Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anaenda kuimaliza CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anaenda kuimaliza CHADEMA

sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Posts
7,640
Reaction score
11,680
Ieleweke tu kuwa Lissu hagombei urais ili awe kiongozi, maana anajua wazi hatapenya na hata heka heka za kampeni kwa hali yake hatoweza.

Anachotafuta Lissu ni platform ya kumshambulia Magufuli na serikali kwa kigezo cha kampeni.

Alipotangaza nia alianza kwa mashambulizi binafsi na moja ya kauli yake ni kuwa hatakuwa rais wa kukimbia matatizo na kwenda kijijini kwao kujificha (kwa akili yake anataka kuaminisha wafuasi wake kuwa Magufuli alikimbia na hakujihusisha na chochote kwenye sakata la corona kama ambavyo walikuwa wanasema)

Lissu ni mtu wa kuendeshwa na mihemko zaidi kuliko utulivu wa akili. Si mtu wa kusoma alama za nyakati au majira au mazingira. Atakachofanya atakuwa anamshambulia Magufuli kisha anawaombea wabunge kura.

Kwa hali ya sasa ukimgusa Magufuli umegusa mwananchi mmoja mmoja. Kama sio mama lishe basi bodaboda, kama sio mama mjamzito au mzazi basi mkulima, kama sio mfugaji basi mwenye kiwanda.

Kitendo cha kumshambulia Magufuli ni dhahiri atakuwa amewatoa watu kwenye reli na hivyo kuwapotezea watu shauku ya kumsikiliza na zaidi kumpuuza.

Muda utasema.
 
Kwa hali ya sasa ukimgusa Magufuli umegusa mwananchi mmoja mmoja. Kama sio mama lishe basi bodaboda, kama sio mama mjamzito au mzazi basi mkulima, kama sio mfugaji basi mwenye kiwanda.

Kitendo cha kumshambulia Magufuli ni dhahiri atakuwa amewatoa watu kwenye reli na hivyo kuwapotezea watu shauku ya kumsikiliza na zaidi kumpuuza.

Muda utasema.

Kwa maelezo ya huko juu, nakubaliana kidogo na mawazo yako kuhusu aina ya kampeni atakayopiga Mheshimiwa Lisu, lakini napingana na wewe kwenye hizi Aya za mwisho.

Kwa hulka ya watanzania hata kama Mheshimiwa Rais angekua kafanya kila aina ya wema pasingekua na mtu anaeweza kumpambania akisemwa vibaya, tutamsikiliza Lisu na yale yatakayokua na ukweli tutayakubali, yaliyokua ya uzushi yatapotea menyewe.
 
sheiza,

Haswaaaaaaa mkuu huyu jamaa lissu amini usiamini hatakuja kutangaza sera za chama chake kwanza hazijui na hana mpango nazo yeye ni chuki yake na jpm tu sasa utaongozaje nchi kwa mihemuko ya aina hiyo? Kila mtu sasahivi anamjua na tushampuuza wabishi waendelee tu kumuunga mkono maana wajinga bado wengi sana Tanzania.
 
sheiza,

Mkuu leo ni siku njema sana kwangu : Hii ni hoja ya pili kwa siku ya leo ambayo naamini muandishi imemchukua muda kuiwakilisha.

Asante.
 
sheiza,

Huu ndio ukweli, dogo Lissu hana ushawishi zaidi yakupoteza kura tarajiwa. Ila natamani sana kumuona kwenye kampeni ili ajue watanzania niwaelewa kuliko alivyodhani. Ni bahati mbaya tu kuwa atafikia Segerea.
 
sheiza,

Mkuu, tatizo lako ni kuwa mtu anapotoa kasoro ama kuzungumzia mapungufu ya serikali wewe unaona kama ni "direct attack" kwa Magufuli binafsi. Endapo Tundu Lissu atapata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CDM, hilo ndilo litakalokuwa jukumu lake kubwa.

Licha ya kuinadi ilani ya chama chake yenye muelekeo wasera mbadala, na hata kuwanadi wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani, bali pia atakuwa na jukumu la kifuchua mapungufu yote yaliyokuwa yamejificha serikali chini ya Rais anayemaliza kipindi chake cha utawala.

Kwa hiyo basi ni lazima utambue atamweka ktk mgombea wa uraisi kwa upande wa CCM ktk mizani, na kkumfanyi "performance evaluation" kupitia yale aliyowafanyia wanachi ktk kipindi cha 2015-2020. Yawe mema ama mabaya, ni lazima yawekwe wazi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa kwa mustakabali wa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom