Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameshauri serikali kuitisha Bunge la dharura kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi, akisisitiza msimamo wa chama hicho wa ‘hakuna uchaguzi bila mabadiliko'.
Vilevile, chama hicho kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kukabili mabadiliko ya kisera kwenye misaada katika sekta ya afya yaliyofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump.
Lissu alisisitiza msimamo huo jana mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, wilayani Kinondoni.
Kwa mujibu wa Lissu, chama hicho hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi ambao alisisitiza kuwa kuingia katika uchaguzi kwa hali ya sasa ni kukubali kunyolewa au kuwa kama kondoo anayepelekwa machinjioni.
Lissu alisema kuna Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, lakini kwao CHADEMA, kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lakini haina maana watasusia uchaguzi.
"Tusijaribu kuitanua lugha kuliko maana yake ya kawaida, hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lazima tuzungumze hayo mambo mawili tuone tunawezaje tukaenda nayo mbele aidha kwa pamoja au kuamua lipi muhimu.
"Sasa hilo sitaki nizungumze hapa, zaidi tunakwenda kujifungia kisha tutaamua kwa pamoja ili uwe uamuzi wa chama na si wangu peke yangu. Tutakwenda kuonana na marafiki zetu duniani tuwaambie msimamo wetu hadharani. Tutawaomba watuunge mkono, na wale wasiotupenda tutawaangalia usoni, tutawaambia msimamo wetu ni huu," Lissu alisema.
"Tunazungumzia kupata mageuzi kwa shuruti kama walivyopata Kenya, Malawi, Bunge letu linaweza kukaa muda wowote hata bila kuwa na ratiba,"
Source: Nipashe