Wakuu,
BAWACHA wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 Mlimani City Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Tundu Lissu
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa akizungumza baada kutoka gerezani
"Waliniletea salamu na hata nilipotoka wengine walinifuata nyumbani kuja kunipa pole na hongera. Gereza limenifundisha Na namwambia Samia anipeleke tena gerezani maana nina mengi ya kujifunza. Tukijifunza tunapata silaha ya kuja kutetea haki. Kwa kukaa gerezani nimejifunza watanzania wanavyoteseka, mimi sikujua kuna watu wanakaa gerezani hawajahukumiwa wanakaa miaka 10"
Akizungumzia ajenda ya No refoms No election
"Hata CCM wanasema No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona ngoma iliyofanyika Dodoma, waliofanya wakati wanatetea wanaogombea. Kwanza wamevunja sheria. Wameanza Uchaguzi wa mapema kinyume na sheria alafu sisi wanatuambia tuko nje ya sheria"
Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika
"Siku kama ya leo mlikuwa na maadhimisho Kilimanjaro na kwa sababu pengine ya dalili zilizokuwepo kwenye maridhiano, BAWACHA mkafanya uamuzi wa kumpa Rais tuzo. Tuzo ya BAWACHA Ingempa motisha zaidi lakini ile motisha ikawa ni uharibifu zaidi''