Tundu Lissu atamani kuwepo na viongozi wanawake kwenye safu za juu za uongozi CHADEMA

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

BAWACHA wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 Mlimani City Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa akizungumza baada kutoka gerezani

"Waliniletea salamu na hata nilipotoka wengine walinifuata nyumbani kuja kunipa pole na hongera. Gereza limenifundisha Na namwambia Samia anipeleke tena gerezani maana nina mengi ya kujifunza. Tukijifunza tunapata silaha ya kuja kutetea haki. Kwa kukaa gerezani nimejifunza watanzania wanavyoteseka, mimi sikujua kuna watu wanakaa gerezani hawajahukumiwa wanakaa miaka 10"

Akizungumzia ajenda ya No refoms No election

"Hata CCM wanasema No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona ngoma iliyofanyika Dodoma, waliofanya wakati wanatetea wanaogombea. Kwanza wamevunja sheria. Wameanza Uchaguzi wa mapema kinyume na sheria alafu sisi wanatuambia tuko nje ya sheria"

Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika

"Siku kama ya leo mlikuwa na maadhimisho Kilimanjaro na kwa sababu pengine ya dalili zilizokuwepo kwenye maridhiano, BAWACHA mkafanya uamuzi wa kumpa Rais tuzo. Tuzo ya BAWACHA Ingempa motisha zaidi lakini ile motisha ikawa ni uharibifu zaidi''

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

“Sisi wenyewe tukoje hili jopo ambalo leo lipo meza kuu ukiniacha mie baada ya leo hawatakaa meza kuu tena. Uongozi wetu wa chama wa juu ukoje, kamati kuu yetu ikoje kwa sababu ya umuhimu wake kwenye uongozi wakuu wa chama ni klabu ya vijana wa kiume naomba tuulizane viongozi na wanachama wote tuliopo hapa mara ya mwisho tuliona lini mwanamke akikaa meza kuu”

“Sikumbuki kama nimewahi kuona mwanamke akikaa meza kuu kwenye chama hiki. Tusinyooshe vidole kwa hawa ambao wameongoza nchi yetu kwa miaka yote hii vilevile tunyoosheane vidole na sisi”

NO REFORMS NO ELECTION!
Imewatia kiwewe viongozi wote wa CCM, ambao sasa wanahaha na kuwahimiza vifaa vyao, aikina Mtungi watafute njia za kuwa epusha na tsunami linalo jikusanya kuwazoa wote.
Polisi tayari wanaanza mazoezi ya vita? Wanajiandaa vita na waTanzania?
 
Mmh napita tuu., wasalimie uko.
 
Kwakweli imependeza, kwa sababu CDM aitumii hela kuleta watu.

Unapoona ukumbi umefurika kama hivyo inatia moyo kuona watu wanataka mabadiliko.
 
Wakuu,

BAWACHA wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 Mlimani City Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa akizungumza baada kutoka gerezani

"Waliniletea salamu na hata nilipotoka wengine walinifuata nyumbani kuja kunipa pole na hongera. Gereza limenifundisha Na namwambia Samia anipeleke tena gerezani maana nina mengi ya kujifunza. Tukijifunza tunapata silaha ya kuja kutetea haki. Kwa kukaa gerezani nimejifunza watanzania wanavyoteseka, mimi sikujua kuna watu wanakaa gerezani hawajahukumiwa wanakaa miaka 10"

Akizungumzia ajenda ya No refoms No election

"Hata CCM wanasema No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona ngoma iliyofanyika Dodoma, waliofanya wakati wanatetea wanaogombea. Kwanza wamevunja sheria. Wameanza Uchaguzi wa mapema kinyume na sheria alafu sisi wanatuambia tuko nje ya sheria"

Sawa
 
Back
Top Bottom