Tundu Lissu atolea ufafanuzi wa kesi ya Halima Mdee na wenzake

Kesi ya Bulyanhulu na Nyamongo alishinda kwa sababu kipindi hicho mahakama ilikuwa bado ni mahakama. Prof. Kabudi kabla ya kuharibikiwa alipata kusema hivi bungeni: when presidents were still presidents and law was law!
 
Wee lisu alikuwa na kesi LUKUKI hazitajiki ni nyingi na zote hamna hanata 1 aliyofungwa... Sasa utasemaje huyo mtu hajui sheria?
Kesi gani kashinda na ipo kwenye Tanzania Law Reports? Hana kesi hata moja.
 
Fedha za kumlipa Lissu mafao yake ya ubunge zilikuwa kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge kama ambavyo fedha za kumtibu aliposhambuliwa zilikuwepo. Idhini ya Bunge haikuhitajika bali wote waliohudumu 2015-2020 walistahili kulipwa. Matibabu yake hayakugharimiwa na Bunge kwa sababu ya matumizi mabaya ya madaraka na uvunjaji wa sheria uliotamalaki hapa nchini. Lissu hakulipwa mafao yake kwa hisani ya Rais bali kwa mujibu wa sheria na haki.
 
Tundu Lissu hana hoja. Kwanini anataka Rais aingilie Mhimili wa Binge? Dhana ya mgawanyo wa madaraka na utawala Bora iko wapi hapa?.

Makosa yapo na yalifanywa na Magufuli na Ndugai. Sioni kwa nini tunayahamishia kwa Rais Samia
Kwamba MADARAKA amekaimishwa kayakubali ila,


Makosa ya Magu hayahamishiki.

Tusubiri.
 
Sawa mkuu.

Ikiwa fedha ya kumlipa Tundu Lissu kwa ubunge wake wa 2015-2020 ilikuwepo na ilikwishapitishwa na bunge, basi Miraji Mtaturu (mbunge wa Ikungi) alilipwa mishahara, posho na pensheni kwa hisani ya Rais na sio kwa mujibu wa sheria, sababu kuu ni kuwa jimbo moja haliwezi kuwa na wabunge wawili kwa wakati mmoja.

Sasa Tundu Lissu kwa kuwa yeye ni mhusika kwenye saga hili alipaswa kuhoji kuwa sawa amelipwa mafao yake, Rais aeleze alitoa wapi fedha ya kumlipa Mtaturu? Rais aliweza vipi kumlipa Lissu ilhali anajua kuwa kuna maamuzi ya Mahakama yanayosema kuwa Lissu sio mbunge tena na nafasi yake ilikuwa wazi kisheria (wakati huo)? Alipaswa kumshangaa Rais kwa kutoheshimu maamuzi ya Mahakama maana ni dalili kubwa kabisa ya mtu asiyejali sheria. Kukaa kimya ilikua ni kama kuunga mkono hoja uvunjwaji wa katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…