Tundu Lissu asusia mkutano Dar

Ok then,toa mwongozo wa namna ya kujadili mbali zaidi ya CDM na CCM.Je unapenda mafisadi washinde?
 
sasa kutoka katika public debate inasaidia nini...! Mbona mchangiaji wa ccm kazomewa ikawa poa tuu... CDM wasipoangalia nao mwisho wa siku wataonekana waigizaji tuu kama kina joti. SIasa za ccm very cheap na za cdm nazo zinaelekea huko huko....ANGALIZO
 
JMushi1,nashukuru kwa kutoa maoni yako juu ya maoni yangu.

Mara zote ninajitahidi kwamba nisiendeshwe na ushabiki kutoa mchango wangu,ama kujadili suala lolote lihusulo maslahi ya Taifa letu.
Na kuhusu kutumia title ya Padre ninapomzungumzia Padre Dr.W.Slaa,nadhani ni athari za mafundisho niliyopewa nikiwa katika u katekumeni,au yale mafunzo ya kanisani ili kupata sakramenti mbalimbali zinazotolewa ndani ya Kanisa katoliki....niliweza kujifunza kwamba kuna sakramenti saba,zikiwemo NDOA na UPADRE,na hii sakramenti ya NDOA ina hadhi sawa na sakramenti ya u PADRE,
Katika kanisa Katoliki,mtu akishaoa ama kuolewa,atabakia kuwa katika hesabu ya ndoa hiyo hiyo(kama hakudanganya kufungishwa ndoa hiyo)mpaka atakapofariki
Pia atabakia kuwa Padre maisha yake yote(uchunguzi wa kina hufanyika ili asiingie upadre kama kuna vitu vinavyomzuia asiwe Padre,mengine huachiwa Mungu),isipokuwa muda fulani anaweza tu kwa wakati fulani ama maishani kupunguziwa uwezo fulani (kama vile kuungamisha,kuadhimisha ibada ya Sakramenti ya Ekaristi takatifu),lakini hatoondolewa u Padre wake kama sakramenti ya msingi aliyoipata ndani ya kanisa,hivyo kuendelea kuwa Padre maisha yake yote.Na pia U Padre ndio cheo ambacho ni BASIC kwa watumishi wote ndani ya kanisa katoliki kuanzia ngazi ya Padre,hata mtu awe askofu,awe Kardinal,awe Papa(kama ilivyo kwenye fani ya udaktari wa tiba,kuanzia digrii moja wewe ni dr,master ni dr,Phd ni dokta,Profesor bado ni dokta)
Hivyo basi,kwangu mimi kutumia Padre Slaa,ndio maadili yangu niliyolelewa nayo na kuyaelewa,na sioni ni kosa.Siongeil hili kwa sababu unazozisema wewe,nadhani kwa maelezo haya,Padre Dr.W Slaa atakuwa mtu wa nafasi ya juu kuweza kunisahihisha kama mafundisho yangu niliyoyaelewa ya tatizo....anaweza(ama mtu yeyote anaweza kunisahihisha)
anhaa nilisahau,na by the way,Padre kwa kiswahili maana yake ni BABA,na kwa kiingereza ni FATHER
Asante
 
Mlienda kukodi wahuni ili muweze kupata nafasi ya kuongea haya mnayoongea.Kama ilikuwa ni zomea zomea ya kivyama,mbona Warioba hakuzomewa?Msilete mchezo kwenye hii issue mtalipeleka Taifa pabaya.Watu wa kukodi kuleta vurugu hawana passion na kile wanachokifanya,mwishowe wata run away like cowards,si mmeona wamelala?
Sasa mnaleta mchezo nyie,si ndiyo?
 
Ok then,toa mwongozo wa namna ya kujadili mbali zaidi ya CDM na CCM.Je unapenda mafisadi washinde?

