Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Lisu ni mtu mwadilifu na mkweli, ndiyo maana anataka watazamaji huru. Mtu yeyote mwenye akili timamu na dhamira njema, ataunga mkono wazo hilo. Uchaguzi ukiwa huru na wa wazi, na ulioshuhudiwa na watu huru, hata mgombea akishindwa, hawezi kupata pakusimamia kwa sababu mambo yote yalikuwa wazi, na watu huru wameshuhudia.
 
Amesema WAJUMBE wakodishiwe mabasi na pia wasipewe hela Ila bills zao ziwe covered na kamati maalumu itakayochaguliwa.

Amewaza vizuri Sana Ila asiache Ku-spread positivity na awareness Kwa 'WAJUMBE'
 
Watu wa chama chake ndo walitaka aongezewe muda.
 
Unataka uwenyekiti,unaanzisha vita na mwenyekiti aliyeko madarakani!
Na ushindi unautaka! Lissu alisomea wapi siasa?
 
Reactions: Tui
bora iingie huko ili tupate Katiba mpya na utawala wa haki & demokrasia, hakuna nchi hata moja ambayo ina katiba nzuri ilyopatijana bila machafuko. kafara ni muhimu ili kupata kilicho kizuri na bora
Shida ni nani atangulie
 
Amesema WAJUMBE wakodishiwe mabasi na pia wasipewe hela Ila bills zao ziwe covered na kamati maalumu itakayochaguliwa.

Amewaza vizuri Sana Ila asiache Ku-spread positivity na awareness Kwa 'WAJUMBE'
Wakodishiwe mabasi na huku hataki kutoa mchango wake wa milioni 30.Je anataka kutoa masharti bila kufanya lolote? Wakodishiwe mabasi na nani?Hiyo kamati maalum inapata pesa kutoka wapi?Bills ziwe covered bila pesa?Anawaza ujinga bila kuwajibika.Anataka free lunch kila kitu aamrishe kifanyike bila kujua pesa zinatoka wapi?Talking is cheap.
 
Hivi ccm mnataka MBOWE aongoze chama kwa miaka 30? Nyie ndio wa kumtetea MBOWE kweli? Au ni kumuogopa lissu?
 
Nia na mawazo ya TAL ni kuivuruga chadema na sio uongozi kwa sababu anajua kura hatapata kura za kutosha .
Nia ya kuvuruga chadema,hatafanikiwa na aliyemshauri amempoteza kisiasa kabisa.
 
Ruzuku tangia 2020 mwezi 11 mpaka Leo imetumika kufanya Kazi gani ?
 
Tafsiri ya uwezo wa mtu inatokana na uelewa wa mtafsiri.

Kuwaambia watu hawana uelewa wa kiwango cha Lissu kwa sababu wewe unamkubali. Maana yake ushahitimisha hao unaowaambia hawakupati hata wewe.

Ambitious
 
Reactions: Tui
Tuseme ukweli FAL ana maslahi sana na CDM either kwa biashara yake au mambo mengine hivyo kuachilia CDM kirahisi sidhani kama ataweza.
 
Watu wa chama chake ndo walitaka aongezewe muda.
Hadithi za JF

Ni sawa na kuamini Lissu alisema, Mbowe kaingia makubaliano ya nusu mkate; vitu ambavyo hakusema kabisa kama ulisikiliza press yake.

Be careful na nadharia za JF, wengine ni wasukuma agenda.

Magufuli ajawahi kutaka kuongezewa muda.
 
Reactions: Tui
Wee ni empty set kumɓe kwaio akae pèmbeni ili uovu uendelee badala ya kuchukua hatua kuingia madarakani kuondoa uovu huo pumbafuu
 
Ruzuku tangia 2020 mwezi 11 mpaka Leo imetumika kufanya Kazi gani ?
Ruzuku huwa zinatumika kuendesha Chama unafikiri zinangojea Uchaguzi wa Mwenyekiti?Chama kimenunua Jengo la Makao Makuu ya Chama Mikocheni.Na ruzuku pia huwa zinakaguliwa na CAG.Unafikiri unapewa tu na unatumia unavyotaka.Asilete tu masharti na malalamiko achangie na nyie changieni kama ni rahisi ili Mkutano ufanyike tarehe 21.
Ni mentality ya kitoto kusema kifanyike hiki na kile bila kujua pesa kama zipo.
 
Kwani Chama hakipokei ruzuku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…