Nimekusamehe kwa kuwa umejitanabahisha kwamba ulikuwa mtoto mdogo mwaka 1995. Ngoja nikueleze mambo matatu makubwa ambayo Tundu Lissu amelifanyia taifa hili:-
1. Wakati wa awamu ya 3 ya Mkapa Tundu Lissu ndiye alipinga vikali uanzishwaji wa shamba la kufuga prawns kwenye bonde la mto
Rufiji. Endapo shamba hili lingeanzishwa lingeharibu mazingira kwa kiasi kikubwa. Wakati TL anafanya jitihada hizi alikuwa hata
hajawa mbunge. Huyo mtu wako unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba uharibifu wa mazingira hayo ulikuwa haumhusu!
2. Kuanzia mwaka 2005 alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza hadi 2015, Tundu Lissu ndo alipinga vikali bungeni kuhusu
kupitishwa na kuwekwa saini mikataba mibaya ya madini ambayo ilikuwa inafanya Tanzania kama shamba la bibi. Wakati huo wabunge
wa CCM walikuwa wanasema 'ndiyoooooo' - wakati mikataba hiyo inapitishwa. Hata huyo unayemshabikia alikuwa bungeni lakini alikuwa bubu. Kwa taarifa yako, yale yote Tundu Lissu aliyokuwa anayepigia kelele ndo ambayo Rais Magufuli ameyachukua na kuyafanyia kazi.
3. Tundu Lissu ndo ambaye alipiga kelele bungeni kuhusu ufisadi mkubwa uliofanywa na viongozi wa CCM kuhusu EPA, Kagoda, Meremeta,
Deep Green Finance, n.k. Wakati anaibua ufisadi huu, huyo unayemshabikia alikuwa kimya kana kwamba ufisadi huo haumhusu.
Nadhani sasa kijana unaweza kuona jinsi ambavyo Tundu Lissu alivyo mzalendo, mwenye uchungu na nchi yake.
Hitimisho: Si lazima uwe Rais ndo utoe mchango kwa nchi yako. Hapo nimekuonyea kwa ufupi tu jinsi ambavyo Tundu Lissu amelisaidia
taifa lake. Naamini sasa umemwelewa huyu mpambanaji na utampa kura ili awe Rais wa JMT, au siyo?