Kwa kuwa suala hili linagusa maslahi ya watu wengi, hebu tuanze kwa kuangalia makundi makuu ya raia wa nchi hii( utagundua kundi l siasa ni dogo sana rejea idadi ya wanachma wa vyama vyote na idadi ya watu waliopiga kura), unaweza kuanza kwa kuchambua makundi makuu yanayounda jamii ya watanzania, halafu tunaweza kuendela kutokea hapo. Kwa bahati mbaya sana siamini mapambano haya yanahusu ufisadi kwa uwa wanaotka tuamini kuwa wanapambana na ufisadi wao pia ni mafisadi wakubwa(kwa shahidi). kwenye hili sijui hata kama mafisdi wanahusika zaidi ya kutumiwa kuficha sura za wanafiki.
 
Mbona wa CCM na UDP walizomewa Chuo Kikuu, hakuna aliyesusa? Hawa Chadema wamezowewa kidogo tu wanajidai kususa. Wazomee wao tu, wakizomewa wanasusa. wakishindwa kura wanasusa, wakoje hawa?
Unapashwa kuelewa CCM wanazomewa kwa sababu ya kutuma wawakilishi hafifu (INCOMPITENT) Kuwawakilisha ambao wanazungumza pumba.Hawazomewi kwa sababu ni CCM bali wanazomewa kwa upupu wao.Na hii inadhihilisha ni kwa kiasi gani CCM na serikali wasivyo serious.Naimani ndani ya CCM kuna watu makini wanaoweza kuwawakilisha katika midahalo mingi lakini CCM haiwatumii au hawako tayari kutokana na msimamo wa chama chao kupingana na ukweli uliopo wazi.Wanataka kuleta utaratibu au nidhamu ya kuburuzana katika vikao vyao.WATAFANYA KILA MBINU KUVURUGA MIJADALA YA KATIBA.Kwa kukusanya watu watoto kujaza nafasi na kuwanyima wachangiaji wa kweli kushiriki,watatuma mjadala wa katiba vijijini ulioandikwa kiingereza!na mbinu nyingi chafu.Mjadala huu kujadiliwa sio matakwa ya CCM bali wanafanya hivyo kwa shinikizo.Wnataka kufanya kama formality.HATUTEGEMEI WATU WALIOIKIMBIA MIDAHALO WAKATI WA UCHAGUZI WAFURAHIE MIJADALA WA KATIBA,CCM WEUPE CCM KUKUBALI MIJADALA AU MIDAHALO NI KUVULIWA NGUO HADHARANI.
 
Nimekupata,hata hivyo msimamo wangu upo pale pale kwamba wengi wa wale wanaomwita Padre,ni wale wenye nia ya kupanda chuki dhidi yake na wenye dini nyingine.Hilo liko wazi.
However sasa na wewe umekuja na gia ya dini ya ukatoliki,huoni tupo kwenye siasa?Tatizo naona athari zako za mafundisho uliyopewa ya katekumeni yanafanana na mafunzo waliyopewa kina Malaria Sugu.
Haya ndugu Aplinari,tuendelee na mjadala,siwezi kumsemea Dr. slaa kwasababu na yeye yumo humu.Hata mimi huwa ningependa kumwita Padre,lakini haina mantiki kwenye mazungumzo haya pamoja na yale anayoyapigania kwasasa,anawapigania watanzania wote,na cheo chake sasa kinatakiwa kireflect status hiyo.
Naona ni wahuni waliotumwa wengi wao wameathirika kama wewe.
 
Taja hao wapambanaji ambao unasema ni mafisadi na ufisadi walioufanyaWeka ushahidi kama unavyodai.Ukiniuliza mimi niwataje mafisadi wa chama chako nitakuwekea orodha ndefu hadi uchoke kuisoma.
 
Akili zako ziko makarioni au tumboni.... Kenya,Malawi,Zambia,Egypti,Tunis,Ivory coast na Libya
kulikuwa na watu wenye nyodo kama wewe, lakini Je'leo wako wapi? wote wamezolewa na upepo wa mabadiliko ya nguvu ya umma
 
Taja hao wapambanaji ambao unasema ni mafisadi na ufisadi walioufanya.Ukiniuliza mimi niwataje mafisadi wa chama chako nitakuwekea orodha ndefu hadi uchoke kuisoma.

