Hii ni wazi. Umepatia kabisa. Tundu lissu hapindishi wala hana muda wa propaganda wala usanii. Yeye kila kitu ni straight talk. Hutamkuta akila hindi la kuchoma wala kununua jogoo kwenye mikutano ya hadhara.
Huyo Magufuli alikuwa ni gwiji la propaganda za ki-Nigeria. Akikamilisha dili ya kuwalipa ACACIA/Barrick anatupiga changa kuwa sisi ndio tutalipwa Noah kila mTz! Eti “mtetezi wa wanyonge”, mcha Mungu, kiboko ya mabeberu, mnyenyekevu. Mara apime corona kwenye mapapai na mbuzi! Mara aagize tiba ya juisi Madagascar na kusisitiza kujifukiza kwa miti shamba!
Katika nchi ambayo wengi wametekwa na waganga wa kienyeji na mitume na manabii, ni wazi Tundu Lissu hawezi kupendwa kama Magufuli.