Bezecky
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 494
- 897
Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,
Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.
Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali
View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4
==============================================
Kuhusu Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Tundu Lissu amesema:
"Kiuhalisia kama sio kisheria, nchi yetu sasa iko kwenye utawala wa kiimla usiokubali ushindani wa kiuchaguzi wa wazi wazi. Kama baada ya chaguzi hizo mbili (2019 na 2020) kuhusu aina ya utawala wa kiimla tulionao mashaka hayo yameondolewa na Uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka huu"
"Kuanzia sasa hakuwezi kuwa na ubishi miongoni mwetu kuwa bila kupigania na kubadilisha mfumo mzima uliopo wa kikatiba, kisheria na kitaasisi wa mfumo mzima wa Uchaguzi, hakutakuwa tena na uwezekano wa kuwa na Uchaguzi ulio wa wazi na haki"
"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"
"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"
"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"
Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.
Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”
Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.
Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”
"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"
"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"

- Lissu ameishauri kamati kuu kuwepo na mabalozi wa nchi rafiki kama watazamaji na waangalizi wa uchaguzi wao wa ndani ya chama:
"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"
- Kuhusu ukomo wa madaraka kwa wabunge na madiwani wa viti maalum ndani ya CHADEMA, Lissu amesema:
"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"
"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"
- Lissu pia ameonesha kushangazwa na watu ndani ya CHADEMA wanaopinga hoja ya ukomo wa madaraka:
Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.
Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”
Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.
Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”
- Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
- Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema: