Pre GE2025 Tundu Lissu amtahadharisha Rais Samia, amtaka aache mambo ya ajabu baada ya Polisi kuzuia vijana wa BAVICHA

Pre GE2025 Tundu Lissu amtahadharisha Rais Samia, amtaka aache mambo ya ajabu baada ya Polisi kuzuia vijana wa BAVICHA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nane nane ni siku aliyozaliwa Yesu.
Utaona Kanisa Kanisa linafanya sgerehe ya vijana at about the same time.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu yuko njiani kuelekea Mbeya Kwenye sikukuu ya Bavicha

Lisu amesema kupitia ukurasa wake wa X kwamba yuko tayari Kukamatwa na Polisi lakini hatasitisha safari yake

Ni hilo tu 🐼
 
Rais Samia usilete mambo ya ajabu ajabu ya Magufuli. Siku ya Vijana Duniani inasherehekewa duniani kote. Kwa nini mapolisi wako wanazuia vijana wa CHADEMA barabarani & kuwakamata? Matumizi ya mapolisi yalimshinda Magufuli, & wewe yatakushinda. Fungua barabara vijana waende Mbeya!

Kwa vijana wote mlioko & mnaoelekea Mbeya: Na Mimi niko njiani kuja Mbeya kuungana nanyi. Kama ni kuzuiliwa au kukamatwa, & mimi wanizuie au kunikamata. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama & kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote!

View attachment 3066839View attachment 3066838

Pia soma=> BAVICHA yaanza kuogopwa na watawala, Polisi watumika kuwakamata ili kuzuia wasihudhurie siku ya vijana duniani itakayofanyika Mbeya
Mbona anamfokea rais kama vile anaongea na mwanae..hata kama ni Uhuru ila kuna mda mnakua wapumbav chadema chama cha fujo tuh hakuna mtu anayejielewa akakifata chadema
 
hawa watu hawajui kuna monkey pox wanasombana na mafuso kwenda mbeya,
 
Umeona watoto wa Samia au Kikwete wakishiriki hiyo Olympic, au unataka vijana wa Bavicha tu?
Ona akili za bavicha hivi kweli hii ni hoja ? Me naona imekaa kichuki chuki tuh na kimaskini bhc ,
 
Barabara zimejengwa kwa fedha nyingi sana, alafu anatokea mpuuzi mmoja badala ya kuwashauri vijana watumie barabara hizo kujijenga kiuchumi, kusafirisha mizigo mbalimbali wapate vipato, au kujikita katika usafirishaji wa abiria au vijana wajikite katika shughuli za kujiinua kiuchumi maana ajira ni ngumu, anawashauri waandamane juu ya barabara na kuwazidishia umaskini, kwani maandamano sio shughuli ya kiuchumi, wanapoteza muda na kuzidi kuwa maskini, mpuuzi yeye anawatumia hao vijana kama mtaji wake, yeye anaingiza kipato na uchumi wake unakuwa, pumbaf
Mkuu, hata wewe UNATUMIKA ila haujitambui; kama kupe asivyo jitambua akiwa kwenye ngozi ya ng"ombe ambaye tayari amesha chinjwa (kafa).
 
TUNDU LISSU ATUA JIJINI MBEYA


View: https://m.youtube.com/watch?v=zjDw0piPknY

Tundu Lissu apewa taarifa juu ya mbinu za kuzuiliwa mkutano wa Siku ya Vijana Dunia na kuelezwa kuwa zaidi ya Magari 100 yaliyokodishwa yakamakwa, vifaa vya PA uwanjani navyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi.

John John Mnyika asema amepokea taarifa kwa njia ya barua kutoka Msajili wa Vyama Vingi kuwa wasitishe shughuli ya Mbeya ya siku ya Vijana Duniani. Katibu mkuu John Mnyika anashangaa msajili wa vyama vingi hajawahi kuiita CCM kuhusu kauli ya Nape Nnauye kule Bukoba juu ya kuingilia mchakato wa uchaguzi wala kauli za kibaguzi za Mwenyekiti wa CCM Taifa kauli zake za kibaguzi kule Morogoro, msajili wa Vyama hajatoa karipio, kuita au barua kuionya CCM ...

1723391003072.png
 
. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama & kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote!
Lakini walio kaa kimya, hata huko CHADEMA ndio wanaotia shaka sana kuhusu yaliyoko huko ndani ya chama.

Ndugu Tundulissu, kanyaga twende.
 
Mkuu, hata wewe UNATUMIKA ila haujitambui; kama kupe asivyo jitambua akiwa kwenye ngozi ya ng"ombe ambaye tayari amesha chinjwa (kafa).
Hivi huyo uliye mjibu atakuelewa kweli, maana jibu hili ni zito sana!
 
Tamko la Lissu ni Tamko la Chadema
Tuache masihara, mkuu 'Erythro' huu ni wakati wa kipekee sana. Tafadhali, jaribu kuelewa ninayo yawasilisha hapa. Sipo hapa kudadisiana na mtu yeyote. Nayasema ninavyo yaona yalivyo.
Lisuu siyo CHADEMA. Tafadhali elewa. Achana na unazi usiokuwa na msingi wowote..

Samahani sana inalazimu iwe hivi sasa.
 
Back
Top Bottom