Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
JF ni vurugu machi atufuatiliani michango ya kila mtu.Ungemsikiliza na kumuelewa usingeleta hii hoja yako. Yeye amesema ubunge wa viti maalumu ulilenga kuwapatia uzoefu wakina mama ili wawezi kwenda kugombea majimboni na kipindi kimoja cha miaka mitano kinatosha kabisa kumjengea mwanamke uwezo huo na akatoa mfano wa kina Halima Mdee ambaye alikuwa mbunge wa viti maalumu kwa kipindi kimoja tu baada ya hapo akaenda jimboni na kushinda tofauti na wengine waliofanywa wabunge wa viti maalumu wa kudumu hivyo kuwanyima wengine fursa hiyo.
Vinginevyo ungekuwa unanisoma; mimi sio mtu wa kutoa opinion bila ya kusikiliza ‘first hand account’ na mara nyingi uomba original source.
Hayo mengine ni hadithi zenu, hakuna amateurs kwenye siasa za juu; labda kwa majimbo. Vinginevyo hakuna chama makini kwa utashi wake kitaacha kuwapa nafasi za teuzi seasoned politicians na kuweka amateurs wakati siasa ni mchezo wa fitna na majungu.
Kuweka amateurs ni kutaka kuburuzwa.