Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Lissu ni typical Magufuli katika kusema hovyo sema tofauti Lissu yuko upinzani na hajawahi kuwa Rais. Wote wawili ni hatari kuwapa madaraka ya juu kabisa ya kuongoza nchi. Tumejifunza kwa Magufuli tusirudie makosa hata kama upinzani watachukua nchi lakini LISSU hafai kuwa Rais.Wadau ni swali najiuliza
Kwamba huyu mgombea urais 2020
Je, hakumbuki chama chake kilipambana kutafuta mariadhiano awamu iliyopita bila mafanikio
Je, amesahau haki ya mikutano ya hadhara anayotumia kuponda mariadhiano ilipatikana kupitia hayo mariadhiano
Ni vyema akaangalia zaidi maslahi mapana ya taifa kuliko nafasi yake
Kwa maoni yangu
Tundu Lissu ni mwanasheria na msimamizi mzuri wa utawala wa Sheria lakini hastahili nafasi kubwa ya urais hata uenyekiti wa Chama, hekima na busara yake haijakaa sawa
Post zangu za nyuma nimemtetea sana Lissu kwa umahiri wake kwenye sheria za madini na mazingira, nimemtetea wakati Magufuli ananyima haki zake baada ya kumpiga risasi 16