Pre GE2025 Tundu Lissu ataka bunge likae kikao cha dharura ili kufumua sheria za Uchaguzi zilizopo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao ndo wanaofanya ccm iendelee kutawala maana wameshawahakikishia maslai yao
Na hili ndio tatizo kubwa kwa nchi zote masikini
Hakuna mzungu anaweza kukupenda bila maslahi
Angalia nchi za Falme za kiarabu, wao wana mafuta lakini ni win win situation
Chimba mafuta tujengee kila kitu kama nyie na tuwe na kila kitu

Ila sisi tunakubali kupewa dawa za ukimwi mpaka leo
Hatuna akili za kujiongeza
Wazungu wana hakikisha mnaendelea kuwa masikini huku baadhi wakinufaika kwa wazungu

Kama Rais anaenda kupewa masharti Vatican usitegemee kitu hapo
Hata leo kama chama kingine kitashika wanaweza kuwa hivyo hivyo kama nguvu itakuwa ya mtu mmoja basi
Lakini kana serikali yote inakuwa na msimamo mmoja tutaendelea
 
Anasema hasusii ila uchaguzi "HAUTAKUWEPO" meaning atauvuruga kwa maandamano, sasa hapa anategemea sapoti ya waandamanaji.

Maandamono yoyote yanayoweza simamisha shughuli kubwa kama ya uchaguzi atahitaji:

1. vijana angalau 200 kila mkoa.

2. Bajeti.

3. Waratibu.

4. Jeshi kumuunga mkono.

Uliye tayari kuandamana kama humuoni akiwa na hivyo vitu vi4 hapo juu, za kuambiwa changanya na zako.

SIASA NI MASLAHI.

Iwapo pakatokea muujiza TAL akafanikiwa kupata wazuiaji uchaguzi, bado Ccm ina kete mkononi ya kuitumia hiyo nafasi kuendelea kukaa madarakani kwa kuchelewesha mchakato ukakamilika 2028 december huko tarehe mpya ya uchaguzi October 2029.

Sasa maumivu yatakuwa double iwapo ccm ikishinda kwa kishindo hiyo 2029.
 
Kwa nchi hii ya waoga ni ngumu kutegemea waishinikize serekali, japo hiyo ndio njia iliyobaki. Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi tusitegemee mabadiliko ya kweli. Sana sana kelele zikiwa kubwa kutakuwa na mabadiliko kadhaa.
Wewe uko tayari umwage damu ili Tundu Lissu awe rais wa JMT na makamu raisi wake Heche? What are you going to benefit? Hakuna mtanzania yo yote mwenye akili timamu anayeweza kufanya hivyo. Hao ni vibaka tu wa kisiasa, achana nao.
 
CHADEMA wanachowaza ni madaraka tu hakuna cha zaidi ya hapo. Wanapambania matumbo yao na si vinginevyo.
Na ndio msingi mkuu wa kushika dola. Sasa inategemea baada ya kushika dola hayo matumbo unayahudumiaje? Kwa kula bila kunawa wala kuwajali waliokuweka kwenye madaraka? Hapo ndipo kilipo kitendawili.
 
Anasema hasusii ila uchaguzi "HAUTAKUWEPO" meaning atauvuruga kwa maandamano, sasa hapa anategemea sapoti ya waandamanaji.

Maandamono yoyote yanayoweza simamisha shughuli kubwa kama ya uchaguzi atahitaji:

1. vijana angalau 200 kila mkoa.

2. Bajeti.

3. Waratibu.

4. Jeshi kumuunga mkono.

Uliye tayari kuandamana kama humuoni akiwa na hivyo vitu vi4 hapo juu, za kuambiwa changanya na zako.

SIASA NI MASLAHI.

Iwapo pakatokea muujiza TAL akafanikiwa kupata wazuiaji uchaguzi, bado Ccm ina kete mkononi ya kuitumia hiyo nafasi kuendelea kukaa madarakani kwa kuchelewesha mchakato ukakamilika 2028 december huko tarehe mpya ya uchaguzi October 2029.

Sasa maumivu yatakuwa double iwapo ccm ikishinda kwa kishindo hiyo 2029.
 
CHADEMA wanachowaza ni madaraka tu hakuna cha zaidi ya hapo. Wanapambania matumbo yao na si vinginevyo.
Chama cha siasa kisipowaza kushika madaraka kinatakiwa kiwaze nini badala yake? Kuunda timu ya mpira au kujifua kwa mashindano ya riadha?
 
Kwani CCM haiwezi kubaki madarakani kwa kutekeleza hizo reform? Au ni kweli kwamba pakifanyika hayo mabadiliko yakiwemo ta Katiba CCM lazima ishindwe? Kama hayo ni kweli basi upo walakini katika utawala wa CCM. Otherwise why worrying if CCM is still on the right track ?
 
Wasira siyo wa kumrefer kwa lolote.

Angekuwa ni kijana au mtu mzima, tungesema ni mjinga, lakini kwa sababu ni kikongwe, tunasema akili yake imechoka.
Hili andiko liwe pinned na lifanyiwe laminated kwa matumizi ya baadae na Wasira mwenyewe aone pamoja na mwenyekiti wake..
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameshauri serikali kuitisha Bunge la dharura kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi, akisisitiza msimamo wa chama hicho wa ‘hakuna uchaguzi bila mabadiliko'.

Vilevile, chama hicho kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kukabili mabadiliko ya kisera kwenye misaada katika sekta ya afya yaliyofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Lissu alisisitiza msimamo huo jana mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, wilayani Kinondoni.

Kwa mujibu wa Lissu, chama hicho hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi ambao alisisitiza kuwa kuingia katika uchaguzi kwa hali ya sasa ni kukubali kunyolewa au kuwa kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

Lissu alisema kuna Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, lakini kwao CHADEMA, kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lakini haina maana watasusia uchaguzi.

