Tundu Lissu atakubalika kwa Utetezi wa Wanyonge lakini hatavunja Rekodi ya Magufuli ya kupendwa na Wananchi

Tundu Lissu atakubalika kwa Utetezi wa Wanyonge lakini hatavunja Rekodi ya Magufuli ya kupendwa na Wananchi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni angalizo tu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Lissu kwamba wanamkubali kwa Kiasi anachofanya kutetea haki zao likiwamo hili la Mfumuko wa Bei yaani inflation.

Atazidi kukubalika ila hatavunja Rekodi ya Kupendwa na Wananchi aliyonayo hata kufani yule Shujaa Magufuli.

Tunaeleweshana tu.

Mungu wa mbinguni akubariki!
 
Mtetezi wa mabeberu na wezi wa madini yetu ndiye unataka kumgeuza awe mtetezi wa wanyonge?
 
Sasa kama magufuli alipendwa kwa nini hakujiamini kwenye uchaguzi? Kipimo cha mtu kupendwa ni kipi? Hizi ni porojo magufuli alilazimisha watu wampende ndo hakujiamini hata kwenye uchaguzi mkuu!

Alafu kitu kingine yule alikuwa rahisi sio kila aliyekuwa anamchekea kuwa alikuwa kweli anampenda wengine walikuwa chawa! Wengine kwa sababu ya hofu! Na wengine kwa kulazimishwa kuhudhuria kwenye mikutano yake na malori kwa lazima!! Tundu lisu ni chuma mzee! Na anapendwa mpaka kesho.
 
Hii ni wazi. Umepatia kabisa. Tundu lissu hapindishi wala hana muda wa propaganda wala usanii. Yeye kila kitu ni straight talk. Hutamkuta akila hindi la kuchoma wala kununua jogoo kwenye mikutano ya hadhara.

Huyo Magufuli alikuwa ni gwiji la propaganda za ki-Nigeria. Akikamilisha dili ya kuwalipa ACACIA/Barrick anatupiga changa kuwa sisi ndio tutalipwa Noah kila mTz! Eti “mtetezi wa wanyonge”, mcha Mungu, kiboko ya mabeberu, mnyenyekevu. Mara apime corona kwenye mapapai na mbuzi! Mara aagize tiba ya juisi Madagascar na kusisitiza kujifukiza kwa miti shamba!

Katika nchi ambayo wengi wametekwa na waganga wa kienyeji na mitume na manabii, ni wazi Tundu Lissu hawezi kupendwa kama Magufuli.
 
Rekodi moja imefikia ukomo na nyingine bado inatengenezeka, kipi kipimo cha rekodi, ili tupime imevunjwa bado au?
 
Ni angalizo tu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Lissu kwamba wanamkubali kwa Kiasi anachofanya kutetea haki zao likiwamo hili la Mfumuko wa Bei yaani inflation.

Atazidi kukubalika ila hatavunja Rekodi ya Kupendwa na Wananchi aliyonayo hata kufani yule Shujaa Magufuli.

Tunaeleweshana tu.

Mungu wa mbinguni akubariki!
Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist , kwanza unaposhindanisha vitu viwili kwa mashindano ya mlingano, lazima vitu hivyo viwe vinafanana!. Huwezi kumlinganisha kupendwa na wananchi mtu mmoja ni rais wa JMT na mwingine ni mbunge tuu!. Mashindano ya kupendwa kwa JPM na wananchi mshindanishe na Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK na Samia na sio na Lissu!.

Kuna vitu kumhusu Tundu Lissu, wewe huvijui!. Mimi nimesoma nae Ilboru hivyo namfahamu vizuri zaidi Tundu Lissu, amini nakuambia kuna baadhi ya vitu Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, na hili nililieleza wazi humu Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Hivyo ili kumshanisha Lissu kupendwa na wananchi, ni if tukimpa Tundu Lissu urais wa JMT kwa term moja tuu, nakuhakikishia, Magufuli anasubiri!.
P
 
Lissu amejibainisha kwa werevu na waelewa, yule jamaa kisanii alijibainisha kwa wajinga, watu duni wenye vinyongo wenzake watatengeneza Jopo lao wakabeba kivuli cha kuwatetea wanyongwe wakasababisha mabanda mabovu ya machinga kujengwa kila Kona ya nchi a real rubbish of centuries, VAGARANT COUNTRY.
 
Back
Top Bottom