Tundu Lissu atolea ufafanuzi wa kesi ya Halima Mdee na wenzake

Tundu Lissu atolea ufafanuzi wa kesi ya Halima Mdee na wenzake

Avunje katiba ipi ambayo haijavunjwa? Labda ya Israel. Ya tz ilishavunjwa saa hii ina P.O.P kila page
Tutakuwa hatuna tofauti na yeye kwenye hilo. Yaani anavunja katiba na sisi tunamtaka avunje tena katiba sababu tu itatufurahisha ikiwa imevunjwa kwa upande wetu!! Tutakuwa tumefanana nae kiakili na kisiasa
 
Take home msg ni hii:

1. Job Ndugai asilaumiwe
2. Tulia Ackson asilaumiwe
3. Alaumiwe anayewalipa mshahara, ambaye ni Rais.

Msikilize, jibu hoja zake kwa hoja, achana na character assassination arguments or what is called Ad Hominem arguments

Tundu Lissu hana hoja. Kwanini anataka Rais aingilie Mhimili wa Binge? Dhana ya mgawanyo wa madaraka na utawala Bora iko wapi hapa?.

Makosa yapo na yalifanywa na Magufuli na Ndugai. Sioni kwa nini tunayahamishia kwa Rais Samia
 
Hivi Tundu Lissu anewahi kushinda kesi gani ya kupigiwa mfano? Ningependa kujua japo kesi moja tu ambayo Wakili Tundu Lissu aliwahi kushinda ni hukumu yake ni hukumu rejea; moja tu.
Tundu ni maneno mengi watu wanaona kuwa ni mwanasheria nguli. Mimi kwangu nafahamu kwamba Tundu anajua historia siyo sheria.
Kwenye kushinda kesi Tundu Lissu namkubali ni gwijj. Kuna kesi ya wachimbaji wadogo wadogo huko Bulyanhulu au Nyamongo kwenye miaka ya 1997-2000 wakati wa Mkapa. Wale watu waliondolewa bila fidia na Tundu Lissu aliwatetea Mahakamani bure na wakashinda. Waliposhinda ndipo wakamchangia fedha kama shukrani.
 
Makosa yapo na yalifanywa na Magufuli na Ndugai. Sioni kwa nini tunayahamishia kwa Rais Samia
The incoming president is obliged to rectify mistakes made by her predecessor(s)!
 
Well said Mh. Tundu Lissu Hassan, Mahakama imekuwa kama kokoro kwa jinsi inavyotumiwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ndiye Rais wa Tanzania.
 
Tutakuwa hatuna tofauti na yeye kwenye hilo. Yaani anavunja katiba na sisi tunamtaka avunje tena katiba sababu tu itatufurahisha ikiwa imevunjwa kwa upande wetu!! Tutakuwa tumefanana nae kiakili na kisiasa
Kweli kabisa!
 
Kwa maana hiyo Chadema mnataka Rais avunje sheria ili kuwafurahisha sio??

Na asivunje kwa mambo mengine bali ya kwenu tu??
 
Haka ka mama bilionea kananiudhi Leo kanaenda Tanga kukoleza uchawi kaliotumia kupata huo uraisi
 
Hivi Tundu Lissu anewahi kushinda kesi gani ya kupigiwa mfano? Ningependa kujua japo kesi moja tu ambayo Wakili Tundu Lissu aliwahi kushinda ni hukumu yake ni hukumu rejea; moja tu.
Tundu ni maneno mengi watu wanaona kuwa ni mwanasheria nguli. Mimi kwangu nafahamu kwamba Tundu anajua historia siyo sheria.
Wee lisu alikuwa na kesi LUKUKI hazitajiki ni nyingi na zote hamna hanata 1 aliyofungwa... Sasa utasemaje huyo mtu hajui sheria?
 
Take home msg ni hii:

1. Job Ndugai asilaumiwe
2. Tulia Ackson asilaumiwe
3. Alaumiwe anayewalipa mshahara, ambaye ni Rais.

Msikilize, jibu hoja zake kwa hoja, achana na character assassination arguments or what is called Ad Hominem arguments

Ilaumiwe na Ilaaniwe CCM iliyoiba SANDUKU la KURA!!!!
 
Ni kweli kabisa, Rais ndiye anayelipa mishahara kwa wabunge wote. Lakini kumtaka Rais azuie mishahara ni kumtaka afanye jambo kinyume cha sheria, ni kumtaka avunje katiba, sasa hatuwezi kufurahia uvunjwaji wa katiba kwa sababu tu utawaondoa Covid 19 bungeni.

Kama ni suala la kuwa Rais aliwapeleka bungeni hao covid 19 kwa maana ya aliwabeba na kuwashawishi basi njia sahihi kwake kuwaondoa bungeni ni kuwashawishi wajiuzulu nafasi zao, jinsi walivyoingia ndio watoke hivyohivyo (off radar).

Rais ana mamlaka makubwa yasiyo kikatiba, mfano kumlipa Lissu fedha bila kuidhinishwa na bunge na pasipo kujustify kwa nini amelipa. Ni kweli inabidi tupate katiba mpya kupunguza mamlaka hayo
Kwanza, Rais alitumia vibaya madaraka yake kuvuruga uchaguzi kwa dhamira ovu ya kuua ushindani wa kisiasa kinyume cha katiba ya nchi hii. Hilo pekee yake lilikuwa uvunjaji wa katiba ya nchi likistahili kuchukuliwa hatua. Pili, baada ya kugundua athari za kutokuwa na wabunge wa upinzani Rais huyo huyo akavunja tena katiba ya nchi kwa kutengeneza wabunge haramu kupitia chama kikuu cha upinzani bila kufuata utaratibu wa kisheria wala mwongozo wa chama husika. Sarakasi zote zinazoendelea sasa ndani na nje ya bunge ni mwendelezo tu ya uvunjaji wa katiba ya nchi na sheria uliosisiwa na Rais mwenyewe na unaondelea kupata baraka zake binafsi. Rais asingekuwa na maslahi na ukiukwaji huu wa katiba, suala hili lingefikia mwisho pale baraza kuu la chama husika lilipothibitisha uamuzi wa kuwavua hao wabunge 19 uananchama. Wabunge hao wanayo haki kabisa kwenda mahakamani kupinga kufukuzwa na chama chao. Uhuni ni pale wanapokingiwa kifua kuendelea kuwa bungeni wakati wakipinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama. Tofauti na wabunge wa majimbo waliopata kulindwa na dola baada ya kufukuzwa uanachama hawa wa viti maalum waliingizwa bungeni kwa mchakato haramu.
 
Back
Top Bottom