Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aliwahi kuisaidia nini Tanzania? Mwenye uelewa atuelezee

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aliwahi kuisaidia nini Tanzania? Mwenye uelewa atuelezee

20200731_211109.jpg
 
Uzwazwa ulionao ndio utakaufanya utakanwe mpaka uwakumbuke wazee wako kijijini, yaani mpaka leo hujajua umuhimu wa lissu? Kwanini hujiulizi kwanini walitaka kumuua mchana kweupe!?
Nadhani ungemjibu tu mkuu, angalia umri wake ni mdogo uelewa huenda pia mdogo.

Sababu ya kupigwa risasi sio msaada WENGINE wanapigwa kwa UGONI, na Makosa kadhaa.

Mjibu huyu naye ajue.

Mi najua alitusaidia kuingia mikataba ya Madini kwa machale na umakini maana alituambia tutashtakiwa MIGA huu umekuwa msaada mkubwa sana.

Mengine wataendelea kujazia
 
Uzwazwa ulionao ndio utakaufanya utakanwe mpaka uwakumbuke wazee wako kijijini, yaani mpaka leo hujajua umuhimu wa lissu? Kwanini hujiulizi kwanini walitaka kumuua mchana kweupe!?

Nimekusamehe kwa kuwa umejitanabahisha kwamba ulikuwa mtoto mdogo mwaka 1995. Ngoja nikueleze mambo matatu makubwa ambayo Tundu Lissu amelifanyia taifa hili:-

1. Wakati wa awamu ya 3 ya Mkapa Tundu Lissu ndiye alipinga vikali uanzishwaji wa shamba la kufuga prawns kwenye bonde la mto
Rufiji. Endapo shamba hili lingeanzishwa lingeharibu mazingira kwa kiasi kikubwa. Wakati TL anafanya jitihada hizi alikuwa hata
hajawa mbunge. Huyo mtu wako unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba uharibifu wa mazingira hayo ulikuwa haumhusu!

2. Kuanzia mwaka 2005 alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza hadi 2015, Tundu Lissu ndo alipinga vikali bungeni kuhusu
kupitishwa na kuwekwa saini mikataba mibaya ya madini ambayo ilikuwa inafanya Tanzania kama shamba la bibi. Wakati huo wabunge
wa CCM walikuwa wanasema 'ndiyoooooo' - wakati mikataba hiyo inapitishwa. Hata huyo unayemshabikia alikuwa bungeni lakini alikuwa bubu. Kwa taarifa yako, yale yote Tundu Lissu aliyokuwa anayepigia kelele ndo ambayo Rais Magufuli ameyachukua na kuyafanyia kazi.

3. Tundu Lissu ndo ambaye alipiga kelele bungeni kuhusu ufisadi mkubwa uliofanywa na viongozi wa CCM kuhusu EPA, Kagoda, Meremeta

Deep Green Finance, n.k. Wakati anaibua ufisadi huu, huyo unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba ufisadi huo haumhusu.
Nadhani sasa kijana unaweza kuona jinsi ambavyo Tundu Lissu alivyo mzalendo, mwenye uchungu na nchi yake.

Hitimisho: Si lazima uwe Rais ndo utoe mchango kwa nchi yako. Hapo nimekuonyea kwa ufupi tu jinsi ambavyo Tundu Lissu amelisaidia
taifa lake. Naamini sasa umemwelewa huyu mpambanaji na utampa kura ili awe Rais wa JMT, au siyo?
 
Ndugu wana bodi! Habari zenu!

Nikiwa kijana mdogo ,mwaka 1995 ,baba wa Taifa mwalimu Nyerere ,wakati akitueleza umuhimu wa uchaguzi na kuchagua viongozi bora wa taifa hili,alituasa kuwa ,tuchague viongozi watakao lisaidia taifa letu.

Mwalimu alisema kwamba ,miongoni mwa
siasa za kiongozi anayefaa kuwa Rais wa nchi hii,ni yule ambaye amewahi kuisaidia au kuifanyia maendeleo nchi yake ya Tanzania.

Tunapotaka kuchagua
kiongozi wa nchi hii ya Tanzania lazima tujue kuwa amewahi kuisaidia au kuifanyia nini cha maana nchi yake ya Tanzania.Mwalimu alienda mbali kwa kutoa mfano wa Rais

John F.Kennedy wa Marekani ,mwaka 1963 ,aliwaambia wamerekani ,wanataka awafanyie nini na sio wao wamfanyie nin.

Ni wakati muafaka kwa watanzania,kumuuliza ndugu Lissu ,JE amewahi kuifanyia au kuisadia nini Tanzania mpaka agombea cheo kikubwa kama urais?
Maana mimi naona kama amekuwa mtu wa kashifa tu.Je tutaongozwa kwa kashifa na kufika uchumi wa juu?Tumchague sasa DR MAGUFULI ILI ATUPELEKE
UCHUMI WA JUU.

