Kumheshimu mwenyekiti sio kugeuzwa zombie, kama mwenyekiti anakuja na agenda zake za mfukoni unasimamia matarajio ya wafuasi, sisi Wafuasi ndio tutajua nani anasimamia tunachotaka. Hii kumuheshimu mwenyekiti ndio tuliishia kuchomekewa Lowassa yule mzee tapeli la kisiasa.
Akae pembeni ufanyike uchaguzi usio na mazonge. Na asipousoma mchezo atajikuta anabaki na wanaccm wakimuunga mkono, huku wafuasi wa cdm wakisimama na Tundu Lisu. Mpakeni Mbowe mafuta kwa mgongo wa chupa, huku akizidi kupoteza ushawishi chamani mwake. Huko CCM mwenyekiti ndio anaamua chochote atakacho kwani ni rais, na ndio mwenye uwezo wa kugawa vyeo. Mwenyekiti wa CDM heshima iko kwenye msimamo, sio kwenye maridhiano ambayo unaona kabisa hayatekelezwi.
Kikao cha nini, huko kwenye vikao ndio anakaa analazimisha agenda zake ambazo watu hawakubaliani nazo. Njia pekee ni kila mmoja aje na agenda yake kwa wafuasi, kisha wafuasi wataonyesha kukubaliana na agenda ipi.
Na kwakukusaidia tu, Mbowe alisema ikifika 2023 at step down kama mwenyekiti, msaidie kumkumbusha hiyo ahadi yake maana ni kama anajikausha. Mwambie hutajasahau ahadi hiyo, tunangoja utekelezaji.