Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

With all due respect to the honorable President of URT Kuliko kuendelea kung'ang'ania kwamba amevaa nguo (read amechagua majaji wenye Sifa), wakati dunia nzima ikimuona kwamba yuko UCHI wa mnyama kwanini asikubali tu kwamba alikosea na kutengua uteuzi wa hao majaji wasio na sifa.

Kama anafikiri mambo haya yanaishia humu humu nchini he is terribly wrong. Kama anabisha afanye mahojiano na HARD TALK ya BBC aone wazungu wanavyofuatilia blunders zake. Kutokuwa MAKINI kwa JK kunatu COST sana sisi kama nchi. Kwani nje ya nchi wanamchukulia pia hivyo hivyo kwamba JK ni RAIS asiye MAKINI na SERIOUS.
 
Halafu huyu Mbaruku masikini ya Mungu si ndiye aliyepangwa awali kusikiliza Rufaa ya Lema, akawahi kujitoa sijui kwanini, nafasi yake kwenye jopo ikachukuliwa na Jaji Mkuu, ambaye naye kuna uzi humu unasema kajitoa, na nafasi yake kuchukuliwa na Jaji Bernard Luanda.

Huyo mwingine CV yake tu ilitosha kumpiga chini. Ukishatimuliwa kwenye utumishi wa umma kwa makosa ya jinai, hutakiwi kurudi humo tena. Mbaya zaidi kurudi kwenye nafasi ya kutoa haki wakati mwenyewe ni reference ya ubadhilifu. Nafikiri ndio maana hawapewi hata kesi za kusikiliza kwa sababu ya "makandokando" (msamiati wa Andrea Chenge) yao!
 
Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.

Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.
. Mheshimiwa Tundu Lisu (Mb) ameeleza kwa kiina mapungufu. Sasa kama Rais alipelekewa majina, hakujua kama hawana sifa za uteuzi kwa mujibu wa sheria, kinachotakiwa ni kubatilisha uteuzi na kuwaomba radhi watanzania kwa kukosa umakini katika uteuzi huu, kumshukuru Mheshimiwa Tundu Lisu kwa kufuatilia kwa makini. Dawa isiwe kutupiana mpira. Penye ukweli lazima tukubali ukweli na kujutia makosa tuliyoyafanya pasipo kukusudia. Kama tunazidi kung'ang'ania tutafikiria tulifanya makosa kwa makusudi na hatupotayari kukiri dhambi zetu na kuziacha.
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action
 
Huyo ndo Kikwete. Jamani, tufanyie kazi katiba mpya hata tukiwa na Rais boga imuongoze na kumuwajibisha katika utendaji wake. Imagine vyeo vingapi Vasco anavigawa namna hii...tutaangamia bandugu...!
  1. Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku
  2. Jaji Fatuma Masengi
  3. Jaji Latifa Mansoor
  4. Jaji Mwendwa Malecela

Tafadhali mwenye CV za hawa jamaa aziweke tung'arishe macho.
 
Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action
Na Jaji Mwendwa Malecela ni Muislam? Sisi hapa hatuungalii dini tunaangalia uteuzi mbovu anaofanya Kiongozi wetu mkuu unaotugharimu watanzania wote. Kama na wewe una majina ya watu wengine yaweke hapa.
 
Kikwete anadai anapelekewa majina na kamati ya mahakama. Anachorekebisha yeye ni kuangalia usawa wa kijinsia( na wa KIDINI kwa siri sana). KATIBA yetu ya JMT kwa sasa inatutesa sana kwenye teuzi hizi za Rais.
Unanikumbusha Misri na rais Mohamed Morsi.
 
Nchi hii tunaongozwa na mtu mwenye kichwa cha NAZI au anayetumia kichwa kufugia nywele (by Werema)!! Yaani wewe unaletewa majina tu kwamba teua hawa na wewe kweli unasaini kuidhinisha uteuzi? Yaani hutafuti kujiridhisha kwenye CV zao? Rais mvivu wa kusoma huyu wa nini sasa?

Huyu alikuwa anafaa kazi ya disco tu wala siyo kuongoza watu! Kwa kweli TZ tuna hasara kuwa na Rais mvivu, dhaifu na mpuuzi kama huyu!

Sasa hao wanaompinga Lissu waje hapa na facts tuone nani mkweli basi!! Na huyu mwandishi naye kama hakuwapigia simu hao waliokuwa wanatetea tusikie majibu yao, basi atakuwa hajamaliza kazi?
 
Kwa wale wanaofuatilia mambo,inamaana tundu lisu ndie anaejua sheria kuliko watz wote?kama jibu ni hapana kwanini kama kuna ukweli na hao wengine mbona hawatoi ufafanuzi?tundu atakuwa ana wivu tu hana jipya.

Huyo Tindu Lissu ni Mdini tu.Amewalenga waislamu ili awachafue.Christian Democratic Movement in Action
Wakuu jibuni hoja kwa hoja.

Katiba inatoa sifa za majaji. Watu walioteuliwa kuwa majaji bila sifa hizo wametajwa na sababu zimewekwa wazi. Kujibu hoja ya Lissu: ama uoneshe kuwa Lissu amepotosha vigezo vilivyowekwa na katiba (uvitaje hivyo ambavyo ni sahihi), au uoneshe kuwa waliotajwa wanakidhi vigezo vilivyowekwa na katiba alivyovitaja Lissu.

