Tundu Lissu asusia mkutano Dar

Kuna watu wanashangaza sana wanatetea kitendo hiki kwa coverup ya haki sawa, lakini ndiyo hulka zetu zilivyo tunatambuana kwa kauli zetu mtu akimyamaza huwezi jua tabia yake.

 

majimshindo wakati mwingine uwe unashirikisha ubongo,watoto kujifunza kwa vitendo ndo wakakae frontline watu wenye kuchangia mada wakose pa kukaa? Kujifunza kwa vitendo ni kuchapa usingizi siyo? Kuwa siriaz kidogo hata kama unalipwa kwa ajili ya propaganda jtdi uwe mzalendo jamani kha!
 
Kuna watu wanashangaza sana wanatetea kitendo hiki kwa coverup ya haki sawa, lakini ndiyo hulka zetu zilivyo tunatambuana kwa kauli zetu mtu akimyamaza huwezi jua tabia yake.


kwa hiyo hawa watoto wanajifunza kwa vitendo! Majimshindo give us a break!
 

Think ure ready bt you really not sir. May be the time has come for the majority to speak, Chadema ni chama siasa sawa na Ccm, Cuf nk hakuna anayemzidi mwingine kwa utanzania. Chadema walijue hilo na kwamba kama wataamua kufanya vurugu kumbe kuna wengine wanaweza pia halafu wakiwa na nguvu zaidi. Katiba tunayoitaka ni ya watanzania wote. Juzi Hiza kazomewa mpaka mkutano ukaahirishwa, wiki iliyopita kadhalika kwa muwakilishi wa Ccm na Udp, najua maoni yako ni kutaka Chadema waendelee kuwa watanzania zaidi ya wengine hata wasiokuwa na vyama. Tulimsifu sana Sumaye kwa kuwaambia Ccm wajibu mapigo ya Chadema kwa hoja, wafanye siasa wasimwachie kazi m/kiti wao.
Few days later Chadema wanaacha hoja na kukodi wahuni wa chuo kikuu kuzomea na kuwatukana watu wasiowataka.
I dont like this but sir it is too logical kwamba hata kama isingekuwa leo nao wangeamua kufanya "siasa" kama za opponents wao hasa kwa kujua kuwa wao wana majority. Tundu Lissu hakulalamika wiki iliyopita wala juzi kuona watu wanazomea mbona jana kalalamika? They should know better that what goes around comes back around. Mtoa thread anasema watoto walienda kulala ukumbini kwa taarifa ya Itv lakini Mlimani Tv wameonesha vijana wamelala nje chini ya miti wakidai kukuta ukumbi umejaa!
Tanzania is much better than this, i said Tanzania...
 

Wewe kama huna la kuongea ni vizuri ukanyamaza usituchafulie hali ya hewa, mtu mwenyewe umejiunga juzi juzi tu, tulia great thinkers wakuonyeshe jinsi ya kuandika
 
hapa ni ujanja ujanja tu umetumika, hili si rika la kuchambua na kukosoa mambo muhimu ya mustakabali wa taifa na maisha ya mtu, wamewakusanya ili waongeze idadi ya watu na baadae waje watuambie wananchi walioshiriki ni 98%... maoni yanakusanywa dar na dom tu, cc wa mikoani mbona hatushirikishwi? kwanini? eti kukusanya maoni siku 3 kweli jamani? kweli hapa kuna kamchezo kanachezwa!
 

Hapo ndipo tujiulize kama ccm walishinda kweli kwenye uchaguzi wa mwaka jana ikiwa wanaweza kuchakachua hata hoja kama hii mchana kweupe. Arusha wakachakachua wakati wa uchaguzi wa meya, yamewashinda kuchakachua kwenye bajeti ya manispaa.
CCM wameiteka hoja ya katiba ambayo ni wananchi wote na sasa wanachakachua ili wakidhi mahitaji yao.
 
Hao watoto wanajua hata maana ya katiba ni nin kweli..? makamba anachapa kazi kwelikweli kwa mara ya mwisho kuhakikisha anakizika chama......Dahh mwisho wa dunia au mwanzo wa tanzania iliyo bora ndo mefika..
 
Endelea kujifanya ujui....lakini iko siku utajuwa. Huwa nafatilia sana hoja zako hapa jamvini....wewe huna tafauti na ccm'kubishana na wakati
 

Chadema mjilaumu wenyewe,tabia ya kuzomea mlianzisha nyie! Sasa tutaenda kwa mwendo wa kuzomeana hadi kieleweke!
 
WanaJF
Hakuna kulala.Waandae tu usalama wa Taifa.Kama tulivyowahi kusema, usalama wa Taifa wamegeuka kuwa usalama wa ccm. Hata hivyo hakuna kulala Maandamano ya nchi nzima yatakapofanyika kitaeleweka. Tumeiambia Serikali kinachotakiwa ni busara, lakini busara itakaposhindikana wasidhani wanaweza kupambana na"nguvu ya Umma". Ukombozi ndio unaanza na ninaona wanazidi kutaidia kufikia iukamilifu wa ukombozi huo.Wenye mapenzi mema na nchi yetu tuendelee kushikamana, Katiba si mali ya CCM, si mali ya Rais. Ni mali ya Rais. Kama nilivyosema kwenye Kongamano "Mtoto hawezi kumzaa Mama yake". Naona wengi hawajaelewa.
 

