Tundu Lissu For Nobel Prize 2026 Tumuunge mkono

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,759
Reaction score
4,872
Pamoja na kunusurika ktk jaribio la kifo, pamoja na mateso yote ya viongozi tulionao kwa sasa, na wafuasi wake kufuatiliwa kwa nguvu zote na vyombo vya dola, bado Tundu Lissu anaonesha anapigania haki za watanzania. Labda wengine wanaona kama mpigananji wa CHADEMA, lakini Huyu m-TZ anastahili heko na shukrani ya pekee ktk bara hili.

Wa-TZ tunaungwa mkono na kumtetea Lissu kutokea Jumuiya ya nchi za Ulaya. Kwa sasa tuandike kwa wingi wetu ili aangaliwe kupata zawadi ya Nobel ya amani kwa mwaka ujao wa 2026. Huenda litakuwa fundisho kwa wanaopanga mauaji ya raia wao mitaani.
 
Jamaa ametufunulia mambo mengi sana ya hovyo yanayotokea kwenye nchi, kiufupi nami naunga mkono hoja na Mungu amtunze sana kwenye hiki kipindi kigumu anachopitia
 
Na wewe umemkubali?
 
Kwa lipi?
 
Kwa kitu gani afikiriwe kwa Nobel? Unafahamu criteria zinazotimika?
 
Ngoja tuone majina ya wagombea ndio tuone yupi kati ya hao anatufaa zaidi.
 
kaa kimya inaonyesha ulivyo mpumbavu serikali inamuweka ndani Lissu uchaguzi mpaka upite alafu unasema tunamkuza sisi serikali yenyewe inamuogopa unaleta chuki zako hapa
Inamuweka ndani kwa sababu ya Kamdomo tu. Lissu yupo overrated sana na nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…