Tunataka kujua vigezo gani vimetumiwa kuwateua hao majaji.

Ni hoja dhaifu kuhoji kuwa "ina maana Tundu Lissu ndie anaejua sheria kuliko watz wote?" au kukimbilia single iliyozoeleka ya udini. Hoja za namna hii nashangaa zinafikaje kwenye jamvi hili, linalopaswa kuwa jamvi la Great thinkers.

Yawezekana kuna wengi wanaoona hilo, lakini ni waoga au wachumia tumbo wanaoogopa kupoteza nafasi zao. Watanzania wenye ujasiri kama Lissu ni wachache, na ndio wanafaa kuwakilisha wananchi, kwani kwenye ukweli hawaogopi yeyote bali wanaisimamia serikali kikamilifu, ambayo ndiyo kazi ya msingi ya bunge.
 
Wana JF,

The list of incompetent judges is long. I am compiling the list with the supporting documents. To put the pants down of those who have replied to what Tundu Lissu said, soon it (the list of cincopetent judges) will be downloaded in this forum. Sioni mantiki ya kuteua majaji wengi (bila kufuata taratibu zilizopo) kama wanaoteuliwa wenyewe hawawezi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria. I am informed by a friend that a High Court judge delivered a ruling which contained no provision of the law to support his decision. Worse enough, where he was supposed to write the provision of the law to support his decision, this judge just left some blanks, but yet he signed the ruling and upon the same being requested by the aggrieved party, the same was issued to that party as it is (containing blanks in the places where the provisions of the law ought to have been sited).

Tatizo lipo kwenye mteuzi (appointing authority). He is taking our country to a deep grave as far as the administration of justice in Tanzania is concerned

Tunaisubiri mkuu!
 
Kwa wale wanaofuatilia mambo,inamaana tundu lisu ndie anaejua sheria kuliko watz wote?kama jibu ni hapana kwanini kama kuna ukweli na hao wengine mbona hawatoi ufafanuzi?tundu atakuwa ana wivu tu hana jipya.
Hii yako nayo ni hoja kwako??? Nadhani na wewe una elimu ya chekechea kama huwezi kuelewa hoja ya TL
 
Lissu yupo sahihi kwa 100%..kata kubali,bwa bwaja :smile:


  • smile.png

 
Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.

Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.
Kimsingi ulichokitaja hapa kiongozi hata wanaojibu hizo hoja kwa ujumla jumla nadhan wanajua ndicho wanachopaswa kufanya. Na kama hawajui ka hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanya basi inabidi tuwe na wasiwasi na utumishi wao. Kinachoonekana hapa kwa huu ukwepajikwepaji wa hoja kwa kutoa majibu ya jumla jumla (Esther Wassira referred to Cheap Answers) ni kushindwa kujibu hoja ambayo ipo very specific mana Lissu kataja majina. Suluhisho ni kuwavua vyeo hao majaji wasio na sifa na sio kuleta majibu ya kijinga kwa wananchi!!!
 
Kikwete anadai anapelekewa majina na kamati ya mahakama. Anachorekebisha yeye ni kuangalia usawa wa kijinsia( na wa KIDINI kwa siri sana). KATIBA yetu ya JMT kwa sasa inatutesa sana kwenye teuzi hizi za Rais.

WildCard, kama kuna kiini macho basi ni haya madudu yaliyomo ndani ya katiba yetu hii. Kwa mfano ibara ya 112 (1) ndio inayounda Tume ya utumishi wa mahakama, ambayo imepewa jina la tume ya ushauri wa uteuzi wa majaji na ajira ya mahakimu wa mahakama Tanzania bara.

Ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo inatamka kuwa:
Wajumbe wa tume hiyo watakuwa;
a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti Mteule wa Raisi angalia Ibara ya 118(2) ya katiba
b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule wa Rais angalia ibara ya 59(1) ya katiba
c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa
atakayeteuliwa kwa ajili hiyo na Rais Mteule wa Rais angalia ibara ya 118(3) ya katiba na bado anateuliwa
baada ya kushauriana na Jaji Mkuu na Rais kuwa mjumbe wa Tume angalia ibara 112 (2) (c)
d) Jaji Kiongozi Mteule wa Rais angalia ibara ya 109(1) ya katiba
e) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais Wateule wa Rais angalia Ibara 112(2) (e)

Kwa vile hawa wote wameteliwa na Raisi kutokama na nyadhifa zao lazima kwa hali yoyote hiyo hawatampinga. Mtu yoyote mwenye akili akiona hii lazima atasema uteuzi wa majaji pamoja na kuwa anatokana na mapendekezo ya tume ya mahakama, kiukweli mapendekezo hayo ni ya Rais kwani tume yote ni ya Rais.

Tuache kuwa wabishi bila sababu, tuionee huruma nchi yetu, muundo huu haufai hata kidogo katika kuendeleza utawala wa sheria.

Tatambishia sana Tundu lakini kwa muundo huu wa tume ni vigumu sana kusema vinginevyo.

Kama waungwana tukubali maneno ya Tundu lissu na kutafuta njia mbadala ya kupata majaji kwa uwazi zaidi sio huu utaratibu wa sasa uliogubikwa na umangimeza.
 
Back
Top Bottom