Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Ungemsikiliza na kumuelewa usingeleta hii hoja yako. Yeye amesema ubunge wa viti maalumu ulilenga kuwapatia uzoefu wakina mama ili wawezi kwenda kugombea majimboni na kipindi kimoja cha miaka mitano kinatosha kabisa kumjengea mwanamke uwezo huo na akatoa mfano wa kina Halima Mdee ambaye alikuwa mbunge wa viti maalumu kwa kipindi kimoja tu baada ya hapo akaenda jimboni na kushinda tofauti na wengine waliofanywa wabunge wa viti maalumu wa kudumu hivyo kuwanyima wengine fursa hiyo.
JF ni vurugu machi atufuatiliani michango ya kila mtu.

Vinginevyo ungekuwa unanisoma; mimi sio mtu wa kutoa opinion bila ya kusikiliza ‘first hand account’ na mara nyingi uomba original source.

Hayo mengine ni hadithi zenu, hakuna amateurs kwenye siasa za juu; labda kwa majimbo. Vinginevyo hakuna chama makini kwa utashi wake kitaacha kuwapa nafasi za teuzi seasoned politicians na kuweka amateurs wakati siasa ni mchezo wa fitna na majungu.

Kuweka amateurs ni kutaka kuburuzwa.
 
Lissu akiwa mwenyekiti Kuna mawili:-

1. Nchi kuingia kwenye machafuko, maana anafahamika jinsi anavopenda Shari

2. Chadema Kua na mwenyekiti hewa, Endapo akitimkia ubelgiji Kama kawaida yake (Kuhofia maisha yake).
bora iingie huko ili tupate Katiba mpya na utawala wa haki & demokrasia, hakuna nchi hata moja ambayo ina katiba nzuri ilyopatijana bila machafuko. kafara ni muhimu ili kupata kilicho kizuri na bora
 
JF ni vurugu machi atufuatiliani michango ya kila mtu.

Vinginevyo ungekuwa unanisoma; mimi sio mtu wa kutoa opinion bila ya kusikiliza ‘first hand account’ na mara uomba original source.

Hayo mengine ni hadithi zenu, hakuna amateurs kwenye siasa za juu; labda kwa majimbo. Vinginevyo hakuna chama makini kwa utashi wake kitaacha kuwapa nafasi za teuzi seasoned politicians na kuweka amateurs wakati siasa ni mchezo wa fitna na majungu.

Kuweka amateurs ni kutaka kuburuzwa.
Nayaheshimu maoni yako japo siyakubali.
 
Uongozi ni falsafa.

Falsafa za lisu zinajulikana hata kwa wasio fatilia siasa
1.Kupinga rushwa
2.Kupinga ufisadi
3.Kupinga uongozi usiofata katiba na sharia

Sasa wajumbe kazi kwenu
Mbona pressure ipo juu Mkuu?Kila Press Conference analalamika tu.Leo kaja na masharti mengi ya namna anavyotaka Uchaguzi uwe.
Anataka viongozi wa dini wasimamie Uchaguzi kama observers eti ili haki itendeke.
Unawapa picha gani wajumbe wanaopiga kura kwamba huwaamini.Wanaopiga kura ndio waamuzi wa nani atakuwa Mwenyekiti kuwaamini na kufanya kampeni ili wakuchague ndio priority.Yeye ameanza kampeni mapema ili akienguliwa aseme kaonewa.Nafikiri ameona wazi hana nafasi ya kushinda. Hiyo scenario ya kuanza kampeni mapema Slaa ameitumia juzi kama kisingizio.
 
Ninashauri kamati kuu ya chadema Taifa, wafanye utaratibu wa kuwapima wagombea, ugonjwa wa akili kabla ya kufanya uchaguzi mkuu
 
Rundu Lisu ndiye tumaini pekee la Tanzania katika kuipata Tanzania ya haki na demokrasia, inayozingatia ukwi badala ya hadaa na unafiki.

Baba Mbinguni, muweza wa yote, tunaomba umlinde Tundu Lisu, mtu mkweli na mwadilifu, nao wenye kumfanyia hiana, wakakutane na mkono wako wenye nguvu.
 
Endeleeni kuhangaika......hata huyo Ndumila kuwili wenu akipita hana sifa tena, haaminiki, hata akiongea tutakuwa tunacbema tu
Wameishaondoka wengi Chadema zaidi ya Lissu bado Chadema ikabaki imara. Aliondoka, Zitto, Mwigamba, Mashinji, Nassari kutaja wachache. Ni kujidanganya kuamini eti Lissu akitoka Chadema itakufa. Kwanza ni wakuja tu, aliletwa na Mbowe na anaweza kuondolewa na Mbowe.
 
All the best on your wishful thinking.

Uhalisia bado kwa uongozi wa juu hata ndani ya CDM, let alone being a president (daah) I can imagine hasa kwa nchi yenye civil services mbovu kama ya Tanzania.
Labda kama unataka mtu wa kutengeneza Nuclear Reactor, then Lissu siyo chaguo sahihi. Ila vision ya utengenezaji wa hiyo reactor, anaweza kuisimamia.

Mpaka unaondoka hapa duniani, hautafikisha hata robo ya kipawa cha uongozi alicho nacho Lissu.

Lissu anaweza akisimamia nafasi yeyote si tu hapa TZ bali duniani kote, zingine ni porojo tu.

Mimi ni mwanachama hai wa CCM na ni Kiongozi pia. Ila, siwezi kubeza uwezo wa kiuongozi na kimaarifa wa Tundu Lissu.Ni mwanasiasa mtimilifu tuliye naye kwa wakati huu.
 
Wameishaondoka wengi Chadema zaidi ya Lissu bado Chadema ikabaki imara. Aliondoka, Zitto, Mwigamba, Mashinji, Nassari kutaja wachache. Ni kujidanganya kuamini eti Lissu akitoka Chadema itakufa. Kwanza ni wakuja tu, aliletwa na Mbowe na anaweza kuondolewa na Mbowe.
Sisi CCM pia hatutaki Lissu awe Mwenyekiti Chadema. Hafai Mbowe ndo anatakiwa aendelee kuwa Mwenyekiti wa chama chenu. Lissu atakiua Chama na kuvuruga makubaliano.
 
Back
Top Bottom