Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse hivi karibuni amesema CHADEMA hakuna utaratibu unaotaka kiongozi awe na ukomo wa Uongozi kwa muda maalumu isipokuwa anatakiwa kugombea na sio kuwa kama mwenyekiti wa CCM ambaye anapewa tu
"Kwa katiba ya CHADEMA mtu anagombea nafasi ya uongozi pasina ukomo, kwa hiyo Mwenyekiti Mbowe amekuwa akigombea miaka yote hii kwa sababu hakuna ukomo. Hajawahi kupita bila uchaguzi tofauti na wengine ambao mnafahamu akishakuwa Rais anakuwa Mwenyekiti wa chama pasina kuwa na uchaguzi, sasa Mbowe amechaguliwa mara zote.
Hakuna habari ya sisi kuwa na fomu moja ya mgombea mmoja, Huu ni msimu wa uchaguzi watu wanagombea, nafasi zote ambazo zinagombewa zipo wazi ninafikiri mmeona nafasi yangu imepata mshikaji juzi (Ezekiel Wenje). Kwa hiyo kwanini amekuwa akigombea miaka yote hii? Muulizeni Mheshimiwa Mbowe lakini sisi kama chama kwa katiba yetu hakujawahi kuwa na kizuizi"-
JAMBO TV