Tundu Lissu: Filamu ya Royal Tour ni biashara kubwa Amazon. Je, nani mwenye hakimiliki? Mgawo wetu ni kiasi gani?

Tundu Lissu: Filamu ya Royal Tour ni biashara kubwa Amazon. Je, nani mwenye hakimiliki? Mgawo wetu ni kiasi gani?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Ameandika Tundu Lissu katika akaunti yake ya Twitter

Movie ya Royal Tour kumbe ni biashara kubwa Amazon. Kukodi Sh. 13,930, Kuuza sh. 37,150. Swali langu ni je, mwenye hatimilki ya movie - & kwa hiyo mmiliki wa pesa hizo - ni nani? Je, mgawo wetu ni kiasi gani kwa vile main character ni Rais wetu & location ya movie ni mbuga zetu?

Royal.jpg
 
Kama tunapata % tu nitamdharau sana bibi Hangaya, nikiangalia ule msafara na posho walizokuwa wakilipana watu kwa siku wakati hiyo filamu ikirekodiwa, kwamba serikali ndio imegharamia halafu sisi tusipate chochote narudia tena nitamdharau sana huyu Bibi.
 
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepanga katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
 
hii tumepigwa asubuhi tu bado vipande vitakavyotumika kutengenezea filamu nyingine na vitabu vitakavyoandikwa kutokana na move hiyo vyenye pande mbili positive na negative kweli watanganyika ni wadanganyika
 
Kama tunapata % tu nitamdharau sana bibi Hangaya, nikiangalia ule msafara na posho walizokuwa wakilipana watu kwa siku wakati hiyo filamu ikirekodiwa, kwamba serikali ndio imegharamia halafu sisi tusipate chochote narudia tena nitamdharau sana huyu Bibi.

Serikali haikutoa hata senti moja. Wamesema ni fedha za wadau wengine.
 
  • Thanks
Reactions: Yhy
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepangwa katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
Kila kitu unageuza siasa, watu wanaongelea jambo serious wewe unaongea upupu.
Shubamit
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho mwaka 2020, Tundu Lissu amehoji nchi yetu inapata kiasi gani katika filamu ya Royal Tour

Amehoji hayo baada ya kukuta filamu hiyo ikiwa inauzwa na kukodishwa katika mtandao wa Amazoni

Kupitia Twitter ameandika “Movie ya Royal Tour kumbe ni biashara kubwa Amazon. Kukodi Sh. 13,930, Kuuza sh. 37,150. Swali langu ni je, mwenye hatimilki ya movie - & kwa hiyo mmiliki wa pesa hizo - ni nani? Je, mgawo wetu ni kiasi gani kwa vile main character ni Rais wetu & location ya movie ni mbuga zetu?”

2635CB50-CE1B-4D1E-B9FF-AC52F0D1FF01.jpeg
 
Wataalamu wa biashara za mitandaoni njooni huku sitaki watu waliosoma degree za kawaida za business hata ziwe PhD au waliosoma somo la business kama somo kwenye digrii zao

Nataka pure expert wa online business wajibu hili la mleta mada
 
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepangwa katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
Out of context, zinaongelewa pesa za umma sio za ponjoro.
 
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepangwa katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
Wewe kweli ni Ki
 
Kwani mliwekeza kiasi gani kwenye hiyo project?
 
Hiyo filamu kama filamu nyingine. Jamaa walilipa Kila kitu Kwa serikali wakati wanatengeneza hiyo filamu hat Ile misafara na per diem za wafanyakazi zote zililipwa na mtenegeneza filamu. Hivo Nina uhakika atakua ana Haki zote za filamu au Kun %kadhaa serikali itapata
Rais Samia: Royal Tour, tulitumia kama bilioni 7 gharama za kila kitu
 
Back
Top Bottom