Ndo zakeUchaguzi watashiriki na ccm itashinda nafikiri atakimbilia nje tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo zakeUchaguzi watashiriki na ccm itashinda nafikiri atakimbilia nje tena
Tume Huru utaipata kwa katiba gani?Na ndicho alichosema Lissu.
Watasimamisha wagombea Nchi nzima bt watahakikisha Tume Huru ndo itasimamia uchaguzi huo.
Katiba mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.Tume Huru utaipata kwa katiba gani?
Yule yule aliyecharazwa masasi na maadui wa taifa hili🤔Huyu huyu Lissu nimjuae au kuna mwingine
Masasi?!Yule yule aliyecharazwa masasi na maadui wa taifa hili🤔
Ninachowaambia CHADEMA ni lazima wawe wakweli kwa wananchi wakati wote ili kuaminiwa katika wanayoyasimamia, kuliko kuendelea kuvungavunga huku wakiiujua ukweli wenyewe ulivyo.Nashukuru mkuu kwa kuliona Hilo la upatinanaji wa katiba Kwa sasa mpaka 2025 ni ngumu,
Linahitaji mchakato mrefu kidogo,
Tukumbuke mwakani uchaguzi serikali za mitaa then 2025 ni uchaguzi mkuu,
So maybe lifanyike mwaka huu huu lipitishwe kwanza kwenye bunge la bajeti then mchakato uanze,
Kitu ambacho Bado ni ngumu
Mkuu mbona unafunua siri kwenye vita.Kati ya kosa ambalo Chadema itakosea ni kutoshiriki Uchaguzi.
Uhalisia ni kuwa hakuna muda wa kupata hiyo katiba mpya kwa sasa na huo ndio ukweli wenyewe.
Ili wapate katiba nzuri inabidi wawe na wawakilishi bungeni, nje ya hapo ni kupoteza.
Watakiwa upigane ukiwa ndani
Wewe jielimishe acha ujinga.Utopolo. Kenya na Afrika ya Kusini waliandika katiba mpya na bado wanalia. Dawa ya kila kitu ni kuwajibika na kuwajibishwa kwa watawala na watawaliwa. Period.
Haya yote Chadema wanayajua. Yako kwenye Maridhiano. Mazungumzo hayajaisha...kumbuka Kauli ya Rais siku akiruhusu mikutano.Ninachowaambia CHADEMA ni lazima wawe wakweli kwa wananchi wakati wote ili kuaminiwa katika wanayoyasimamia, kuliko kuendelea kuvungavunga huku wakiiujua ukweli wenyewe ulivyo.
Katiba Mpya, ni muhimu sana, na inatakiwa waendelee kuishikia bango; lakini wakati huo huo kutokana na hali halisi ilivyo, hasa kutokana na ufinyu wa wakati, ni dhahiri wanajuwa katiba mpya haiwezi kuwepo kabla ya uchaguzi.
Kwa hiyo hili ni jambo linaloeleweka vizuri kwa wananchi.
Kinachotakiwa sasa wakitilie mkazo kabisa kabisa, ni kuhakikisha kwamba mazingira ya uchaguzi utakaokuja, ambao hata hivyo utafanyika chini ya katiba hiyo mbovu, ni lazima uwe wa HAKI, HURU na wa WAZI kabisa, ili matokeo yake yasiwe ya kutilia mashaka.
Hili linawezekana kabisa, na ndilo lililobaki kulifanyia mipango jinsi gani litatekelezwa.
Hii ndiyo kazi wanayotakiwa kuisimamia sasa hivi CHADEMA, kuliko kuendelea kutishia kutoshiriki uchaguzi kama hakuna katiba mpya.
Akina Mahera na wengine wote, kama hao wakurugenzi kusimamia uchaguzi, ni mambo yanayowezekana kuyarekebisha sasa hivi.
Hata huyo Rais, mwenye mamlaka yote dhidi ya Katiba iliyopo sasa, atatambua kwamba kufanya maamuzi yanayovuruga uchaguzi ni njia iliyo wazi kumwondoa madarakani kwa nguvu, kama siyo kumpeleka ICC kabisa.
Kwa hiyo hatakuwa na uthubutu wowote wa kuingilia maamuzi ya wananchi watakayofanya wenyewe kuhusu viongozi wanaotaka wawaongoze.
Hii ndiyo kazi inayowasubiri CHADEMA tangia sasa hadi baada ya uchaguzi 2025. Wasianze kutafuta visababu pembeni.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA mh Tundu Antipas Lissu amesema yeye kugombea Urais wa JMT ni hadi ipatikane Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Kimsingi CHADEMA tutaonekana Watu wa ajabu sana kama tutashiriki Uchaguzi mkuu wa 2025 kwa Katiba hii na Tume hii ya Uchaguzi amesema Lissu.
