LGE2024 Tundu Lissu: Hata mje na mabomu, mabunduki na magari yenu ya vita, kesho tutawashinda!

LGE2024 Tundu Lissu: Hata mje na mabomu, mabunduki na magari yenu ya vita, kesho tutawashinda!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mambo yameendelea kuwa sukari huko Singida kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Lissu akiwa anazungumza leo Singida amesema kuwa CHADEMA itashinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa haki na hata kukiwa na bunduki pamoja na magari ya vita bado tu watashinda.
"Nyie Mapolisi mnaoambiwa mkatishe watu mkapige watu na mabunduki miaka 10 iliyopita hao waliotuma kuja kuumiza watu tuliwaaachia vijiji vitatu tu. Na kesho tutawapiga. Kesho tutawashinda. Mje na mabomu yenu. Mje na magari yenu ya vita. Mje na mabunduki yenu kesho tutawashinda"
PIA SOMA
- LGE2024 - Tundu Lissu: Kama Mnaogopa Mabomu, Mkalale Mshughulikiwe na CCM. Ukiogopa Mabomu Kalale Uchunwe Ngozi na CCM
 
..wanaotuma askari wenye mabomu na mabunduki ndio wamepoa au wako baridi kisiasa?

..hivi kwanini hawatumwi Mzee Hafizi na Abduli badala yake wanatumia vijana wa kimasikini wa Kitanganyika?
jeshi liko kulinda raia na mali zao...doria kuimarishwa shida iko wapi
 
..labda mali za genge la watawala wa Ccm.

..wengine wote tunaishi kwa kubahatisha.

..Na wakikuhisi vibaya wanakupoteza.
amani nchi hii ni ya kutosha utawala wa sheria ni wakutukuka

wengi ulimwenguni wanajifunza kwetu na wengine watataka kupenyeza vijichokochoko ndugu

ondoa wawazo hasi kwa watawala wako uko mikono salama
 
amani nchi hii ni ya kutosha utawala wa sheria ni wakutukuka

wengi ulimwenguni wanajifunza kwetu na wengine watataka kupenyeza vijichokochoko ndugu

ondoa wawazo hasi kwa watawala wako uko mikono salama

..hukumsikia mtoto wa Mzee Kibao alichokisema?

..wao waliishi kwa imani kuwa wanaotekwa na watu fulani tu, wao hayawahusu.

..endelea kuamini uko salama, ila siku watawala wakikuhusi ndivyosivyo utajua kuwa hujui.

..Ni mpaka waliposikia Mzee wao ametekwa. Na mwili uliopatikana ulionyesha alikuwa ameteswa, macho yametobolewa,na amemwagiwa tindikali.
 
Back
Top Bottom