Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Lissu akiwa mwenyekiti Kuna mawili:-

1. Nchi kuingia kwenye machafuko, maana anafahamika jinsi anavopenda Shari

2. Chadema Kua na mwenyekiti hewa, Endapo akitimkia ubelgiji Kama kawaida yake (Kuhofia maisha yake).
JF tuna slogan ya kuheshimu mawazo ya kila mtu, lakini yapo ya kijinga pia ila hayo tunayasikiliza tuu, hayatufikirishi bali tunayapuuza kama haya.
 
wakati lissu anajiunga chadema, katiba ya chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi, yeye akachana kurasa kwenye katiba tena bila kuhusisha vikao halali vya chama, akina zitto kafulila kitila mkumbo walipinga hili, lakini yeye akawaundia mbinu akawafukuza chamani, leo huyohuyo anatuletea story hizi, anataka kutatua tatizo alilolitengeneza mwenyewe
Miaka yote hii yeye alikuwa mmoja wa hao wenye chama. Leo anawalaumu hao hao waliohakikisha anafika alipofika sasa. Nyalandu alilalamika kuchezewa faulu lakini akapuuzwa. Wakina Lwakatare waliondolewa kinamna, yeye akiwa mshiriki.
Badala ya kulalama, anatakiwa aiambie Kamati Kuu ya chama chake namna ya kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na uwazi.

Amandla....
 
Tunapowaambia CCM tunataka uchaguzi huru na wa haki, basi na CDM ihakikishe chaguzi zake zinakuwa huru na haki, tutapozungumzia ukomo wa uongozi na kufuata Sheria na katiba basi na Sisi CDM tuwe mfano.

CCM sio chama rafiki Kwa Watanzania bali CCM ni kikundi cha watu wanaotumia chama na siasa kuwaslave Watanzania na kujinufaisha na familia zao kupitia rasirimali na nguvu za watanzania.

Watanzania wanahitaji utawala na system mpya zitakazosimamia rasirimali na Mali za watanzania Kwa maslahi ya Watanzania.
Njia mbaadala wa kuitoa CCM ni kupitia chama na watu wenye msimamo migumu isiyoyumbishwa ili waweze kuisimamia Nia ya dhati ya Watanzania kuendeleza nchi yao.

Ni ngumu sana Watanzania kuitoa CCM kwa CDM ya Mbowe ambayo ilishatekwaa kitambo na wahuni walewale walio nyuma ya CCM wakiwa na lengo moja tu lakuwaslave Watanzania.
 
Yake matusi,ngebe na mafumbo yake kwny press conference, Mara aseme "tuna Raisi uchwara" n.k

Akizileta awamu hii, hakuna mwenye muda WA kumpeleka mahakamani.

Tumeshuhudia wengi TU wanavohukumiwa underground,

afu Maza anapiga Kimya,
Yaan Kama vile hamna kilichotokea.

Kila mtu anaendelea na ishu zake.
Mtuakikuita mpu...vu hajakosea. Wakati watu wanalaani hayo wewe unayapigia chapuo!
 
analalamika chadema ni mali binafsi ya badhi ya viongozi nqŵadhani anamnanga mbowe hapo
Kazi kulalama na kudai Chadema ni mali binafsi. YEYE alikuwa Makamu Mwenyekiti alifanya nini?Kulaumu na blame game ni rahisi sana kwa watu wasio na maono na ufumbuzi.Kila hotuba ni kulalamika tu.
 
Yake matusi,ngebe na mafumbo yake kwny press conference, Mara aseme "tuna Raisi uchwara" n.k

Akizileta awamu hii, hakuna mwenye muda WA kumpeleka mahakamani.

Tumeshuhudia wengi TU wanavohukumiwa underground,

afu Maza anapiga Kimya,
Yaan Kama vile hamna kilichotokea.

Kila mtu anaendelea na ishu zake.

Hizo hukumu ndio hatuzitaki na hawa mnaowapa hizi hukumu kila siku wataonekana washindi na upande mwingine mtadhidi kuumiza watu na mwisho wake itaback fire na kuwarudia wahusika hao hao tunaowasifia.

Kuua na kuumiza watu bila sababu za msingi ni kuja kuuingiza nchi kwenye machafuko tu maana watu hawa hawa wakichoka na kutafuta njia yakujilinda hugeuka kuwa hatari na kuiingiza nchi kwenye machafuko.
 
Mtuakikuita mpu...vu hajakosea. Wakati watu wanalaani hayo wewe unayapigia chapuo!
Sijayapigia chapuo,
Ila nmeongea uhalisia uliopo
Hata nisipoyasema, sote twajua yapo

Ni vema tukapeana tahadhari,
maana siasa Ni mchezo mchafu sana
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4

Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,

Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.

Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali👌👌

==============================================

  • Lissu ameendelea kupigilia msumari hoja yake ya ukomo wa madaraka ambapo amedokeza kuwa ni ngumu watu kuendelea kujitolea CHADEMA iwapo kutakuwa hakuna mfumo wa kurithishana madaraka ndani ya chama hicho.

"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"

"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"

  • Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
"Huu ulikuwa ni mwaka wa George Sanga mfungwa mwingine wa kisiasa ambaye amemaliza miaka 4 na amemaliza mwaka wa 5 ndani ya gereza la Njombe akiwa ni mhanga wa siasa za kiuchaguzi za John Pombe Magufuli na kazi inayoendelea na Samia Suluhu Hassan."

  • Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema:
"Kuna wale ambao kwa sababu ya maslahi na vijimanufaa fulani fulani wamejisahau na kuanza kumsifia na kumsafisha utawala wa kiimla wa Samia Suluhu Hassan"

"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"

"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"

Amesema atawapa Katiba Mpya au? 😂😂😂😂
 
Hizo hukumu ndio hatuzitaki na hawa mnaowapa hizi hukumu kila siku wataonekana washindi na upande mwingine mtadhidi kuumiza watu na mwisho wake itaback fire na kuwarudia wahusika hao hao tunaowasifia.

Kuua na kuumiza watu bila sababu za msingi ni kuja kuuingiza nchi kwenye machafuko tu maana watu hawa hawa wakichoka na kutafuta njia yakujilinda hugeuka kuwa hatari na kuiingiza nchi kwenye machafuko.
Sahii kabisa mkuu
 
wakati lissu anajiunga chadema, katiba ya chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi, yeye akachana kurasa kwenye katiba tena bila kuhusisha vikao halali vya chama, akina zitto kafulila kitila mkumbo walipinga hili, lakini yeye akawaundia mbinu akawafukuza chamani, leo huyohuyo anatuletea story hizi, anataka kutatua tatizo alilolitengeneza mwenyewe
LISU NJAAAAAA ili kuna wajinga awajamuelewa uyo jamaa.
 
Back
Top Bottom