1. Dr Wilbroad Slaa - mkataba wa kufasidi ruzuku halali ya CHADEMA kujilipa mshahara wa mamilioni.
2. Samuel Sitta - Matumizi mabaya ya fedha za ofisi ya mbunge(ametumia umia zaidi ya Milioni 500, achalia mbali gharama za matibabu karibu milion 30 kwa dawa tu)
 
Akili zako ziko makarioni au tumboni.... Kenya,Malawi,Zambia,Egypti,Tunis,Ivory coast na Libya
kulikuwa na watu wenye nyodo kama wewe, lakini Je'leo wako wapi? wote wamezolewa na upepo wa mabadiliko ya nguvu ya umma

Tatizo huwa mnakalilishwa historia nusu nusu, leo nenda Kenya, Egypt, na Libya uulize nini kilifuata baada ya mapambano? unadhani ni kama fairy old tales zenye happy ending? Hayo matusi yageuze kama mimi namuambia mama yako mzazi kisha ujiulize vipi kama nisinge yatamka?
 
jmushi1 hujamuelewa nduka. Hawa ni wale waliolewa ulevi wa sumu ya mihadhara inayohubiri chuki badala ya amani kama hiyo dini ya jangwani inavopenda kujitambulisha na ndivo tungetegemea wawe lakini matendo yao, kauli zao na husuda zao zaonyesha ni watu wa vita chuki na hila za kisiasa zilizofunikwa kwa mwanvuli wa dini ya amani feki. Wanafikiri watanzania hawawezi kuungana nje ya hizo fikra potofu za kidini na kuwaondoa hao watawala waovu wanaowashabikia kwa njaa zao na kutoelewa kwao. Wanafikiri wataweza kuzuia nguvu ya umma kwa kuwalaghai watanzania wa imani hiyo ya jangwani kuwa huo umma ni maadui zao hivo na wenyewe waungane kuwapapinga hii ndiyo nguvu potufu anayoota huyo ndugu yetu na hao waovu wenzake.
Hawa nao watapitiwa kama upepo kwani tumeona huko mashariki ya kati walikoweka hizo nguvu zao potofatu wamekuja kuwatimua mchana mchana na nguvu ya umma. Nguvu ya umma ni zaidi ya wigo wa kidini na siasa dhaifu za chuki. Daima watashindwa tu wapende wasipende. Nguvu ya umma ni haki hizo zingine ni dhulma na upotoshaji ambao daima unashindwa tu maana haki siku zote inashinda. Unaweza kufanya mahubiri na kupaza sauti kuwa mawazo yako ni haki lakini haki yenyewe siku moja inakuumbua tu kama ilivomuumbua Ghadafi na wadhalimu wenzake.
 
Te teh teh!Mkuu naona hauko serious kabisa,tafadhali sitaki nijutie kujikita kwenye mjadala huu.Sitaki nijutie muda wangu.Huo ndiyo ushahidi wa ufisadi?Please be serious otherwise tuwaachie wengine wanaotaka kuchangia waendelee kufanya hivyo.
Yani dili moja tu la RA vs ruzuku ya CDM?Ebu quantify hayo maelezo yako hapo juu,then baada ya hapo tuangalie ni kivipi ruzuku ni ufisadi.Na kama matumizi ya ruzuku hiyo yako kinyume na taratibu zao ndani ya chama chao(jambo ambalo sijalisikia),then hayo ni matatizo ya wanachadema na uwaachie wanachadema,pili pili isiyokuwasha....Kama ni ufisadi wenu ccm,ukweli ni kwamba unaliangamiza Taifa na ndiyo umetufikisha hapa tulipo.Pia unaweza kuwa unakumbukumbu ndogo sana ama ni makusudi tu.
 

