Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Kwani joshua mutale (mb) nae anaongea lini au bado wako location kutengeneza igizo lingine
 
Yaani wewe unaweza ignore veteran politician, kwa kuweka njuka bungeni.

Akili zake zinamtosha mwenyewe.

Mwanasiasa ajajingea ufuasi kwenye jamii umuweke bungeni, utoe mwenye influence kwenye jamii. Kisa katiba ya chama.

Akili zake zinamstosha mwenyewe, Lissu ni mwanaharakati sio mwanasiasa.
Sasa huo u-veteran unasaidia nini kama haumuwezeshi muhusika kuwashawishi Wananchi wamchague? Pengine wewe ndo huelewi dhana ya POSITIVE DISCRIMINATION.

Mtu yeyote anayelitakia mema taifa hili, atatamani kuwepo na upinzani imara, na huo upinzani imara unahitaji uwe na watu wenye haiba kama ya Tundu Lissu.

Chadema ikisuasua, watakaoathirika ni walalahoi. CCM sababu haitakuwa tena na cha kuhofia, haitahitaji wapiga debe kama wewe, bali watagawana vyeo kwa kuzingatia ukwasi, undugu na urafiki. Nyinyi wengine labda itakoee zali la mtende kuota jangwani.

Tunaweza kuitetea CCM , ila tusiombee mabaya vyama vinavyokosoa mwenendo wa uendeshaji wa taifa letu.
 
Lissu akiwa mwenyekiti Kuna mawili:-

1. Nchi kuingia kwenye machafuko, maana anafahamika jinsi anavopenda Shari

2. Chadema Kua na mwenyekiti hewa, Endapo akitimkia ubelgiji Kama kawaida yake (Kuhofia maisha yake).
..ni maoni yako, lakini taasisi sio mtu mmoja, lissu akiwa makamu alikuwa anaongoza vikao akiwa nje, shida ilikuwa nn?
 
Alikuwa mmoja wa wanasheria wa chama wakati ukomo unaondolewa. Sasa hivi anamlalamikia maamuzi yaliyofanyika chini yake. Ni sawa na kutengeneza tatizo halafu ujinadi kuwa unaenda kulitatua
..kwani kubadilisha kitu ni dhambi? Katiba zinabadilishwa tu mkuu
 
Yaani wewe unaweza ignore veteran politician, kwa kuweka njuka bungeni.

Akili zake zinamtosha mwenyewe.

Mwanasiasa ajajingea ufuasi kwenye jamii umuweke bungeni, utoe mwenye influence kwenye jamii. Kisa katiba ya chama.

Akili zake zinamstosha mwenyewe, Lissu ni mwanaharakati sio mwanasiasa.
Hata wewe akili zako zinakutosha kuosha vinyeo vya vizee vya kizungu
 
Tunapowaambia CCM tunataka uchaguzi huru na wa haki, basi na CDM ihakikishe chaguzi zake zinakuwa huru na haki, tutapozungumzia ukomo wa uongozi na kufuata Sheria na katiba basi na Sisi CDM tuwe mfano.

CCM sio chama rafiki Kwa Watanzania bali CCM ni kikundi cha watu wanaotumia chama na siasa kuwaslave Watanzania na kujinufaisha na familia zao kupitia rasirimali na nguvu za watanzania.

Watanzania wanahitaji utawala na system mpya zitakazosimamia rasirimali na Mali za watanzania Kwa maslahi ya Watanzania.
Njia mbaadala wa kuitoa CCM ni kupitia chama na watu wenye msimamo migumu isiyoyumbishwa ili waweze kuisimamia Nia ya dhati ya Watanzania kuendeleza nchi yao.

Ni ngumu sana Watanzania kuitoa CCM kwa CDM ya Mbowe ambayo ilishatekwaa kitambo na wahuni walewale walio nyuma ya CCM wakiwa na lengo moja tu lakuwaslave Watanzania.
..uko sahihi, chadema hii ya sasa hata operesheni mikoani hakuna, ni kwa kushitukiza tu.Lissu aamshe chama mikoani na kutia matumaini mapya
 
TAL ni mwanaharakati! Anachosema vifanyike kwenye chama ,hakuna vikao ndani ya chama?
Chama kisipofanya,atalaumu nani na atakifanyia nini?
 
Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,

Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.

Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali



View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4

==============================================

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Tundu Lissu amesema:

"Kiuhalisia kama sio kisheria, nchi yetu sasa iko kwenye utawala wa kiimla usiokubali ushindani wa kiuchaguzi wa wazi wazi. Kama baada ya chaguzi hizo mbili (2019 na 2020) kuhusu aina ya utawala wa kiimla tulionao mashaka hayo yameondolewa na Uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka huu"

"Kuanzia sasa hakuwezi kuwa na ubishi miongoni mwetu kuwa bila kupigania na kubadilisha mfumo mzima uliopo wa kikatiba, kisheria na kitaasisi wa mfumo mzima wa Uchaguzi, hakutakuwa tena na uwezekano wa kuwa na Uchaguzi ulio wa wazi na haki"



  • Lissu ameishauri kamati kuu kuwepo na mabalozi wa nchi rafiki kama watazamaji na waangalizi wa uchaguzi wao wa ndani ya chama:

"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"


  • Kuhusu ukomo wa madaraka kwa wabunge na madiwani wa viti maalum ndani ya CHADEMA, Lissu amesema:

"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"

"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"



  • Lissu pia ameonesha kushangazwa na watu ndani ya CHADEMA wanaopinga hoja ya ukomo wa madaraka:
“Mimi nimependekeza kurudisha ukomo wa madaraka katika mfumo wa uongozi wa chama chetu, na katika uwakilishi wa wanawake bungeni na katika halmashauri za serikali za mitaa.

Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.

Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”

Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.

Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”


  • Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
"Huu ulikuwa ni mwaka wa George Sanga mfungwa mwingine wa kisiasa ambaye amemaliza miaka 4 na amemaliza mwaka wa 5 ndani ya gereza la Njombe akiwa ni mhanga wa siasa za kiuchaguzi za John Pombe Magufuli na kazi inayoendelea na Samia Suluhu Hassan."

  • Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema:
"Kuna wale ambao kwa sababu ya maslahi na vijimanufaa fulani fulani wamejisahau na kuanza kumsifia na kumsafisha utawala wa kiimla wa Samia Suluhu Hassan"

"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"

"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"

Tunaanza Upyaaaa!!
 
Back
Top Bottom