Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Kimsingi ulichokitaja hapa kiongozi hata wanaojibu hizo hoja kwa ujumla jumla nadhan wanajua ndicho wanachopaswa kufanya. Na kama hawajui ka hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanya basi inabidi tuwe na wasiwasi na utumishi wao. Kinachoonekana hapa kwa huu ukwepajikwepaji wa hoja kwa kutoa majibu ya jumla jumla (Esther Wassira referred to Cheap Answers) ni kushindwa kujibu hoja ambayo ipo very specific mana Lissu kataja majina. Suluhisho ni kuwavua vyeo hao majaji wasio na sifa na sio kuleta majibu ya kijinga kwa wananchi!!!Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.
Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.