"Tusijaribu kuitanua lugha kuliko maana yake ya kawaida, hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lazima tuzungumze hayo mambo mawili tuone tunawezaje tukaenda nayo mbele aidha kwa pamoja au kuamua lipi muhimu.

"Sasa hilo sitaki nizungumze hapa, zaidi tunakwenda kujifungia kisha tutaamua kwa pamoja ili uwe uamuzi wa chama na si wangu peke yangu. Tutakwenda kuonana na marafiki zetu duniani tuwaambie msimamo wetu hadharani. Tutawaomba watuunge mkono, na wale wasiotupenda tutawaangalia usoni, tutawaambia msimamo wetu ni huu," Lissu alisema.

"Tunazungumzia kupata mageuzi kwa shuruti kama walivyopata Kenya, Malawi, Bunge letu linaweza kukaa muda wowote hata bila kuwa na ratiba,"

Source: Nipashe
CHADEMA ni nani hasa watupangie cha kufanya. Wasipokuja wao kwenye uchaguzi mbona kuna vyama vingine vitashiriki!!
 
Kwa nchi hii ya waoga ni ngumu kutegemea waishinikize serekali, japo hiyo ndio njia iliyobaki. Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi tusitegemee mabadiliko ya kweli. Sana sana kelele zikiwa kubwa kutakuwa na mabadiliko kadhaa.
Mulete machafuko halafu mkimbikie Belgium kwa waume zenu!! That will not happen
 
Wasira siyo wa kumrefer kwa lolote.

Angekuwa ni kijana au mtu mzima, tungesema ni mjinga, lakini kwa sababu ni kikongwe, tunasema akili yake imechoka.
Pamoja na jana wako huwezi kufika hata 25% ya akili ya Stephen Wassira. Ndiyo maana unaandika sentensi za kumkashifu
 
Mzee Wasira yuko sahihi. Huyu jamaa amebaka uenyekiti kutoka kwa Mbowe na sasa anataka kubaka urais wa nchi toka kwa Mama. Mbinu wanazotumia kufanya huo ubakaji ni pamoja na matusi wakishirikiana na wale nchi rafiki zao.

Mbona tafsiri ya hayo maneno iko wazi tu na kila mtu anaelewa. Ni kwamba bila hayo marekebisho ya sheria na katiba, chadema itazuia kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa October 2025.

Ni wazi kwamba hayo mabadiliko wanayoyataka chadema hayatakuwepo. Hivyo waendelee kujifungia wao na wale washiriki wao wa nchi za nje kupanga mikakati ya namna watakavyouzia huo uchaguzi mkuu. Serikali yetu nayo inapanga mikakati ya kuhakikisha hicho watakachofanya chadema na washirika wao hakifanikiwi kwa vyo vyote vile.

Wakumbuke nchi yetu ni sovereign state. Hakuna nchi ya nje inayoweza kuingilia sovereignty yetu. Hili raisi wetu alishaliweka wazi kwa wamerikani walipotaka kutuingilia miezi michache iliyopita.
all in all uchaguzi uwe huru.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameshauri serikali kuitisha Bunge la dharura kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi, akisisitiza msimamo wa chama hicho wa ‘hakuna uchaguzi bila mabadiliko'.

Vilevile, chama hicho kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kukabili mabadiliko ya kisera kwenye misaada katika sekta ya afya yaliyofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Lissu alisisitiza msimamo huo jana mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, wilayani Kinondoni.

Kwa mujibu wa Lissu, chama hicho hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi ambao alisisitiza kuwa kuingia katika uchaguzi kwa hali ya sasa ni kukubali kunyolewa au kuwa kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

Lissu alisema kuna Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, lakini kwao CHADEMA, kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lakini haina maana watasusia uchaguzi.

"Tusijaribu kuitanua lugha kuliko maana yake ya kawaida, hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lazima tuzungumze hayo mambo mawili tuone tunawezaje tukaenda nayo mbele aidha kwa pamoja au kuamua lipi muhimu.

"Sasa hilo sitaki nizungumze hapa, zaidi tunakwenda kujifungia kisha tutaamua kwa pamoja ili uwe uamuzi wa chama na si wangu peke yangu. Tutakwenda kuonana na marafiki zetu duniani tuwaambie msimamo wetu hadharani. Tutawaomba watuunge mkono, na wale wasiotupenda tutawaangalia usoni, tutawaambia msimamo wetu ni huu," Lissu alisema.

"Tunazungumzia kupata mageuzi kwa shuruti kama walivyopata Kenya, Malawi, Bunge letu linaweza kukaa muda wowote hata bila kuwa na ratiba,"

Source: Nipashe
Wabunge milele hawatadhubutu kufumua Sheria za uchaguzi!
Wakifanya hivyo ,wote waturudi makwao kwenye uchaguzi mkuu
 
CHADEMA ni nani hasa watupangie cha kufanya. Wasipokuja wao kwenye uchaguzi mbona kuna vyama vingine vitashiriki!!
Mkuu wewe ghadhabu yako ilikuwa kwa Magufuli tu? Madhambi mengine ya wengine kwenye chama tawala dhidi ya Watanzania (injustice) hayakupi tabu kabisa!

Yaani baada ya Magufuli kutoweka basi hakuna shida tena CCM ikitawala milele kivyovyote vile. Sio?
 
Huo ni ukweli Magufuli alikuwa shetani. Hajawahi kutokea kiongozi mkatili na dhukumat kama Magufuli.

Mbona Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK hatuwaandiki kihivyo??

Mama Samia hana hata chembe ya ukatili tuliouona kwa yule shetani wa Chato
 
Back
Top Bottom