halala ya kodi zao. Lissu na wenzake waone aibu katika hili!!!

Ninyi si mnasema hakuna jambo la kuzuia raia zaidi ya milioni 40 kudai haki yao hata litumike jeshi la aina gani! Mimi pia nakubaliana na ninyi kwenye hilo. Sasa kama kweli ongozeko la deni la taifa kwa muda mfupi lingekuwa la kutilia mashaka na hakuna haki imetendeka....unadhani serikali ya awamu ya tano ya nchi yetu ingehimili nguvu ya umma ya watu milioni zaidi ya arobaini kupinga ongozeko hilo kama kunge kuwa na mangumashi? Ukweli watanzania wanaona ela zinaelekea wapi na matunda wanayaona! Na hiki ndicho kisa cha matokeo ya uchaguzi ya mwaka huu. Unata hivyo hivyo hutaki hivyo!

Mkuu, wewe ni mmoja ya wale ambao hawakuathiriwa sana na tabia za Antipasu za uongo . Mara kadhaa umeonyesha objectivity kwenye kutoa maoni. Sasa umekwama wapi kiasi cha kutotambua kabla haya niliyoeleza hapo juu!? Mkuu ebu weka mambo sawa usiniangushe.

Waalimu kila siku wanalalamika kunyimwa haki zao pamoja na mazingira duni ya kazi, ni lini wameandamana kupinga hali hiyo, au kutokuandamana kwao ni kuridhika na hali yao? Kwani kuandamana ni lazima iwe sasa tu? Huko Egypt na Sudan walikuwa wakilalamikia kuongozwa kibabe bila ridhaa yao, mbona viongozi wao walikaa madarakani zaidi ya miaka 30, wakiwatesa wananchi wao mpaka ikafikia tamati? Alichofanya Lisu sasa ni kupanda mbegu ya kuondoa woga, hata kama hajafanikiwa sasa ni lazima mbegu hiyo iote. Hata kwenye mpira sio kila shuti linazaa goli, lakini ukweli ni kuwa anayejaribu ndie anayepata goli.

Watanzania wangekuwa wanaridhika na hali ya mambo tusingeona 2/3 kutokujitokeza kupiga kura. Watanzania waliopiga kura hawazidi 1/3 ya waliostahili kupiga kura. Ni kwanini hawa wachache iwe kipimo cha kuridhika, na sio 2/3 ambayo hakujitokeza kupiga kura? Kilichofanyika kwenye uchaguzi huu tumekiona, kura za kwenye mabeg tumeziona, umwagaji damu tumeuona ili ccm kutangazwa washindi. Sasa sijui ni kipi mnataka kutuambia. Tuna imani ya hali ya juu na Lisu, na hata wakati wa kampeni tumejitokeza kwa wingi wetu kuonyesha kuwa tunamkubali na kuikubali cdm, lakini hatuna imani na mfumo wa uchaguzi. Na kwamba mfumo wetu uchaguzi hauminiki, hilo wala halina mjadala kwani limeonekana banana kwenye uchaguzi huu.
 
Katika kuishi kwangu, kumbukumbu zinaniambia hakuna mwaka taifa liliombea uchaguzi kama 2015
Chadema ilikua na ushawishi mkubwa karibia tuu na ilivyokuwa CCM.

Kwenye ibada za kuuga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 viongozi wa madhehebu yote, makanisani na misikitini waliukaribisha mwaka kwa maombi ya kumpata kiongozi sahihi wa kuongoza taifa hili.

2015 watanzania walikosa matumaini, imani kwa serikali ilipotea. Wengi walitegemea chadema chini msingi imara wa viongozi wake ingeinusuru nchi huku watanzania wakiombea taifakwa zaidi ya miezi9.

Ilipofika wakati wa teuzi kwenye vyama yaliyotokea ilikua miujiza ambayo hakuna aliyewahi kuwazia. Waliotegemewa kupata wakikosa na wasiotegemewa walitokea ghafla na kupata.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mngesusia Kama ambavyo mlisusia Uchaguzi wa Serikali za mitaa sababu mlisha doubt kuwa mtaibiwa

Tulisusa uchaguzi SM tukatarajia mmejirekebisha uchaguzi huu, lakini uchaguzi huu kila mtu kaona tulikuwa sahihi kususia uchaguzi ule. Tunataka kujua unataka tususe ili nini kitokee, nijue unachotaka kwenye hilo.
 
Back
Top Bottom