LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Iko hivi, Singida haina amshaamsha ya upinzani kama mikoa ya kilimanjaro, arusha, mbeya, kigoma, lindi, mtwara na mara. Singida huwa wanaona ukichagua upinzani ni kuleta vurugu. Singida wanachojua ni CCM tu ndivyo mentality yao ilivyojengeka. Jimbo la singida mashariki anakotoka Lissu ndilo lilikuwa na amshaamsha ambaye yeye alisimamia shoo hiyo. Baada ya kupata matatizo yale upinzani ulilegea wengi walirudi ccm waliona isiwe taabu. Hayo majimbo mengine ya mkoa wa singida Lissu hakuwa na ushawishi huko, cheki majimbo ya manyoni yote mawili ni ccm tu imetamalaki huko. Iramba yote pia hakuwa na ushawishi mkubwa. Ukiangalia kanda ya kati yote ni ngome ya ccm, haina upinzani. Kuna dhana kuwa nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao.