sheiza
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 7,640
- 11,680
Ieleweke tu kuwa Lissu hagombei urais ili awe kiongozi, maana anajua wazi hatapenya na hata heka heka za kampeni kwa hali yake hatoweza.
Anachotafuta Lissu ni platform ya kumshambulia Magufuli na serikali kwa kigezo cha kampeni.
Alipotangaza nia alianza kwa mashambulizi binafsi na moja ya kauli yake ni kuwa hatakuwa rais wa kukimbia matatizo na kwenda kijijini kwao kujificha (kwa akili yake anataka kuaminisha wafuasi wake kuwa Magufuli alikimbia na hakujihusisha na chochote kwenye sakata la corona kama ambavyo walikuwa wanasema)
Lissu ni mtu wa kuendeshwa na mihemko zaidi kuliko utulivu wa akili. Si mtu wa kusoma alama za nyakati au majira au mazingira. Atakachofanya atakuwa anamshambulia Magufuli kisha anawaombea wabunge kura.
Kwa hali ya sasa ukimgusa Magufuli umegusa mwananchi mmoja mmoja. Kama sio mama lishe basi bodaboda, kama sio mama mjamzito au mzazi basi mkulima, kama sio mfugaji basi mwenye kiwanda.
Kitendo cha kumshambulia Magufuli ni dhahiri atakuwa amewatoa watu kwenye reli na hivyo kuwapotezea watu shauku ya kumsikiliza na zaidi kumpuuza.
Muda utasema.