Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
CHADEMA ambayo ilikuwa inanufaika na ruzuku ya zaidi ya shilingi milioni 328 kwa mwezi imejikuta katika hali mbaya baada ya ''Mtaalam wa sheria'' kuwaaminisha wanaCHADEMA kuwa anakwenda siyo kuifanya ipate ruzuku zaidi bali pia kuifanya iingie Ikulu.

Baada tu ya kuwaaminisha, kelele zikawa kila kwenye ofisi ya CHADEMA na makamanda ''maandazi'' NI YEYE, NI YEYE

Matokeo yake amekuwa ni kati ya wanasiasa ambao wameididimiza CHADEMA kimaslahi huku yeye akiamua kwenda kupata ''income support'' nchi za watu.

Kelele za ''mtaalam wa sheria'' kwenye majukwaa zilikuwa ni nyingi huku akiwaaminisha anaenda Ikulu lakini ufanisi ni zero.

Tukumbuke kuwa, Mwaka 2005, ''Mzee wa anga'' aliikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 4 na baada ya Uchaguzi akaiacha ina wabunge 5.

Mwaka 2010, ''Baba Paroko'' akaikuta CHADEMA ikiwa na wabunge 5 na baada ya uchaguzi aliiacha ina wabunge 48.

Mwaka 2015, ''Fisadi Papa'' akajitosa na kuikuta CHADEMA ina wabunge 48 na kuiacha ina wabunge 70

Mwaka huu, ''Mtaalam wa sheria'' ameikuta CHADEMA ina wabunge zaidi ya 50 na ameiacha ina mbunge 1 ambaye kwa aibu hataki kumtambua!

Unaweza kusema lolote au kuchanganua na kuchambua lakini ukweli utabaki palepale kuwa amekuwa ni mmoja wa watu walioiporomosha CHADEMA kimapato na kuikimbia haraka sana!

''Fisadi Papa'' ilimchukua miaka 4 baada ya uchaguzi Mkuu kuikimbia CHADEMA, huyu ''Mtaalam wa sheria'' hata mwezi mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu haujaisha ameamua kuikimbia CHADEMA!

Wafuasi wake ''maandazi'' walituaminisha huyu ''mtaalam wa sheria'' sio kama ''Fisadi Papa'' kwa sababu ni jasiri na kwa maana hiyo ''chama cha kijani'' kisimpuuze!

Thread zilijazana hapa Jamiiforums za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' kwa ujasiri na nguvu za kisiasa alizonazo huku mgombea wa ''chama cha kijani'' akiambiwa ajiandae kukabidhi Ikulu kwa kupenda au kutopenda baada ya Uchaguzi Mkuu.

Mtu mwenye akili timamu atajiuliza, imekuwaje mtu aliyetuambia haogopi lolote akimbie haraka iwezekanavyo!

Hizi ni baadhi ya thread za kumsifia ''mtaalam wa sheria'' ambaye alikimbilia kwenye majengo ya balozi za Ulaya baada tu ya kumaliza kuitisha maandamano yasiyo na kikomo!

Kinachofurahisha zaidi, ameamua kukimbia bila kuwaeleza makamanda ''maandazi'' kama amesitisha maandamano au bado yapo palepale!

LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
LINK>>>
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nn ?
Hata mimi nawashangaa sana CHADEMA wanaojibu maongezi ya wanaCCM wakati wamewaacha waongee!

Kwa nini wanawafuatilia wanaCCM wanaoongea?
 
Mimi nawashangaa sana CCM. Wapinzani mmeshawamaliza hivi mnahangaika nao wa nini tena.? Tumewaacha muongoze mpaka mtakapo choka. Lakin bado tu mnawafuatilia wapinzani mnawataka wa nn ?
Tatizo la hawa maccm yanataka kuwaaminisha watu upuuzi wao kuwa ndiyo ukweli. Nafsi zinawasuta mno kuvikalia viti ambavyo siyo vya kwao.
 
ifike hatua tuache kuwalaumu wakina mbowe

Kwani hamumuoni anavyowafunga na kujinadi hadharani kuua upinzani

Shiiit
Wewe hujui lolote, hujasikia wanasema upinzani hauwezi kufa kwa sababu upinzani uko moyoni!

Ni upinzani gani huo umekufa wakati wapinzani wanatuambia upinzani haufi!
 
Back
Top Bottom