Hoja ni moja tu, nani kakuambia umma ni wa Slaa, Mbowe na Lissu peke yao? kwani sisi hata tukiwa dhaifu kama unavyoaminishwa/kukaririshwa sio umma? au ni nani anayeamua kuwa nani awe umma na nani asiwe umma? rejea hapo juu, regardless ya nguvu ya umma wenu na sisi tuna umma wetu na ikifika kwenye kupambana tutapambana be informed brother.
 
Yani dili moja tu la RA vs ruzuku ya CDM?Ebu quantify hayo maelezo yako hapo juu,then baada ya hapo tuangalie ni kivipi ruzuku ni ufisadi..

Kwangu mimi haijalishi umefasidi kiasi gani, fisadi ni fisadi tu, pili sijasema ruzuku ni ufisadi ila kumlipa Slaa mamilioni kwa mikataba ya siri ni ufisadi. Kama Slaa angekuwa msafi angekuja na mkataba huu hadharani kama kawaida yake kutoa mabomu hadharani.
 
Ndiyo maana kuna watu bado hawaamini kuwa mlishinda uchaguzi uliopita kiuhalali,wanadai mlichakakchua,ukweli ni kwamba nachelea kusema inaweza kuwa kweli kwasababu hamna umma ulioko nyuma ya ufisadi ndugu yangu,mnalazimishia kuwa mna umma,hakuna kitu.Na hao watoto wenye njaa mmewaleta ili mseme mna umma?
Mwenzako Majimshindo ndio anakuja na hoja dhaifu kabisa kuwa eti wameenda kujifunza.Mko very out of touch.
Kwa taarifa yako,kudai kuwa mna umma ni sawa na kusema youre delusional.
 
Reactions: BAK
Siwezi kuwasemea,na pia siwezi kukujibu kwasababu sioni ushahidi.Si umesema unao?Uweke hapa basi.
 


Hao watoto walibana nafasi watu wenye mawazo pevu wasiingie kujadili katiba.

Kwa wasomi na wanazuoni hiyo katiba ata wasomi bado wote hawajauelewa kwa sababu ya St Kayumba sasa hao watoto wamepewa sh ngapi pili wameletwa na nani haiwezekani mtu mwenye akili timamu ukajumuika na hao watoto ambao ata katiba hawajui maana yake.
Namuunga mkono Mh Lisu kutoka nje.
 
Mafisadi wameshauteka mjadala wa Katiba mpya. Sioni sababu yoyote ya Watanzania kuendelea kupoteza muda wetu katika kuchangia mjadala huu ambao mwisho wake ni utungaji wa katiba ambayo itakuwa haina maslahi yoyote kwa Watanzania.

Inasikitisha sana hali hii labda watu ambao bado wana heshima ndani ya nchi yetu kama vile Warioba, SAS na wengineo wazungumzie tatizo hili kubwa na kumuonya Kikwete na kundi lake la mafisadi kwamba Katiba inayotungwa ni katiba ya Watanzania wote bila kujali itikadi zetu hivyo kuwe na uhuru wa ukweli katika kukusanya mawazo bila vitisho vya aina yoyote ile au vurumai zitakazofanywa na mafisadi. Vinginevyo kushiriki katika mjadala huu kwa maoni yangu ni kupoteza muda tu.
 
Hivi una habari kuwa huko Haiti mtu aliyewahi kuwa mwanamziki ameshinda kiti cha urais?....mtamkashifu sana dr Slaa,lakini ukweli karibu ya umma wa watanzania wengi wameamua oneday huyu jamaa aje kuwa rais wa Tanzania. We jifanye tu ubishi wa kiburi....lakini oneday utakubaliana na maneno yangu!. Hata huko Haiti kulikuwa na watu kama wewe waliokuwa wanamponda huyo mwanamziki,lakini siku ya mwisho wananchi ndiyo waliamua....kazi kwako baki na chuki zako uone zitakufikisha wapi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…