JMushi1,nashukuru kwa kutoa maoni yako juu ya maoni yangu.
Mara zote ninajitahidi kwamba nisiendeshwe na ushabiki kutoa mchango wangu,ama kujadili suala lolote lihusulo maslahi ya Taifa letu.
Na kuhusu kutumia title ya Padre ninapomzungumzia Padre Dr.W.Slaa,nadhani ni athari za mafundisho niliyopewa nikiwa katika u katekumeni,au yale mafunzo ya kanisani ili kupata sakramenti mbalimbali zinazotolewa ndani ya Kanisa katoliki....niliweza kujifunza kwamba kuna sakramenti saba,zikiwemo NDOA na UPADRE,na hii sakramenti ya NDOA ina hadhi sawa na sakramenti ya u PADRE,
Katika kanisa Katoliki,mtu akishaoa ama kuolewa,atabakia kuwa katika hesabu ya ndoa hiyo hiyo(kama hakudanganya kufungishwa ndoa hiyo)mpaka atakapofariki
Pia atabakia kuwa Padre maisha yake yote(uchunguzi wa kina hufanyika ili asiingie upadre kama kuna vitu vinavyomzuia asiwe Padre,mengine huachiwa Mungu),isipokuwa muda fulani anaweza tu kwa wakati fulani ama maishani kupunguziwa uwezo fulani (kama vile kuungamisha,kuadhimisha ibada ya Sakramenti ya Ekaristi takatifu),lakini hatoondolewa u Padre wake kama sakramenti ya msingi aliyoipata ndani ya kanisa,hivyo kuendelea kuwa Padre maisha yake yote.Na pia U Padre ndio cheo ambacho ni BASIC kwa watumishi wote ndani ya kanisa katoliki kuanzia ngazi ya Padre,hata mtu awe askofu,awe Kardinal,awe Papa(kama ilivyo kwenye fani ya udaktari wa tiba,kuanzia digrii moja wewe ni dr,master ni dr,Phd ni dokta,Profesor bado ni dokta)
Hivyo basi,kwangu mimi kutumia Padre Slaa,ndio maadili yangu niliyolelewa nayo na kuyaelewa,na sioni ni kosa.Siongeil hili kwa sababu unazozisema wewe,nadhani kwa maelezo haya,Padre Dr.W Slaa atakuwa mtu wa nafasi ya juu kuweza kunisahihisha kama mafundisho yangu niliyoyaelewa ya tatizo....anaweza(ama mtu yeyote anaweza kunisahihisha)
anhaa nilisahau,na by the way,Padre kwa kiswahili maana yake ni BABA,na kwa kiingereza ni FATHER
Asante