James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Nafikiri ukisoma hapo chini jinsi JokaKuu alivyokujibu utajua kati ya mimi na wewe nani mjinga. Napata mashaka sana kama kweli kazi yako ni kufundisha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hewala mzee; mimi ni mwalimu na muongeaji mzuri sana lakini najua kuwa kuwa raisi haihitaji sifa ya uongeaji bali kichohitajiwa ni vision, decisiveness na fairness. Mtu asiyekuwa na vision kuwa anataka kuipeleka wapi nchi na hayuko decisive kwa maana ya kuwa misimamao yake inaweza kubadilika wakati wowte na vile vile ana visasi moyoni siyo wa kumpa command ya nchi.Mdahalo wa kazi gani? Mwezi ujao hatuendi kuchagua mtu anayeongea vizuri. Hayo tulikuwa tukiyafanya shuleni kwenye 'debating clubs'. Kukiwa na mashindano kati ya shule na shule, kila shule inachagua wale wanaokimwaga Kimombo vizuri kwenda kuiwakilisha shule. Mwezi ujao tunaenda kuchagua mtu wa kutuongoza na kutuletea maendeleo. Tunahitaji mtendaji, Siyo mzungumzaji. Magufuli ameisha dhihirisha utendaji wake. Huenda hana kipaji cha uongeaji. Hata Kimombo chake si kizuri sana kama wapinzani wanavyokazia. Lakini hata kipofu ameona utendaji wake. Anafuatilia mambo yeye mwenyewe. Siku ya kwanza baada ya kushika madaraka aliibukia Hazina kwa kutembea kwa mguu. Siku chache baadaye akaenda Muhimbili ambako kulikuwa na uwozo mkubwa. Mambo yakaboreshwa. Miezi michache iliyopita tulishuhudia akimpagasha Mkuu wa Mkoa wa wakati huo kuhusu kiwanda cha machinjio hapo Dar. Kwa hiyo ameendelea na ufuatiliaji hivyo hivyo tangu siku ya kwanza mpaka juzi aliposikika akimuagiza Mfugale kuhusu barabara ya Kilomita 46 huko Ukerewe. Wengine wakahusisha hilo na uchaguzi ujao ambapo ukweli ni kwamba amekuwa mfuatiliaji tangu siku ya kwanza kuingia madarakani. Lissu ni mzungumzaji tu. Kila kuhutubia kwake amekuwa akijikita katika madhaifu ya Magufuli kuliko kusema atatutendea nini. Hakuna maana kuwadanganya watu kwa maneno mazuri. Hakuna haja kabisa ya mdahalo.
Tundu Lissu si mwanasiasa ni mwanaharakati hilo wengi wanasema, wengi wape.
Nimewahi kusema humu kwamba namfahamu Tundu Lissu vizuri tu na ni mtu wa kawaida sana.
Ni kweli kapata tatizo la ulemavu ambao haijulikani mpaka leo wahusika shambulizi dhidi yake ni akina nani, hivyo mimi siwezi kuliongolea hilo.
Lakini baada ya uchaguzi October 28 Tundu Lissu ataendelea kuwa mwanaharakati wa kawaida akiwa Chadema.
Ila huko mbele atajifunza namna ya kufanya siasa akiwa Chadema.
Soma tena thread hiyo hapo chiniNafikiri ukisoma hapo chini jinsi JokaKuu alivyokujibu utajua kati ya mimi na wewe nani mjinga. Napata mashaka sana kama kweli kazi yako ni kufundisha.
View attachment 1569201
Hahaha mbunge gani amewahi kuona mikataba ya Magufuli?!Kuyatetea kwa nani? Kama mtu anasema kweli anakubali makubwa yamefanyika,ila anataka aone mkataba wa mikopo ya pesa ambazo serikali inakopa. Kwani yeye ni mbunge!
Soma tena thread hiyo hapo chini
Wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye hasira sana kwa sasa
Hakuna niliposema Magufuli na Lissu wanaongea kiingereza sawa, ila nilisema kuwa wote kiingereza chao ni substandard. Iwapo huwezi kuona mapungufu ya kiingereza cha Lissu hayo ni matatizo mengine yako kabisa.
Mara nyingi watu wajinga au wapumbavu ni wepesi sana wa kunyoosha vidole kwa wenzao kuwa ndio wajinga! Hiyo inajulikana kabisa kawenye psychology. ndiyo maana ya msemo wa " Never argue with a fool"
View attachment 1569203
Unazidi kuonyesha ujinga wako unaposhindwa kuelewa maana ya kusema kati yao hakuna bingwa; watoa lugha za matusi na kelele nyingi huwa ni watu wenye akili ndogo sanaYou wrote, "kati yao hakuna bingwa". You clearly tried to imply that Lissu and Magufuli are in the same category. Lissu's command of English might not be perfect but it's far superior comparing to Magufuli.