Naamini Sasa wewe ni mtot wa unmri wa miaka 9 kwenda chini na ndiyo sababau uelewei chochote, ungekuwa mtoto wangu leo ungekula viboko vya kutosha.
Pumbavu kabisa!!!!!!!!!!!!!!!
 
Endelea kujifanya ujui....lakini iko siku utajuwa. Huwa nafatilia sana hoja zako hapa jamvini....wewe huna tafauti na ccm'kubishana na wakati

Chadema watalaamu wa zomeazomea wanafuata CCM na CUF ya mwisho kwa utalaamu wa zomeazomea!
 

Hili ndiyo Serikali ya Kikwete inataka, Bagbo alikatalia Ikulu na sasa amekosa pakukumbilia, nasema sisi tutadai Katiba bora hadi ikulu, Tunawtaarifu kuwa vipengele vyote ambavyo vimeshataja kuwa vina mapungufu ni bora wakavifanyia kazi. Huu ni wakati wakuanza kuhamasisha Watanzania wanaotaka nchi huru tujiandae kwa maandamano makubwa kwenda kudai Katiba Bora iliwajue yote wanayofanya ni bure katiba Bora itapatikana kwa Nguvu ya Umma!

Pipoooos!!!!!!!!!!!!!!!
 
<br />
<br />


Kuna Tofauti kati ya Mbunge kulala Bungeni na hao kula kulala waliowahishwa hapo Kamrijee,Kila Mbunge anayonafasi bungeni kwa hiyo akilala hazuii michango ya wengine whereas Karimjee hao watoto walimwaga kuzuia nafasi,Period!!
Chagua Kufikiri!!
 
Afadhali watoto wanaoenda ukumbini na kusinzia kuliko majitu mazima yanasoma chuo kikuu yanadanganywa na chadema kwenda kuzomea! Hopeless kabisa!
 
BEPARI,
Nakubaliana sana na wewe. Katiba ni ya Watanzania wote na vyama vyote ni sawa.
i) Kushangilia au kuzomewa ni mtu anazomewa au mawazo. Ni haki duniani kmute kupongeza au kuzomea mawazo mazuri. Lukini ni ujuha kuzomea mawazo mazuri kwa sababu tu ya ushabiki. Ni vema tufike mahali objectively nini kiko objective na nini ni mawazo Objective as distionct from ushabiki. Katika Kongamano la Dar juzi na jana mtu yeyote mwenye busara angeweza kutambua kinachozomewa ni nini na kwanini kiuna kuzomeea.
ii) Nashukuru Bepari anakiri kuwa "wanajua fujo zaidi". Ieleweke Chadena kuhamasisha wanavyuo kwa lengo la kuchangia si dhambi wala kinyume na sheria. Lakini kitendo cha kukusanya vijana kwa lengo la kuvuruga ni jambo lisiloweza kuvumilika na kushushia hadhi Chama kikongwe kama chama cha Mapindfuzi. Nadhani kama Taifa bado hatujajua tunachotakiwa kufanya kupata mchakato mzuri wa Katiba. Tujue kuwa tukikosea kwenye Mchakato na Katiba tutakayotengeneza itakuwa ya ajabu
 
Kuna watu wanashangaza sana wanatetea kitendo hiki kwa coverup ya haki sawa, lakini ndiyo hulka zetu zilivyo tunatambuana kwa kauli zetu mtu akimyamaza huwezi jua tabia yake.


Kitu pekee ninachoweza kusema hapa hii NI AIBU.
Mara hii CCM "risasi imewatokea nyuma ya bunduki", wamejiumiza wenyewe.
Yote inaonesha jinsi wasivyokuwa makini. Angalau walipowajaza hao watoto hapo wangezuwia waandishi wa habari kupiga picha ili kuficha aibu hii. Masikini CCM, imeishiwa mbinu, imeishiwa ujanja. Wamekuwa kama samaki nje ya maji, kutapatapa tu. HII NI AIBU!

Ikiwa Serikali haitaki tuwe na katiba upya wasifanye usanii kama huu. Ielewe kuwa wananchi ndio waajiri wao, wapo kwa sababu ya wananchi. Kuufanya usanii kama huu ni kuzidi kuonesha nia yao mbovu na hili linazidi kuwapandisha ghadhabu wananchi.
 

Dr Slaa Phd(kuzomea)! Mzee wangu Slaa hii tabia ya kuzomea ulianzisha wewe! Sasa ni bora twende kwa kwa mwendo wa kuzomeana tu! Umeanza kusingizia Usalama wa Taifa siku nyingi lakin kwa hili kuwarubuni vijana wa Vyuo vkuu wazomee watanzania wenzao linakupa aibu kubwa na haingii akilini kwa mtu ambae ulitaka kuongoza Nchi uwe na tabia ya kuzomeazomea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…