Pre GE2025 Tundu Lissu ataka bunge likae kikao cha dharura ili kufumua sheria za Uchaguzi zilizopo

Pre GE2025 Tundu Lissu ataka bunge likae kikao cha dharura ili kufumua sheria za Uchaguzi zilizopo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hata sasa kuna wengi wamemwaga damu ili ccm ikae madarakani, ww umefaidika nini.
Wewe uko tayari umwage damu ili Tundu Lissu awe rais wa JMT na makamu raisi wake Heche? What are you going to benefit? Hakuna mtanzania yo yote mwenye akili timamu anayeweza kufanya hivyo. Hao ni vibaka tu wa kisiasa, achana nao.
 
Mpaka kufika oktoba tutashuhudia mengi
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameshauri serikali kuitisha Bunge la dharura kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi, akisisitiza msimamo wa chama hicho wa ‘hakuna uchaguzi bila mabadiliko'.

Vilevile, chama hicho kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kukabili mabadiliko ya kisera kwenye misaada katika sekta ya afya yaliyofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Lissu alisisitiza msimamo huo jana mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, wilayani Kinondoni.

Kwa mujibu wa Lissu, chama hicho hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi ambao alisisitiza kuwa kuingia katika uchaguzi kwa hali ya sasa ni kukubali kunyolewa au kuwa kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

Lissu alisema kuna Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, lakini kwao CHADEMA, kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lakini haina maana watasusia uchaguzi.


"Tusijaribu kuitanua lugha kuliko maana yake ya kawaida, hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lazima tuzungumze hayo mambo mawili tuone tunawezaje tukaenda nayo mbele aidha kwa pamoja au kuamua lipi muhimu.

"Sasa hilo sitaki nizungumze hapa, zaidi tunakwenda kujifungia kisha tutaamua kwa pamoja ili uwe uamuzi wa chama na si wangu peke yangu. Tutakwenda kuonana na marafiki zetu duniani tuwaambie msimamo wetu hadharani. Tutawaomba watuunge mkono, na wale wasiotupenda tutawaangalia usoni, tutawaambia msimamo wetu ni huu," Lissu alisema.

"Tunazungumzia kupata mageuzi kwa shuruti kama walivyopata Kenya, Malawi, Bunge letu linaweza kukaa muda wowote hata bila kuwa na ratiba,"

Source: Nipashe
 
Mzee Wasira yuko sahihi. Huyu jamaa amebaka uenyekiti kutoka kwa Mbowe na sasa anataka kubaka urais wa nchi toka kwa Mama. Mbinu wanazotumia kufanya huo ubakaji ni pamoja na matusi wakishirikiana na wale nchi rafiki zao.



Mbona tafsiri ya hayo maneno iko wazi tu na kila mtu anaelewa. Ni kwamba bila hayo marekebisho ya sheria na katiba, chadema itazuia kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa October 2025.

Ni wazi kwamba hayo mabadiliko wanayoyataka chadema hayatakuwepo. Hivyo waendelee kujifungia wao na wale washiriki wao wa nchi za nje kupanga mikakati ya namna watakavyouzia huo uchaguzi mkuu. Serikali yetu nayo inapanga mikakati ya kuhakikisha hicho watakachofanya chadema na washirika wao hakifanikiwi kwa vyo vyote vile.



Wakumbuke nchi yetu ni sovereign state. Hakuna nchi ya nje inayoweza kuingilia sovereignty yetu. Hili raisi wetu alishaliweka wazi kwa wamerikani walipotaka kutuingilia miezi michache iliyopita.
Na uliamini alikuwa serious
 
Wewe uko tayari umwage damu ili Tundu Lissu awe rais wa JMT na makamu raisi wake Heche? What are you going to benefit? Hakuna mtanzania yo yote mwenye akili timamu anayeweza kufanya hivyo. Hao ni vibaka tu wa kisiasa, achana nao.
Kwani sasa una benefit kitu gani we karai
 
Hatujasema bila Reforms tutasusia, tumesema bila reforms tutahakikisha Uchaguzi haufanyiki kabisa.
 
Back
Top Bottom