Pre GE2025 Tundu Lissu amtahadharisha Rais Samia, amtaka aache mambo ya ajabu baada ya Polisi kuzuia vijana wa BAVICHA

Pre GE2025 Tundu Lissu amtahadharisha Rais Samia, amtaka aache mambo ya ajabu baada ya Polisi kuzuia vijana wa BAVICHA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu ni wakati wa kutumia akili kubwa, hasa upande wa CHADEMA; nikiwa na maana ya wafuasi wa chama hicho wanao kataa kunuliwa na CCM.

Kwa yatakayo fuata kwenye tukio hili inawezekana ndio ukawa mtego wa kuwaondoa njiani ili CCM ipate pumzi ya kuendelea na mipango yake bila ya bughdha!

Jemedari vitani ni lazima ajue jinsi ya kuliamrisha jeshi lake na wakati sahihi wa kutumia mbinu husika. Kuna nyakati ni lazima kuepa mitego ya kizembe ili jeshi litoe pigo sahihi wakati mwafaka.
 
Kesho ni siku ya Vijana Duniani.

Ambapo vijana kama Taifa la Kesho wanakutana kuwa na National Dialogue ya pamoja kujadili mstakabali wa mambo yao na Nchi yao.

Wakati kama huu Majukwaa mbali mbali ya vyama mbali mbali hutumia fursa hii kuwakutanisha Vyama vya Vijana kuongelea mambo hayo.

Jambo la kushangaza ni namna ambavyo Magari yanayokusanya vijana wa Chadema.

Hata hivyo wababu hasa haijabainishwa.

Je ni hofu na woga kwamba vijana hawa watawafunika wale wenzao waliofanya Kambi Kule Zanzibar ambayo hata haisikiki?

View: https://youtu.be/1z-I16U3vvI?si=6hY5g1gg8soMW7Ux
 
Ndio tatizo la kuwa chini ya watu wasioweza kurusha mkojo hata hatua Moja toka waliposimama ni uoga uoga na ushenzi ushenzi tu
 

Attachments

  • IMG_1537.jpeg
    IMG_1537.jpeg
    109.4 KB · Views: 1
Wewe bila shaka yoyote ni masikini wa akili na hela


Wewe Chawa wa Mbowe, hooligan, crook and poorest human being, bring all your familly clan, huwezi nikuta kwa vyote, utabakia kuwa house boy wa Mbowe all your life..!!
 
Rais Samia usilete mambo ya ajabu ajabu ya Magufuli. Siku ya Vijana Duniani inasherehekewa duniani kote. Kwa nini mapolisi wako wanazuia vijana wa CHADEMA barabarani & kuwakamata? Matumizi ya mapolisi yalimshinda Magufuli, & wewe yatakushinda. Fungua barabara vijana waende Mbeya!

Kwa vijana wote mlioko & mnaoelekea Mbeya: Na Mimi niko njiani kuja Mbeya kuungana nanyi. Kama ni kuzuiliwa au kukamatwa, & mimi wanizuie au kunikamata. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama & kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote!

View attachment 3066839View attachment 3066838

Pia soma=> BAVICHA yaanza kuogopwa na watawala, Polisi watumika kuwakamata ili kuzuia wasihudhurie siku ya vijana duniani itakayofanyika Mbeya
Bure kabisa huyu jamaa,Hana adabu hata kidogo,akiwa Rais huyu nadhani atakuwa Rais wa kwanza asiye na adabu ulimwenguni. Taka taka kabisa huyu
 
Kihesa Kilolo
Iringa Tanzania

MAADHIMISHO NA KONGAMANO LA SIKU YA VIJANA DUNIA, MSAFARA WA CHADEMA WAZUIWA USIELEKEE MBEYA


View: https://m.youtube.com/watch?v=NR61OhD9dzo

Msafara wa magari ya vijana wa CHADEMA kutoka mikoa mbalimbali Shinyanga, Simiyu, Mara, Singida, Arusha, Kilimanjaro n.k wasimamishwa na traffic police huku polisi wengi wakiwa wazingira ....

Viongozi wa jeshi la Polisi mkoani Iringa wanasema wamesimamisha msafara huu wakitekeleza maelekezo kutoka juu....

Mwaka jana 2023 kongamano la CHADEMA kuadhimisha siku ya Vijana Duniani likifanyika bila shida yoyote ... mwaka juzi 2022 pia Kongamano la Siku ya Vijana Duniani likifanyika Shinyanga ambapo vijana toka kona zote za mikoa hawakuzuiliwa kwenda ktk makongamano hayo...


Vijana wa CHADEMA kupitia Baraza la Vijana CHADEMA wanahoji iwe vipi mwaka huu 2024 Kongamano la Mbeya linawekewa vikwazo kibao kitaifa,...
 
Barabara zimejengwa kwa fedha nyingi sana, alafu anatokea mpuuzi mmoja badala ya kuwashauri vijana watumie barabara hizo kujijenga kiuchumi, kusafirisha mizigo mbalimbali wapate vipato, au kujikita katika usafirishaji wa abiria au vijana wajikite katika shughuli za kujiinua kiuchumi maana ajira ni ngumu, anawashauri waandamane juu ya barabara na kuwazidishia umaskini, kwani maandamano sio shughuli ya kiuchumi, wanapoteza muda na kuzidi kuwa maskini, mpuuzi yeye anawatumia hao vijana kama mtaji wake, yeye anaingiza kipato na uchumi wake unakuwa, pumbaf
Ile mipuuzi ya CCM inayoandamana Zanzibar kusherekea hiyo siku ya Vijana ni mishetani ya wapi?
 
Vijana wa CHADEMA kupitia Baraza la Vijana CHADEMA wanahoji iwe vipi mwaka huu 2024 Kongamano la Mbeya linawekewa vikwazo kibao kitaifa,...

UPDATES
Kilolo, Iringa

Polisi wawazingira vijana wa CHADEMA waliokuwa wanaelekea Mbeya kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani , Vijana wapakiwa ktk lori na kutupwa selo katika kituo cha Polisi mkoani Iringa


View: https://m.youtube.com/watch?v=ByHwUEB0Zkk

Makambako vijana kutoka Zanzibar , Pemba na Dar es Salaam Ubungo wazuiliwa eneo hilo.

Nako huko Mtera vijana kutoka mikoa ya Dodoma na Mwanza wamezuiliwa njiani Mtera wasiendelee na safari yao kufika Mbeya

Jumla ya coaster 200 zilikuwa zinaelekea Mbeya kutoka sehemu mbalimbali kuungana na,wenzao kufika ktk Kongamano la Siku ya Vijana mkoani Mbeya kitaifa
 
Back
Top Bottom