Tundu Lissu is entitled to his opinion. Yaana ana haku ya kutoa mawazo yake. Nimeiisoma yote kikubwa anaponda hotuba ya Rais SSH kuwa imetaja maendeleo ya mabarabara, hospitali na mashule na magereza.
Mimi ni kati ya watu waliolaani sana kushambuliwa kwa Lissu na Kikundi cha Makonda kwa amri ya Magufuli. Nimeandika sana humu kuwa ulikuwa UNYAMA wa hali ya juu.
Lakini sikubaliani na Lissu kwa aliyoyaandika hapa. Lissu anahitaji tiba ya KISAIKOLOJIA baada ya kupata tiba ya majeraha ya risasi 16. Mtu anayetarajia kuomba kura za uRais hapaswi kubeza maendeleo tuliyoyapata kwa miaka 60.