By the way, don't give me this lecturing bullshit with these quotes. Take them back and shove in your @$$.
View attachment 1569207
Unazidi kuonyesha ujinga wako unaposhindwa kuelewa maana ya kusema kati yao hakuba bingwa
soma tena quote uliyoleta kutoka kwenye simu yako.Ulimaanisha nini?
Unazidi kuonyesha ujinga wako unaposhindwa kuelewa maana ya kusema kati yao hakuba bingwa; watoa lugha za matusi na kelele nyingi huwa ni watu wenye akili ndogo sana
View attachment 1569216
kwani alichoongea hujamuelewa au. Hoja zote alizotoa hujaelewa basi hutakuja kuelewa.Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
Rais Magufuli endelea kuchapa kazi na kuwaletea maendeleo watanzania. Kampeni unazofanya ni kama kutimiza matakwa ya katiba ya JMT, unazunguka kufanya presentation ya mazuri ambayo umewafanyia watanzania.
Itakuwa na mantiki gani kufanya mdahalo na mgombea ambae anasema eti hata wakoloni walijenga barabara! Hivi mwaka 1997 hivi majuzi tu kulikuwa na barabara ya lami hapo kwao Ikungi? Amesahau kuwa ulikuwa unatoka Dar asubuhi na kufika kwo Ikungi saa nne usiku?
Kwa nini Rais wetu kipenzi unayetufanyia makubwa uje ufanye mdahalo na mgombea ambae anadanganya watu eti Rufiji basin ipo eneo la Kitropiki na hivyo uhakika wa kuwa na maji ya kudhalisha umeme ni mdogo!
Hajui kuwa Rufiji river ina matawi ya mito mikubwa kama minne kama mto Kilombero,Ruaha mkuu na mingine mingi,hivyo muda wote wa mwaka una maji ya kutosha!
Rais wetu itakuwa ni kupoteza muda kufanya mdahalo na mgombea ambae anasema mradi kama JNHPP ni White E lephant hivyo hauna manufaa kwa wananchi. Maana ni mradi mkuubwa lakini hauta wanufaisha wananchi. Hivi hajui kuwa gharama za umeme zitashuka na wananchi wa kawaid na wenye viwanda watanufaika! Na hili litapunguza ukali wa maisha!
Itakuwa ni kupoteza muda kufanya mdahalo na mgombea ambae anakubali kweli umefanya makubwa ila anataka uweke wazi hizo pesa ulizitoa wapi. Yaani pamoja na kuwa mgombea wa urais hafahamu kuwa vyanzo vya mapato ni,mikopo,kodi,misaada na fine zinatozwa na serikali. Na haoni aibu kusema eti serikali ikikopa mikataba iwe inawekwa wazi hadi kwenye magazeti.
Itakuwa aibu kwa rais mchapa kazi kama wewe ambae anasema atafuta kodi na kuacha kutoza kodi. Huku akijua hakuna serikali duniani inajiendeha bila kodi. Na hii ni aibu kubwa sana kwa chama chake kuwa na mgombea kama huyu.
Leo ameshuhudia utiaji saini wa mradi wa bomba la mafuta la EACOP nafikiri roho imemuuma sana maana halitakii meme taifa hili.
Maana kama kununua ndege anasema hakuna faida sababu zipo grounded sasa hivi, huyu unafanya nae mdahalo wa nini! Ina maana hajui kuwa ugonjwa wa Covid-19 umesababisha ndege nyingi ziwe grounded. Kwa ujumla usipoteze muda kufanya mdahalo na mgombea ambae saizi yake ilikuwa ni kugombea ubunge.
Tundu Lissu na Magufuli nani aliyekulia kijijini ?? Anaongea kama unaharisha.Huyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao
Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert
Kuyatetea kwa nani? Kama mtu anasema kweli anakubali makubwa yamefanyika,ila anataka aone mkataba wa mikopo ya pesa ambazo serikali inakopa. Kwani yeye ni mbunge!
Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"
=====
LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.
Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.
“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.
Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.
Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.
Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.
Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.
“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.
“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.
Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.
Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.
“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.
Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.
Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Midahalo imekuwa ikiombwa tangu 1995 na haijaweza kutokea.
Kwa iyo magufuli ana vision gani?hewala mzee; mimi ni mwalimu na muongeaji mzuri sana lakini najua kuwa kuwa raisi haihitaji sifa ya uongeaji bali kichohitajiwa ni vision, decisiveness na fairness. Mtu asiyekuwa na vision kuwa anataka kuipeleka wapi nchi na hayuko decisive kwa maana ya kuwa misimamao yake inaweza kubadilika wakati wowte na vile vile ana visasi moyoni siyo wa kumpa command ya nchi.