Lissu amesema CHADEMA ndio Chama pekee cha Upinzani nchini ndio sababu walipokataa kujumuishwa Kwenye Kikosi Kazi cha Prof Mkandalla na Kikosi chenyewe kikafa ganzi hapo hapo na hakisikiki tena popote.
Chanzo: ITV
Hakuna kitu kigumu. Rasimu ya Warioba iko tayari. Rais akiamua hata mwaka huu huu inapatikana. Kwani marekebisho ya Rasimu inachukua miezi mingapi? Ikienda mingi ni 3months only.Nashukuru mkuu kwa kuliona Hilo la upatinanaji wa katiba Kwa sasa mpaka 2025 ni ngumu,
Linahitaji mchakato mrefu kidogo,
Tukumbuke mwakani uchaguzi serikali za mitaa then 2025 ni uchaguzi mkuu,
So maybe lifanyike mwaka huu huu lipitishwe kwanza kwenye bunge la bajeti then mchakato uanze,
Kitu ambacho Bado ni ngumu
Wewe ni mwana ccm mambo ya chadema achana nayoSometimes uwa nahisi tundu lissu ni wakala wa CCM ambae anatumika kuwapa ccm ushindi mwepesi tena wa bure kabisa
Coz hata wakigoma sio kama uchaguzi hautofanyika hapana,
Uchaguzi utakuwepo na viongozi wataapishwa na Maisha yataendelea then yy anapata faida gani?
Ningemwelewa ishu yake kama angekuwa na uwezo wa kusimamisha uchaguzi, au kuandamana uchaguzi usifanyike, but hakuna kitu anaweza kufanya zaidi ya kutoroka na kwenda ulaya
Huyu jamaa Mwangalieni vizuri
Hata kwenye mambo ya viti maalumu, ni yy ndio alileta siasa zake za majitaka na akaondoka zake eeeh what happen? Wakina mdee si wapo bungeni?
Hivi hizi taarifa nyingine huwa mnazitowa wapi?wakati kipindi kimerushwa wote tumekifuatiria hakuna kauli kama hiyo aliyoisema,tena ni kwa kiswahili kabisa,hayo maneno huwa mnayatoa wapi na kwa faida gani??!Makamu mwenyekiti wa CHADEMA mh Tundu Antipas Lissu amesema yeye kugombea Urais wa JMT ni hadi ipatikane Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Kimsingi CHADEMA tutaonekana Watu wa ajabu sana kama tutashiriki Uchaguzi mkuu wa 2025 kwa Katiba hii na Tume hii ya Uchaguzi amesema Lissu.
Lissu amesema CHADEMA ndio Chama pekee cha Upinzani nchini ndio sababu walipokataa kujumuishwa Kwenye Kikosi Kazi cha Prof Mkandalla na Kikosi chenyewe kikafa ganzi hapo hapo na hakisikiki tena popote.
Chanzo: ITV
Mkuu, mimi hayo ya mazungumzo ya "maridhiano", sina ufahamu nayo, na kama wewe unataarifa zake, basi jaribu kutudokeza nasi tuwe na ufahamu juu yake.Haya yote Chadema wanayajua. Yako kwenye Maridhiano. Mazungumzo hayajaisha...kumbuka Kauli ya Rais siku akiruhusu mikutano.
magufuli alimuua BEN SANANE kwa mikono yake akiwa ikulu.Makamu amechalala.
Wait and seeMkuu, mimi hayo ya mazungumzo ya "maridhiano", sina ufahamu nayo, na kama wewe unataarifa zake, basi jaribu kutudokeza nasi tuwe na ufahamu juu yake.
Kwa nini nayasema haya.
Viongozi wa CCM wameonyesha kwa muda mrefu sana kuwa wasiokuwa na uaminifu; kuwa watu wanaolinda maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya nchi. Kwa hiyo, binafsi siwaamini. Wawe wale waliokuwa wakitumia miguvu mingi na kuumiza watu ambao hawakukubaliana nao, au hawa sasa hivi wanaotumia mbinu za kulainisha, bila kuumiza, lakini wakijuwa matokeo yatakuwa ni yale yale ya wao kuendelea kubaki madarakani wakifanya madudu yale yale wanayofanya miaka yote.
Kwa hiyo, mimi ninawatahadharishahawa CHADEMA, wasilazwe usingizi kabisa, na kuja kustuka wakati umepita kwamba wamekwishaachwa kwenye mataa.
Hata hivyo, kama kweli CHADEMA wanayafahamu hayo maridhiano kama unavyodai wewe hapa, iweje sasa wawe wanasikika tena kwamba "hawatashiriki uchaguzi kama hapatakuwepo na katiba mpya"?
Au umesahau yanayozungumziwa kwenye mada hii?
Nimesoma baadhi ya michango yako kwenye mada hii.Wait and see