Fortilo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 5,807
- 17,416
Tukisema kiongozi anapimwa kea perfomance na sio blabla muwe mnatuelewa.
Toka uchaguzi wa vyama vingi 1995, na Tundu Lissu kujiunga CHADEMA kama mwanachama Muandamizi, takribani miaka 30 sasa.
Singida haijawahi kuwa na mbunge yeyote wa Upinzani ukiacha yeye mwenyewe Tundu Lissu jimboni kwake Singida Mashariki.
Nadhani ndie mbunge pekee ambae Kanda yake haina mbunge hata mmoja wa Upinzani ukiacha Morogoro.
Pamoja na ushawishi wake kwanini wananchi wa maeneo anayotoka hawamuelewi?
Sio Dodoma sio Singida Mambo manne;
1. Hapendi kusaidia wengine
2. Anawadharau wengine
3. Hakubaliki kwao ukiacha jimboni kwake pekee.
4. Hafanyi kazi za chama ipasavyo.
Majimbo nane yeye ana score ya 1/8 alafu analeta hoja za kujenga chama? Unajenga vip chama wakati huna historia hiyo?
Tofaut na Mpinzani wake mkuu, Freeman Mbowe... Ameijenga ipasavyo Kaskazini na zaidi mkoa anaotoka kuna kipindi alikuwa na wabunge 8/9.
Anaongea sana lakini anazidiwa Mbali sana na Heche, Sugu, Mnyika, Bony Yai, Wenje, na viongoz wengine wasio na majigambo lakini kazi zao zinaonekana.
Lissu sio mchapa kazi kama anavyojitapa? Kama hilo dogo anashindwa ataweza vipi kujenga Chadema nchi nzima?