Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ameielezea vizuri Sera ya Majimbo kwa mara ya kwanza. Haina ukabila wala ukanda

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ameielezea vizuri Sera ya Majimbo kwa mara ya kwanza. Haina ukabila wala ukanda

tathmini

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
318
Reaction score
250
Mimi kama wengine, na kama mgombea pinzani anavyopotosha, mwanzoni nilidhani sera ya majimbo ni ya kufanya maeneo ya watu yajitegemee kikanda au kikabila.

Kumbe maana yake ni kuwa (1) Rais asihodhi maamuzi yanayohusu maendeleo. (2) Viongozi wote wenye maamuzi muhimu kuhusu maendeleo ya mkoa na wilaya wasiteuliwe na Rais, bali wachaguliwe na wananchi wa mikoa, wilaya na halmashauri hizo ili wawajibike kwao. (3) Wabunge warudishiwe madaraka yao ya uwakilishi wa matakwa ya wananchi. Wasiburuzwe na Rais.

Hii ndiyo jinsi ya kumzuia Rais mbaguzi asiyependa kupeleka maendeleo kwenye majimbo ya upinzani ambako nao wanalipa kodi. Tundu Lissu elezea hili kwa dakika mbili kila unakokwenda kama ulivyofanya Kagera.
 
Sera ya majimbo inachochea majimbo yenye utajiri kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili. Jimbo la kwanza kujitenga litakuwa Jimbo la kaskazini then Kanda ya ziwa. Iko mifano mingi tu Africa na dunia kwa ujumla.
 
Chadema waliitengeneza hiyo sera wakiilenga wao watoka kilimanjaro wachaga huyu mnyaturu Lisu kadakia tu vitu asivyovijua undani wake
 
Propaganda ya hovyo toka kwa wafuasi wa Ccm. Hivi huoni kuwa wateule wa Rais wanakuwa na nguvu kubwa dhidi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi ?!. Huoni kuwa wilaya , halmashauri na mikoa hutegemea hisani ya serikali kuu kufanya chochote wanachokitamani ?!
 
Sera ya majimbo inachochea majimbo yenye utajiri kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili. Jimbo la kwanza kujitenga litakuwa Jimbo la kaskazini then Kanda ya ziwa. Iko mifano mingi tu Africa na dunia kwa ujumla.
Itajitengaje??? Marekani jimbo gani limejitenga?? Ujerumani pia???

Pia umetumia kigezo gani kusema Jimbo la kaskazini ndo litakuwa jimbo tajiri???
Jimbo la Mashariki lenye mikoa ya Dar es Salaam , Tanga na Pwani ambako Kuna bandari, biashara nyingi na viwanda litakuwa sio tajiri???

Jimbo la Nyanda za Juu kusini ambalo lina mikoa inayolisha Tanzania na Africa mashariki ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe ambayo pia itakuwa na mapato ya mipaka miwili ya Malawi na Zambia nayo itakuwa sio tajiri???

Jimbo la Kusini lenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo Kuna gesi nyingi na korosho nalo litakuwa masikini???

CCM rudini shule na jitahidini muelimike na kujifunza
 
Sera ya majimbo inachochea majimbo yenye utajiri kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili. Jimbo la kwanza kujitenga litakuwa Jimbo la kaskazini then Kanda ya ziwa. Iko mifano mingi tu Africa na dunia kwa ujumla.
Kuna thread nime kuquote unapotosha na hapa pia unarudia kitu hicho hicho,
 
Kuna thread nime kuquote unapotosha na hapa pia unaridia kitu hicho hicho, naona mmetumwa kupotosha kama anavyo fanya baba 'enu Meko.
Sera hii ndo mzizi wa kifo cha CCM!! Unafikiri watachota wapi fedha za kampeni?

Au viongozi wao unafikiri kukiwa na majimbo watapata wapi fedha za ufisadi za kujichotea tu pale hazina na kwenda kujenga viwanja vya ndege kwao, kuendeleza ma ardhi makubwa ya wananchi wanayojimegea?

Sera ya majimbo ndo kifo cha CCM na viongozi wake walafi. Usione wanatumia nguvu kubwa kiasi hiki kupotosha!!
 
Sera ya majimbo inachochea majimbo yenye utajiri kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili. Jimbo la kwanza kujitenga litakuwa Jimbo la kaskazini then Kanda ya ziwa. Iko mifano mingi tu Africa na dunia kwa ujumla.
Una uhakika gani watajitenga?

Mbona jimbo la kaskazini sio tajiri kama la mashariki au nyanda za juu kusini?
 
Chadema waliitengeneza hiyo sera wakiilenga wao watoka kilimanjaro wachaga huyu mnyaturu Lisu kadakia tu vitu asivyovijua undani wake
Chadema imetapakaa nchi nzima.

Hadi huko rukwa ndanindani watu wanaijua chadema.
 
Hii Sera huwa haiundwi kwa karamu inajiunda automatically, ukijaribu kuiunda unaumia. Mara nyingi inafaa sana kwa mataifa ambayo hayajawa codified from the beginning, Kama hapa unaweza kuwa na Jimbo la Zanzibar na Jimbo la Tanganyika sivyo unavyodhani.

Ukigawa majimbo unatengeneza kitu kinaitwa spirit of nationalism kwenye hayo majimbo na huwez kukwepa kutugawa katika Makabila. Decision itatokana na Ile Nia ya kila Jimbo kuongoza central government. Lissu Zanzibar ndogo tuu Ni tatizo usituongezee shida nyongine
 
Sera hii ndo mzizi wa kifo cha CCM!! Unafikiri watachota wapi fedha za kampeni???
Au viongozi wao unafikiri kukiwa na majimbo watapata wapi fedha za ufisadi za kujichotea tu pale hazina na kwenda kujenga viwanja vya ndege kwao, kuendeleza ma ardhi makubwa ya wananchi wanayojimegea???

Sera ya majimbo ndo kifo cha CCM na viongozi wake walafi. Usione wanatumia nguvu kubwa kiasi hiki kupotosha!!
Uko sahihi sana, haya majinga ya ccm hayana nia njema na hii nchi hata siku moja, huwa namshangaa sana mtu anaye jitutumua kuwatetea.

Mbali na kukosa namna ya kuiba na kujiamulia kutumia hovyo pesa za wananchi, mfumo huu utampokonya mamlaka rais anayeteua DCs, RCs, RAS, DAS, Wakurugenzi nk.

Hao wateule wote wa rais hawana cha maana wanachofanya zaidi ya kuitumikia ccm huku wakilipwa kwa kodi zetu. Bunge litakuwa huru kuiwajibisha serikali na Mahakama itajisimamia katika kutenda haki.

Na kauli kama ile ya Meko eti 'ole wako umtangaze mpinzani kashinda' hazitasikika tena na huo ndio utakuwa mwisho wa ccm iliyo bakiza mbinu za kuengua wagombea kwa hila na uwizi wa kura.
 
Wanaikataa hii sera maana wanajua itawazuia kukusanya pesa za korosho kusini au za halimashauri Arusha na kwenda kujenga international airport vijijini kwao.
 
Back
Top Bottom