Lengo lake ni kuwafurahisha zaidi Elton John/George Michael/boy George na wenzie.
Na sio kuwapa ujumbe watanzania walio wengi..
Hiyo ndy Siri ya kuandika ujumbe kwa kingereza bila kujali 95% ya watanzania hawajuwi kuongea na kuandika English kwa ufasaha..
Lengo lake ni kuwafurahisha zaidi Elton John/George Michael/boy George na wenzie.
Na sio kuwapa ujumbe watanzania walio wengi..
Hiyo ndy Siri ya kuandika ujumbe kwa kingereza bila kujali 95% ya watanzania hawajuwi kuongea na kuandika English kwa ufasaha..
EEeeeh Bhwanah, unawafahamu wote hao jamaaa. Mbona umemwacha Frddie Mercury!
Kama tulivyo binaadam wote, Tundu Lissu naye anao udhaifu wake. Hapa sijui alikuwa anamwandikia nani huu ujumbe! Anawaandikia wasomi wenzake, au waTanzania?
Hata wasomi wa siku hizi ni shaka sana kuelewa ujumbe anaouwasilisha. Hili ni tatizo kubwa kwa Lissu, hata kama yeye atadhani ni tatizo dogo.
Wakati huu kila fursa ya kuwafikishia ujumbe waTanzania ni jambo la muhimu sana linalotakiwa kufanywa kwa uangalifu mkubwa.
Ujumbe huu, pamoja na kutokuwa na njia ya kuwafikia wananchi kwa sababu ya lugha iliyotumika, njia hii inayotumika pia inajionyesha dhahiri kwamba Lissu na Chama chake wanajiweka mbali na wananchi.
Lakini la muhimu zaidi ni ujumbe uliomo kwenye andiko lenyewe. Mambo aliyozungumzia ni ya msingi sana kufuatana na hali iliyopo sasa hivi. Lakini cha kushangaza, yeye anaelekeza ujumbe wake kwenye historia, wakati wa Mwalimu Nyerere.
Nyakati hizi ni tofauti kabisa na nyakati zile. Kulikuwa na sababu kwa nini baadhi ya mambo ililazimu yafanyike kama yalivyofanyika kwa wakati ule, ambapo, kama yakifanyika wakati huu yataonekana kuwa ni tofauti sana.
Asisahau kwamba dunia nayo imekwishabadilika tokea nyakati za "vita Baridi" kwa pande mbili za Magharibi na Mashariki.
Hivi hakumbuki kwa mfano, kwamba Marekani walikuwa na utumwa na ubaguzi mbaya sana wa rangi enzi zile? Hata kama kubaguana hakujaisha ndani ya nchi hiyo, lakini angalao wamepiga hatua. Litakuwa ni jambo lisilokuwa na nguvu sana kwenda kuwaeleza wamarekani historia yao hiyo kwa wakati huu, kama njia ya kutaka kuboresha zaidi hali yao ya leo.
Kulalamikia mambo yaliyofanyika katika enzi tofauti na hizi inafanya kazi yake na chama chake kupata ugumu sana kueleweka mwelekeo wao ni upi.
Ajikite zaidi kwa haya yanayotokea wakati huu.