Naomba tujenge hoja.TUACHE MATUSI :

Kwa miaka 27, mfungwa Nelson Mandela alihangaika na kufungwa jela kwa miaka 27 akifanya jitihada za kuamsha umma wa wa Afrika kusini kuleta demokrasia nchini humo. Mwaka 1985 ungemuuliza mtu hasa wa aina yako kuwa Nelson Mandela kaifanyia nini Afrika ya Kusini ili tumuunge mkono? Nadhani ungehangaika kupata jibu! Pengine ungempa maksi nyingi Peter Boath kwani kajenga viwanda vingi Afrika kusini, bara bara, fly over, nuklia, mandege na kukuza uchumi.

Lakini bahati nzuri mwaka 1994 chama cha Peter Boath kikishiriki uchaguzi dhidi ya Nelson Mandela, chama cha Peter Boath kikashindwa vibaya sana licha ya maendeleo makubwa iliyofanya.

Jibu langu lilikuwa moja tu katika mchakato ule: Kikubwa zaidi katika siasa ni ushawishi wa kukuza kiwango cha akili ya wananchi kufikiri na kuelewa chanzo cha matatizo yao. Kama tunakubali kuwa kuwa AKILI NI MALI, basi huko ndiko kwa kuanzia kama tunataka kupambana na adui wa wananchi.

Hitimisho: Kikubwa alichofanya Lissu ni kuwaamsha wananchi kujua adui wa matatizo yao/ ugonjwa sugu usiotibika kwa zaidi ya miaka 50. Leo mwananchi anajivuna kuwa na jibu na mwarobaini wa kutibu gonjwa/cancer hiyo. M Mungu akupe nini zaidi ya hilo!!!
 
Labfa tu juzi akiwa Kenya ametusaidia anasema mna CORONA vaaeni barakoa, Lockdown, tupime kila wakati, ila dawa hakuna.
Ila hata yeye aliitoa airport na kugusana bila kujali social distance.


Kwa kweli amekuwa msaada sana akiungana na Kenya kusema halali tutengwe na dunia.
 
Yeye hajawahi kuisaidia nchi kama nchi bali amesaidia sana wananchi wanyonge tunaomfahamu toka miaka ya 1992,kwenye kuwapigania wachimbaji wadogo wa madini hadi anaingia bungeni bado aliwapigania sana!! Yeye ana asili ya uana harakati ndio maana toka miaka hiyo yeye na serikali ni matatizo tu, wanyonge ndio wanaufahamu umuhimu wake. Achana na hao wanaojiita watetezi wa wanyonge baada ya kupata madaraka!!
 
Mambo mengi sana Tundu amelisidia taifa

1. Aliyoa information kwa mkulima akakamate ndege yetu

2. Alimzuia JPM kuwa asizuie makinikia bandalini kwamba kama nchi tutashitakiwa na kufilisiwa.

3. Alimkataza JPM asiipitiie upya mikataba ya madini kwamba mikataba ikashafungwa haitenguliwi. Vinginevyo tutashitakiwa na kufilisiwa.

4. Amezunguka nchi mbalimbali wa ulaya na amelika uuzuia nchi yetu isipewe misaada.


5. Kuketa sera ya ushoga nchini.

Au hukumbuki mkuu
Kuna sifa moja kuu inayompaisha huyu jamaa hata kuingia kwenye mioyo ya watu na kufuta hayo yote, anao uthubutu wa kufa akitetea na kupingana na kila dhulma manyanyaso, sheria kandamizi na hila za watawala ndio maana watu watakuona kama mavi unapotoa kila unalodhani lina mashiko na ni hoja kwako.

Kundi la watu ambao ni wahanga wa sheria mbovu na mbaya linakuwa kila kukicha nadhani hata wewe kesho unaweza kuingia huko kama mkondo utakupitia.

Bila shaka akifuzu kusimama nadhani tutapata katiba mpya na bora kwa umahiri wa sheria alionao
 
Kwa taaluma yake ya sheria aliwahi kutetea nini katika kesi amabayo ilipatia taifa ushindi?
Taja hata moja?
Zaidi ya kuwatetea mabeberu waendelee kutunyonya.

Nenda nyamongo utakuta habari zake. Halafu weka kesi yoyote ambayo aliwahi kuwatetea wazungu.
 
Subiri ma.ta.a.h.i.r.a ya machadema yaje na mitusi yao! utasikia eti oooh! alipigwa risasi!! so what? hata kama alipigwa kwa kuiba mke wa mtu basi ndio ahurumiwe awe tena rais!!!!? Hell no!!!!
Kuiba trilion 1.5 kumtoa CAG kafara kuficha Aibu ndiyo unafikiri ni tiketi ya kumrejesha ikulu mtukufu? Kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge katoa pesa zake binafsi toka mfukoni?
 
Uwepo peke yake wa Tundu Lissu ni msaada tosha kwa Tanzania.
Watanzania wameamka wanataka maneno yenye vitamini kuwapanua Ubongo kuwainua kifikira haki za binadamu utawala wa haki na Sheria, siyo kuwakaririsha eti CCM imejenga Reli kwa gharama kubwa kukiwa na ufisadi wa kutisha kwenye miradi yote, hakuna miradi ya CCM isiyo na kasoro kila sehemu kuna wizi na kampuni zinazosaidia ujenzi ni kampuni zao za rafiki zao ndugu zao, CCM ni ile ile ukoo wa panya
 
Back
Top Bottom