rais analaumiwa na baadhi ya wanajf pamoja na mh, Tundu Lissu. wanajf wale mnaoamini rais amekosea. na mmetoa michango yenu humu baadhi yenu pia mnakosea, kwani suala hili, iwe kuna makosa au hakuna makosa yaliyofanywa na rais, si sifa tena za kisiasa kwa chama fulani ni Tanzania kwanza, wengi wanadharau mawazo ambayo ndani yake kunaharufu ya uchamachama matokeo yake issue inakosa mashiko. kwa suala hili mimi binafsi linaniachia maswali mengi saana na najiuliza hivi hii nchi yetu kweli ina wanazuoni. kweli ina wasomi wenye uchungu na nchi yao. kweli kuna vitivo vya sheria kwenye vyuo vyetu , kwanini Mungu amewafanya hivi wasomi wetu hawa;hawaoni kama rais hana makosa/anamakosa, hawaoni sababu ya kumfokea/ kumuunga mkono lissu? . kuna sababu gani ya kuwa na baadhi ya hawa kwenye taifa, jaji Agustino Ramadhani, jaji Joseph Warioba, prof Ibrahim Lipumba, prof Safari, dr Lwaitama,dr Bana, dr MKumbo, dr Lamwai, MH Mabere Marando, na wengine wengi wenye majina na wasio na majina, vilevile TISS mko wapi? na maneno makali dhidi yenu nadhani mmeelewa nini? maana yangu mko hatua nyingi nyuma jamii yetu sasa si ile iko njema badilikeni, mnawafanya wananchi wawe na maswali mengi juu ya mustakabali wa taifa lao.