HIVI NDIVYO KATIBA INAVYOSEMA KUHUSU UTEUZI WA MAJAJI:
Ibara ya 109 kifungu cha 6:Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (8) ya ibara hii, mtu aweza tu kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya kuu ikiwa ana sifa maalumu, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (7) ya ibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi.
Kifungu cha 7: Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo za (6), (8) na (10) ya ibara hii, sifa maalum maana yake ni mtu aliye na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na mamlaka ya ithibati Tanzania na -
(a) amekuwa hakimu.
(b) amefanya kazi katika utumishi wa umma akiwa na sifa za kufanya kazi ya uwakili au ni wakili wa kujitegemea.
(c) ana sifa ya kusajiliwa kuwa wakili, na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.
Kifungu cha 8: Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka kumi, lakini mtu huyo anauwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya jaji wa mahakama kuu na kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutengua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa jaji wa Mahakama kuu.