Ni kweli kabisa, Rais ndiye anayelipa mishahara kwa wabunge wote. Lakini kumtaka Rais azuie mishahara ni kumtaka afanye jambo kinyume cha sheria, ni kumtaka avunje katiba, sasa hatuwezi kufurahia uvunjwaji wa katiba kwa sababu tu utawaondoa Covid 19 bungeni.
Kama ni suala la kuwa Rais aliwapeleka bungeni hao covid 19 kwa maana ya aliwabeba na kuwashawishi basi njia sahihi kwake kuwaondoa bungeni ni kuwashawishi wajiuzulu nafasi zao, jinsi walivyoingia ndio watoke hivyohivyo (off radar).
Rais ana mamlaka makubwa yasiyo kikatiba, mfano kumlipa Lissu fedha bila kuidhinishwa na bunge na pasipo kujustify kwa nini amelipa. Ni kweli inabidi tupate katiba mpya kupunguza mamlaka hayo