Sawa ila kama Lissu hafai hata kwa 20% then Maguguli yupo kwenye 0%he is real incomplete na anaficha incompetence yake kwenye ukali na the so called kuabana matumizi ndo maana hasafiri .anashindwa kujua kuwa kuna mambo baba unatakiwa ukafanye mwenyewe na si kutuma mke au mtoto
sawa hayo ni maoni yako....Rais Magufuli alichokifanya yeye alipoingia madarakani tu ni kuwakumbusha watendaji wote wa serikali na taasisi zake pamoja na wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa nchini....kitu ambacho ilifika hatua ambayo kila kiongozi mahalin pake pa kazi anaamua yeye nini afanye bila kujali sheria zinasemaje na ndiyo maana wengi wetu sasa wanaona kuwa ofisi za umma kwa maana ya serikali kwasasa zinatoa huduma kwa mujibu wa sheria na hakuna mtu ambaye anaonewa kila mmoja anapata haki yake.
tumeona watendaji wengi wamepoteza nafasi zao za kazi kwasababu ya kufanya kazi kwa mazoea na wengine wameacha kazi kutokana na kujua kabisa hawezi kuendana na jinsi Rais anavyotaka yote hayo ni kusimamia sheria na uwajibikaji.
Tumeona wengi tu wako magereza wakiwa wamefungwa au kuendelea na kesi zao za ufisadi na wizi ndani ya serikali.tumeona jinsi alivyodhibiti matumizi mabaya ya serikali kwa watendaji wa serikali ambao walifika mahali kuona kuwa pesa za serikali ni kama pesa zao ni kuchukua na kutumia wanavyotaka leo hii hilo utalisikia kwenye ndoto na hao wengi wanamchukia RAIS KWASABABU WALISHOZOEA KULA KIRAHISI TU PESA YA UMMA.
Uliona wapi kiwanja cha heka moja kinanunuliwa kwa million 600 hapa nchini lakini watendaji wa serikali wamenunua hivyo tena mkoani mashambani kabisa si maajabu ya dunia hayo.
Unasema kana mambo baba inabidi afanye mwenye na asitume mtoto.....RAIS Magufuli amekwenda mwenyewe maeneo mangapi hapa nchini na kukuta madudu tu huko na kuamua nini cha kufanya.
Unakumbuka ziara za bandarini mara ngapi amekwenda na kuona mambo ya ajabu ambayo ndiyo ulikuwa utamaduni wa watenda wa huko kushirikiana na makumpuni machafu katika kukwepa ulipaji wa kodi na kupitisha mizigo bila kulipa chcochote pale bandarini.leo waliokuwa wamezoea kufanya huo uhuni pale bandarini wanalia tu njaa kila siku mitaani.
Tumeona pale airport watendaji wakiacha tu mizigo kupita bila ukaguzi kwenye scanner zilizopo huku wakisema zinafanya kazi wakati hazifanyikazi na rais kuchukua maamuzi...umeona sasa Muhimbili ilivyo tofauti kabisa na ilivyokuwa nenda hata sasa kaangalia pale kama utaona mauchafu yalivyokuwa na wogonjwa kulala chini tena.
Tatizo kubwa la sisi watanzania ni kupenda mtelezo,bure ubwete urahisi mteremko harakaharaka starehe kutofanya kazi dezo utajiri pasipo jasho short cut na mengine mengi tu yanayofanana na hayo.
TUBADILIKE FIKRA ZETU TUTAFANIKIWA KIMAENDELEO.......Lissu ni mtanzania kama watanzania wengine hana miujiza yoyote zaidi kutafuta umaarufu duniani na ndiyo maana anaeneza propaganda ambazo hazipo Tanzania ili walimwengu waamini......sawali moja ameulizwa ktk mahojiano yote ya BBC,DW na VOA kuhusu mazuri ya serikali lakini amekuwa akijibu kwa kebehi....wewe tafuta clip zake umsikilize kwenye hilo swali.